Mpango mpya wa usalama wa Marekani ni tishio kwa Kim Jong-Un

Gerald Robert

JF-Expert Member
Jan 2, 2013
337
219
MPANGO MPYA WA USALAMA WA MAREKANI NI TISHIO KWA KIM JONG-UN.

Katika siku ambayo baraza la usalama la Umoja wa mataifa linapiga kura kuidhinisha vikwazo vikali zaidi dhidi ya Korea kaskazini, kiongozi wa taifa hilo, Kim Jong-un, amesema taifa lake linawakilisha tishio kubwa la nyuklia kwa Marekani.

Katika hotuba iliyoripotiwa na shirika la utangazaji habari nchini (KCNA) Kim amesema kuendelezwa kwa haraka kwa mpango wa nchi yake wa nyuklia kunashinikiza ushawishi muhimu katika siasa za kimataifa.

Azimio la hivi karibuni la baraza hilo la usalama katika Umoja wa mataifa linalenga kupiga marufuku usafirishaji wa bidhaa zote za mafuta kwenda Pyongyang na kuitisha kurudishwa kwa raia wa Korea Kaskazini wanaofanya kazi katika nchi za nje katika muda wa mwaka.

Korea Kaskazini imetaja nakala za kiusalama za Marekani zinazosisitiza kuhusu utumizi wa mabavu dhidi ya Pyongnyang kuwa za kihalifu, vyombo vya habari vya taifa hilo zimesema.

Wizara ya maswala ya kigeni ilimlaumu rais wa Marekani Donald Trump kwa kutaka kukandamiza ulimwengu kupitia sera yake mpya ya usalama.

Siku ya Jumatatu rais Trump alisema kuwa Washington lazima ikabiliane na changamoto inayoletwa na mpango wa kutengeza silaha wa Pyongyang.

Msemaji wa wizara ya maswala ya kigeni nchini Korea Kaskazini amesema kuwa mpango mpya wa Marekani kuhusu usalama hauna lolote bali mpango wa kutaka kutumia nguvu kulingana na chombo cha habari cha kitaifa KCNA.

Ameilaumu Marekani kwa kutaka kujaribu kuvuruga taifa hilo na kugeuza rasi yote ya Korea kuwa eneo litakalotawaliwa na Marekani.

Siku ya Jumatatu rais Trump alielezea kuhusu mpango huo mpya akiikosoa Korea Kaskazini kwa kufanya majaribio ya silaha za kinyuklia licha ya shutuma kutoka Marekani na Umoja wa Mataifa.

Mwezi uliopita, rais wa Marekani pia aliliweka taifa la Korea Kaskazini miongoni mwa mataifa yanayofadhili ugaidi.
 
*Nilazima Amerika irejee nguvu yake ilokua nayo,, nilazima Amerika iweke Aman duniani kwakutumia "Nguvu"*.

Marais Wa Marekan wote wanakuaga waharibifu tu !!!.
 
Marekan ana mbwembwe sana hatukatai kuwa Kim atapigwa anachofanya Kim ni kudhibitisha mwanaume huwa hapigwi bali huwa anapigana kuna mataifa yamesubili tu Marekani ajichanganye kulianzisha sio. Zama za kuogopana hizi kilichobaki ni kuheshimiana
 
Li nchi kama Tanzania yani majungu2 hawana wanachowaza zaidi yamajungu bora2 niende hata north Korea nikaone uwezekano wa kupambana na trumpet
 
Hakuna nchi itakayokubali raia wake wafe kwa nyuklia kisaa upuuzi wa NK,si Russia wala China.
 
Li nchi kama Tanzania yani majungu2 hawana wanachowaza zaidi yamajungu bora2 niende hata north Korea nikaone uwezekano wa kupambana na trumpet
Nadhani wewe hujui kuwa sisi Tanzania tuna kikosi cha watu wasiojulikana. Kwa taarifa yako ni kuwa hiki kikosi cha wasiojulikana ni hatari zaidi kuliko hizo nyuklia za Kim coz zenyewe zinajulikana.
 
Nadhani wewe hujui kuwa sisi Tanzania tuna kikosi cha watu wasiojulikana. Kwa taarifa yako ni kuwa hiki kikosi cha wasiojulikana ni hatari zaidi kuliko hizo nyuklia za Kim coz zenyewe zinajulikana.
hakuna ki2 hapo wanajeshi wenyewe mpaka wapewe msaada na marekani sasa marekani imesema kwa yoyote anae mpinga juu ya Jerusalem hapati msaada ndio mtakapo kiona chamoto pumbavu jeshi la tz
 
wacha marekani waendelee kupanga mipango Kim yeye anaendelea kutest makombora yake.
 
Li nchi kama Tanzania yani majungu2 hawana wanachowaza zaidi yamajungu bora2 niende hata north Korea nikaone uwezekano wa kupambana na trumpet
samahani kunatenda huku yakupaka rangi achana na mitandao kuza kipajichako hicho maana umepatia kweli hizo herufi........
 
Back
Top Bottom