Mpendazoe aanika walioanzisha CCJ

Hawa wanasiasa wananichanganya hata siwaelewi..huyu mpendazoe nae anakurupuka sana.
Mkuu si kukurupuka huu ndo muda muafaka kuwaumbua, akina Sitta walikuwa kwenye sherehe kufanikiwa kuwavuruga akina Lowassa, sasa CDM wamewapiga kuwavuruga zaidi.

Hii ni furaha kwa kina Lowassa hivyo hapo CCM inazidi kubaki halijojo. Lakini pia hawa wakina Sitta ni wanafiki, mara nyingi wanakuwa wakali maslahi yao yakiguswa na wanatumia uchafu wa wenzao si kwa maslahi ya taifa rejea issue ya Richmond uwajue vizuri hawa watu na sasa CCJ yale yale!
 
Hawa wanasiasa wananichanganya hata siwaelewi..huyu mpendazoe nae anakurupuka sana.

huwezi kuelewa kwasababu uwezo wako wa kuelewa mambo ni mdogo sana, hata mwalimu anapofundisha sio lazima waelewe wote.
 
Reactions: LAT
wakuu hii habari inazidi kuwavuruga ccm,fikiria akina sitta na lowasa na mkulu na wale fata upepo meza moja nini watazungumza as a team?
 
Mpendazoe aliwahi kuulizwa kama yeye ni mwanzilishi wa CCJ akasema hapana,leo anasema yeye ni miongoni mwa Wanzilishi! Hopeless kabisa!
umetumwa na nape? kazi unayo hoja imeeleweka sana kwamba nape,sitta,mwakyembe ni wachumia tumbo tu wanapiga kelele ili wapate nafasi wakipewa wanakaa kimya
 
wakuu hii habari inazidi kuwavuruga ccm,fikiria akina sitta na lowasa na mkulu na wale fata upepo meza moja nini watazungumza as a team?
Tena as team mazungumzo yawe ni jinsi ya kuidhibiti cdm na other national interest unafikiri watawaza na kutenda as a team tena? Maana hapa walipo hakuna unafiki tena lazima kundi moja linyanyue mikono juu na lingine lisamehe! Hayo yanawezekana?
 
Wakati ule alibembelezwa awataje akagoma,kwa sasa ni wrong time.Ni sawa na hadithi za kufikirika.Mi namuona sawa tu huyo Nape.Je CCJ ingeandikishwa angekua CDM?

Nadhani amesema kuwa CCJ ilikuwa iungane na CDM kupambana na ufisadi. Na ndio maana CDM ilijivuta kumtangaza mgombea wake wa uraisi, ni baada ya uasi huo wa kina Six na Mwakyembe, ngoma ilibidi ibadilishwe na Dr Slaa akaangukiwa ili aache kugombea ubunge ambapo alishachukua hata fomu akagombee uraisi. But nadhani mvuto wa Dr Slaa ni mara mia mbili ya hao kina Six na Mwakyembe, ooh na Nape loh, and i think CDM walifanya busara sana kumteua Dr Slaa

Nadhani Mpendazoe ni mzalendo wa kweli. Aliacha hata kiinua mgongo chake. But Nape alisema wamuulize Mpendazoe CCJ ilikufaje? Hilo ndo jambo la kujiuliza
 
Jamani hivi CCM huko kinatenda mambo yake kichama au kila mtu kivyake vyakena wanaunganishwa na ufisadi na sare ya kijani?

Ukichunguza kauli za viongozi wake kuanzia JK utagundua ya kua hotuba zao haziandaliwi kwa makini au hakuna maadalizi yoyote kila mtu anazungumza linalomuijia kinywani nyingi zimejaa ubabaishaji na hazina mantiki.Mfano mzuri jaribu kuipitia hiyo katibu Mkuu wa CCM Mukama mwanzo nilikua nafikiri ya kua tatizo ni Makamba sasa nimegundua ya kua tatatizo ni CCM yenyewe yoyote atakaebadilishwa katika nafasi hiyo ya ukatibu bado atabaki "MAKAMBA"Nawashauri waache kutumia cheo au jina katibu Mkuu badala yake watumibe MAKAMBA ,Makamba, Makamba wa pili.......n.k.Anaposema CHADEMA wanabeza kwao kujivua magamba na kwamba wanasema ya kua CCM inasema uongo.

Hapa anaesema uongo ni nani?Magamba gani waliyoyavua tangu kutangazwa dhana hiyo?Anakanusha na wakati huohuo kubali ya kua CCM kuna wafanyabiashara wanao kitumia chama kwa manufaa yao binafsi.Hapa nani muongo,kua na wafanyabiashara katika chama sio makosa, makosa ni kwa wafanyabiashara hao kukitumia chama kutuibia rasilimali zetu.

