Elections 2010 Mpendazoe aangushwa kinyang'anyiro cha ubunge segerea

Mutu

JF-Expert Member
Mar 30, 2008
1,329
47
Aliyekuwa Mbunge wa Kishapu CCM na baadae kukihama chama hicho na kuhamia Chama mfu CCJ na kuhama tena CCJ kwenda CHADEMA, Freddy Mpendazoe leo hii amebwagwa vibaya katika kura za maoni kuomba ridhaa ya wajumbe ya kugombea ubunge jimbo la Segerea.Katika uchaguzi uliofanyika ukumbi wa baa ya Seper Karatu Ukonga na kukamilika jioni hii Mpendazoe ameangushwa vibaya na Mwanamama Rachel Mashishanga kwa zaidi ya kura 20, Rachel Mashishanga amepata kura 48, ikiwa Fred Mpendazoe akiambulia kura 28 tu. Kwa matokeo hayo Rachel Mashishanga ndiye Mgombea ubunge jimbo la Segerea jijini Dar es Salaam kwa Tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)



SOURCE:mjengwa
 
Basi labda akazane kumpigia bede Slaa ,akiwa rais kuna ubunge wa kuteuliwa na mengineyo ya kuweza kumtumia anapofaa sio kwa kununeo huruma bali kwa uwezo wake.

Wajuvi wa mambo mnasemaje?
 
Hayo yatakuwa ni majaribu makubwa sana kisiasa! Itabidia aonyeshe mshikamano, sio tena kuhamia chama kingine!!
 
Basi labda akazane kumpigia bede Slaa ,akiwa rais kuna ubunge wa kuteuliwa na mengineyo ya kuweza kumtumia anapofaa sio kwa kununeo huruma bali kwa uwezo wake.

Wajuvi wa mambo mnasemaje?

LOL..

Hii dhana ya wabunge wa kuteuliwa ni kichekesho kikuu. Hivi hawa wabunge wa kuteuliwa huwa wapo loyal kwa nani haswa?
 
Mpendazoe anatakiwa sasa atulie ajijenge vema ndani ya chama. Kukosa na kupata ni sehemu ya maisha ya kisiasa na hata yote kwa ujumla. Akianza kuroroma atakwisha vibaya sana. Namheshimu Mpendazoe kwa jinsi alivyolishikia bango swala la Mkapa kujiuzia mgodi wa Kiwira. Hakutetereka kusema wazxi bungeni, wengi walikuwa wanaogopa sana. Fred, usilalame, ungana na kampeni ya Chadema mchukue nchi.
 
Ningeshangaa sana endapo CHADEMA wangempa ridhaa Mpendazoe.
Yaani ndani ya miezi michache tayari kawa mwanachama wa vyana vitatu.
Ni dhahiri nia yake ni madaraka tu na hakuna kingine.
 
Natumai sasa atatulia na kukijenga chama,kwake litakuwa funzo zuri la kujipanga upya na natumai katika uchaguzi ujao atakuwa amejijenga,sasa ni wakati wake wa kumsaidia Dr Slaa katika kampeni
 
kuhamia chama fulani sio tiketi ya moja kwa moja kugombea ubunge! akitumikie chama kwanza baadae akionyesha ukomavu atapewa ridhaa, hili ndio liwe fundisho kwa wakurupukaji wote kudadadeki!
 
Kwa kweli anatakiwa kutulia kwanza maana na kuzoeleka kwenye chama, na huyu mtu anaitwa Malaria Sugu nafikiri anamatatizo fulani kwenye ubongo wake wa kushabikia saana Chama cha mafisadi, hembu tueleze mwenzetu wewe unafaidika na nini katiaka nchi hii na serikali yake maana tunaona kukicha maisha yanakuwa magumu na hakuna mikakati ya maksudi kuinua halai ya maisha ya watanzania wenye kipato cha chini
 
Back
Top Bottom