Wakati wa mkutano wa UNGA mataifa au mashirika mbalimbali hutumia ile platform kupush agenda zao mbalimbali ambazo wao hudhani zinaweza pata attention ya kidunia maana ni likely dunia nzima huwa Newyork for the time being.
Mfano UNGA session ya Mwaka huu ambayo ni ya 81 agenda zilikua nyingi sana ikiwemo masuala kuhusu IRAN, Palestine, Cuba etc katika geopolitics na masuala kama ulazima wa dunia kukusanya USD 3 Billion kwa ajili ya elimu bora kwa watoto 750 Million kutoka Nchi masikini duniani ambayo ilikua agenda ya Italy, Nigeria na Global Partnership for Education, GPE.
Katikati ya hizi agenda Tanzania nayo ilikua na agenda yake ambayo iliita TRIPLE ZERO au Three Zero Health Iniative ambayo imeripotiwa na vyombo vyote vikubwa duniani kama one of the best initiative kuwa presented katika UNGA Session ya 81 ambapo kimsingi here is what it real means;
Rais wa Tanzania Dkt. SSH na Serikali yake katika angle ya kimataifa alishaamua kupaint legacy yake katika maeneo mawili makubwa kuelekea 2030 ambayo ni: 1. Akumbukwe na dunia kama champion wa Afya ya Mama na mtoto na kwamba she 's ready to go extramiles trying to defend this course. 2. Dunia ije imkumbuke kama champion wa nishati safi clean energy na upatikanaji wake (access) katika bara la Africa, na sasa basi;
Katika UNGA 81, Tanzania iliwasilisha hoja ya ulazima wa dunia kuhakikisha kwamba ifikapo 2030 iwe ime achieve malego ya sifuri 3 yaani vifo sifuri vya mama na watoto vitokanavyo na uzazi, pili case sifuri za wamama kujifungulia majumbani au mazingira yasiyo salama na zero case ya mtoto kukosa esseential vaccines etc.
Basis ya hoja ya SSH ni kwamba Africa ndio victim mkubwa wa neonatal deaths/vifo vitokanavyo na uzazi na ambavyo kama facilities na mazingira yangekua sawa basi vingeweza kuepukika ambapo kwa data za CDC zaidi ya 70% ya vifo hivyo vinarekodiwa Africa na yeye kama mshindi wa Tuzo a prestigious Global Goalkeeper Award kwa sababu ya efforts zake kwenye hili eneo akaona ni vema alibebe kama agenda yake katika UNGA 81.
Tanzania as of now kwa kipindi cha miaka kuanzia 2015-26 imepunguza idadi ya vifo vitokanavyo na uzazi for up to 81% making it the right voice ku-champion "Tripple Zero" Health Initiative mbele ya majukwaa kama UNGA. Tatizo langu pekee ni sijui kwanini jambo hili limeripotiwa kwa ukubwa sana media za nje
kuliko zetu.