Mpe mtoto au mbwa jina baya limharibu/ Give a child or a dog a bad name and spoil it

CalvinKimaro

JF-Expert Member
Sep 11, 2017
244
312
Hakika Chadema inateseka kutokana na kaulimbiu na tambulisho inazotumia!

Makamandaa kunja kunja kunja ngumi! Bado sijaona/sijasikia! piiipoooz, pawa! Sasa ni NO HATE NO FEAR!

Ni majina mabaya ambayo baba "mwamba" anayafyatua kadri atakavyo bila kuwaza vyema!

Tatizo hili liliwahi kuikumba CUF. Ule utambulisho wa NGANGARI. Wakakutana na NGUNGURI. Matokeo yake jina likafanya watu wauane na wengi wao wakimbilie shimoni Mombasa na Darfur! Akili ikarudi kuwa jina sio zuri, wakajikita kwenye "HAKIIIIII SAWA KWA WOTEEEE"! Salama ikawajia.

Jina umpalo mbwa au mtoto humuongoza katika utendaji/maisha.

Kama Chadema hawatang'amua umuhimu wa jina au utambulisho basi wafuasi na viongozi wao watatenda na kunena mambo ya hovyo mno!

Huu ujinga wa hivi karibuni ni kiashiria chema cha jinsi utambulisho au jina linavyoitesa Chadema! NO HATE NO FEAR imeanza kuzaa matunda yenye miiba! Matunda machungu mno!

Bora hata jina lingekuwa fupi: NO HATE!
Lakini NO FEAR ndio imepelekea watu kuacha shughuli zao kwenda kugombana na polisi Kisutu! Ndio hiyo hiyo NO FEAR imepelekea watu kupata akili ya kwenda kugombana na askari magereza Segerea! Eti kupokea mfungwa kwa maandamano! Jina linawatesa!

Baba kawakatia mbwa/watoto wake majina mabaya! Chausiku, Ubaya, Selasini, Cheusi, Kadogoo, Cheupe, Pesambili, n.k. Sasa mbwa anauma hadi wageni wake!

Majina mazuri yapo! Jaribu kutizama slogan ya Republicans na Democrats kule US?

Jaribu kutizama za Conservative na Labour kule UK? Haya rudi Tanzania angalia HAPA KAZI TU? Walau nenda kwa Odinga tizama slogan? Unaona nini?

Je, unakumbuka slogan ya kina Zuberi Mtemvu au hata ya Oscar Kambona alipokimbilia London? Ziliwatesa sana! Jaribu kukumbuka majina ya watawala wa kale walioisumbua dunia? (Tafiti usitake utafuniwe kila kitu!!!).

Mwite mwanao jina jema kama Yahya/Yohana uone atakavyofanikiwa maishani!!! Ndio maana PAPA YAHYA/YOHANA II anakumbukwa sana duniani!!!!! Mwite mwanao YESU/ISSA uone atakavyonyooka kimaisha! Nadra sana jina zuri kuharibu mtoto!

Baba anapaswa kubadili majina ya wanawe na mbwa wake ili nyumba ibaki na amani. Ama sivyo hili la NO FEAR litawaletea majonzi makubwa zaidi hasa mwaka huu wa njaa!

Huu ni ushauri usio na malipo lakini muhimu sana mwaka huu! CHADEMA jina linawatesa!

Onyo: Fikiri kifalsafa ndio utaelewa😄😀😂Kama umekatiwa jina baya jitahidi sana kuelewa hii hoja!
 
Back
Top Bottom