Mpango wa kuboresha elimu Arusha

Mpango wa kuboresha elimu Arusha

Itoye

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2017
Posts
531
Reaction score
1,026
Wakuu Salaam.

Katika maadhimisho ya "Karume Day" Mkuu wa mkoa wa Arusha alipokuwa akitoa hotuba yake ktk uwanja wa Sheikh Amri Abeid, aligusia suala la ku-adopt mfumo wa kuwa na mtihani mmoja kwa kila somo kama jinsi mitihani ya taifa ilivyo, lakini hii itakuwa kwa ngazi ya mkoa wake wa Arusha kwa shule za msingi na sekondari za serikali.

Lengo kubwa likiwa ni kuendelea na harakati za kuboresha elimu na hii ikiwa kama njia mojawapo na hapa alilisisitiza kuwa hili litawabana wale walimu ambao hawafundishi na kumaliza syllabus kama inavyotakiwa na kwa muda husika na wanapotunga mitihani wanatunga kwa yale tu waliyofundisha na kufanya wanafunzi waonekane wanaufaulu mzuri kwa ngazi ya shule lakini unapokuja mtihani wa taifa wanafeli vibaya maana wanakutana na mambo ambayo hawakujifunza ingawa yamo ndani ya syllabus.

Binafsi naona jambo hili ni jema ingawa tunasubiri matokeo yake maana alisema mfumo huu utaanza kutumika kuanzia mitahani ya nusu muhula maana yake mwezi huu wa June 2018. Mikoa mingine ni vizuri wakaumiza vichwa na kubuni mambo mbalimbali yatakayosaidia kuboresha elimu kwa njia ambazo ni za kistaarabu, kiungwana na kitaaluma ili mwisho wa siku kila mtu ajikaange kwa mafuta yake mwenyewe.

Kila la Kheri Mh. Gambo katika kuwatumikia wananchi wa Arusha.
 
Back
Top Bottom