Anaposema ya kua CHADEMA wanambeza Baba wa taifa kwa kutembelea makaburi ya baba wa taifa Mwalimu Nyerere wakati wanatenda kinyume chake.Hapa nani anaetenda kinyume na maadili ya Baba wa taifa CCM au CHADEMA? CHADEMA kinapigania walalahoi, rasilimali za taifa na kuwakomboa walalahoi kutoka katika umasikini uliopindukia(Elimu,afya,malazi n.k)Ambao ndio ulikua msingi mkuu katika vitendo vyake.

CCM kujilimbikizia mali kwa viongozi wake na familia zao kwa kujinufaisha na rasilimali zetu na ufisadi.Ushauri wangu " CCM ikome kuitisha mikutano au maandamano na wananchi lau wakifanya hivyo waviachie vikundi vya usanii kutumbuiza kwani kwa sasa hawana cha kuwaambia wananchi,badala yake wafanye vikao vyao vya ndani na kujadili nini cha kufanya na nini cha kuwambia wananchi"

MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
Mtu akimwaga ugali, wewe unamwaga mboga, haya sasa tuone nani atalia zaidi!
 
Hapa sasa mambo yanaelekea kuiva,hoja hiyoooo magamba mnatakiwa kuijibu.
 
Mpendazoe anawataja sasa hivi kwa faida ya nani? Mbona wakati anatoka CCM hakuwataja wenzake. Haya na aseme ni nini kuliwazuia kumfuata. Au walimpiga changa la macho, wao walitaka kuona ni nani CCM damu.
 
Mpendazoe, kada wa ccm, ccj na sasa chadema, natafuta maana ya kada
 
hilo gazeti limeona aibu kuwataja wote ni hawa hapa SITTA,MWAKYEMBE,MWaMbAlASWA,NAPE na yeye mwenyewe MPENDAZOE
 
Siasa mbaya sana, inabidi ukiingia uwe umejipanga vizuri
 
Mapacha watatu wameshashinda vitani bado asubuhi. Hao kina Mwakyembe na Sitta wana nini kipya kwa sasa? Siasa ya bongo bwana.
 
Hayawi hayawi sasa yamekuwa, kumbe magamba mengi loooh CCM kazi wanayo mwaka huu
 


hahaha...wanajaribu kutisha wananchi?!
 
Wakati ule alibembelezwa awataje akagoma,kwa sasa ni wrong time.Ni sawa na hadithi za kufikirika.Mi namuona sawa tu huyo Nape.Je CCJ ingeandikishwa angekua CDM?

Mpendazoe aliwahi kuulizwa kama yeye ni mwanzilishi wa CCJ akasema hapana,leo anasema yeye ni miongoni mwa Wanzilishi! Hopeless kabisa!
Jibuni hoja katibu mwenezi wa CCJ Nape lini alijitoa CCJ siyo kutuletea story za zamani hapa.
 
Sitta, Mwakyembe, Nape n.k wote wanafiki tu
Tatizo la wanasiasa wa TZ ni njaa, wanapiga kelele ili wapewe ulaji. Nape alipigia kelele swala la mradi wa jengo la umoja wa vijana akapewa Ukuu wa wilaya- akafunga mdomo. Sitta na mwenzake walishikilia Richmond- wakapewa ulaji-wako kimya na leo hii wanafanya kazi na Dr. Hosea na aliyekua N/Katibu wizara ya nishati ambao walipendekeza wafukuzwe kazi.
Ni wanasiasa wachache wakuweza kuaminika.😛ound:
 
Aisee sikujua kama Mpendazoe sio mtu makini kwa kiwango hiki, uchungu mwingi moyoni uliotokana na kuruka melini mapema na kisha kupotezwa na mawimbi umempunguzia busara na ufahamu.

Pole sana mpendazoe, ni ajabu sana kwa Chadema kuanza kuwataja wasaliti wa wapinzania wao CCM,eti ili CCM iwajue wale wanaowasaliti ndani yao...inatia shaka sana hii , sasa nauona kwa mbali ule ushirika usio mtakatifu kati ya mapacha watatu na chadema kama ulivyotangazwa na Nape.

Hii sio news kwa CCM, wanachotakiwa kufanya akina Sitta ni kutojibu in detail kuhusu CCJ bali kuutangazia umma kwa urefu kuhusu ushirika wa Chadema na Mafisadi katika kufanya lolote litakalosaidia kuwanusuru Mafisadi, mahakama ya umma itaamua in favour of either Wapiganaji au Chadema+Watuhumiwa wa ufisadi, usinipe jibu!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…