mpasuko sehemu ya haja kubwa

youngforeva

Member
Apr 26, 2011
25
1
jamani naomba msaada wenu,maana mwenzenu nilikuwa najisaidia sana choo kigumu hadi nikapata mpasuko katika sehemu ya haja kubwa,nilielekezwa kutumia vidonge vya ANUS but ilinisaidia tu kukata damu iliyokuwa ikitoka nikijisaidia,,but mpasuko bado upo na mda fulani wanipa maumivu makali wakati wa kujisaidia,,,,mwenye kuelewa tiba please anisaidie au anielekeze wapi naweza pata mtaalamu
 
POLE MKUU ,ILA UMEFANYA JAMBO JEMA KULETA HAPA MaDAKTARI WETU HAPA JF WATAKUSAIDIA SASA HIVI NA HII ITASAIDIA WENGINE WENGI WANAOONA AIBU KUSEMA.

MADAKTARI HESHIMA KWENU ,TAFADHALINI MSAIDIENI NDUGU YETU

POLE SANA
 
Tatizo la muundo huu huwa lipo sana tu na ni lakawaida kama ni lile ninalo lifahamu mie,huwa linapotea baada ya muda so kuwa mvumilivu ila epuka vyakula vinavyoweza kupelekea wewe kupata haja ngumu kama mapera nk!Kunywa maji ya kutosha baada ya kula na penda kushushia msosi kwa matunda kama mapapai,tikiti maji na tango yatasaidia kulainisha haja!Pole sana mgonjwa si tatizo la kukuumiza kichwa hilo!! NB:Mimi si daktari bali naongea kutokana na experience ya tatizo husika kama ni lile ninalokumbana nalo mara kwa mara!!!
 
Jichunguze Usije ukawa na tatizo liitwalo Rectal prolapse....Google hiyo litu uisome!
 
Wewe unahitaji kufanya colonoscopy..nenda aghakan pale..lakini ni ghalama kidogo, jiandae kama 600,000

pole sana..na kunywa sana maji na matunda mkuu
 
jamani naomba msaada wenu,maana mwenzenu nilikuwa najisaidia sana choo kigumu hadi nikapata mpasuko katika sehemu ya haja kubwa,nilielekezwa kutumia vidonge vya ANUS but ilinisaidia tu kukata damu iliyokuwa ikitoka nikijisaidia,,but mpasuko bado upo na mda fulani wanipa maumivu makali wakati wa kujisaidia,,,,mwenye kuelewa tiba please anisaidie au anielekeze wapi naweza pata mtaalamu

Pole mkuu, unaweza kuwa na tatizo la ANAL FISSURE, fika hospital kumwona daktari wa upasuaji. Kama upo Dar, nenda Tumaini hospital mara nyingi surgeons wa muhimbili jioni wanakuwa hapo.
 
Pendelea sana kula mkuu bt jitahdi kula matunda hasa papai, tango na kunywa maji mengi pia ili kulainisha haja kubwa(gogo).
 
Back
Top Bottom