Twilumba
Platinum Member
- Dec 5, 2010
- 13,610
- 16,545
SOMA MPANGO HUU MCHAFU DHIDI YA WANAFUNZI WA VYUO VYA ELIMU YA JUU VYA DSM
Nitasema tu bila kuogopa chochote. Katika uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura unaoendelea sasa sidhani kama tume imeangalia suala hili kwa umakini.
Uchaguzi wa mwaka 2010 wanafunzi wengi walikosa haki yao ya msingi ya kupiga kura kutokana na muingiliano wa ratiba kati ya eneo la kujiandikisha, tarehe ya kupiga kura na ratiba ya vyuo. Nilidhani mwaka huu tume italiangalia hilo ila naona kuwa limepuuzwa.
Ikiwa imebaki siku moja kabla ya wakazi wa Dar Es Salaam kuanza kujiandikisha ukweli ni kwamba wanafunzi wengi wa vyuo vikuu vilivyopo jijini hapo watakosa haki hii kwani asilimia zaidi ya 90 ya vyuo hivyo vimefungwa wiki 2 zilizopita.
Zoezi la uandikishaji kwa jiji la DSM limekuwa likisogezwa sogezwa mbele bila sababu zozote za kimsingi, nadhani upo mpango maalum wa kuwakwamisha wanafunzi kupiga kura katika uchaguzi mkuu 2015 kwani wanafunzi hao kwasasa wameenda mikoani ambapo tayari zoezi hilo lilishafanyika.
Jiulize wanafunzi hao watajiandikisha wapi maana wameenda likizo mikoani kwao ambapo zoezi lilishafanyika na watakaporudi Dar Es Salaam watakuta zoezi pia limeshafanyika, watakuwa wageni wa nani?
Ombi langu kwa tume ya uandikishaji kuwa kama wanahitaji kila mtu apate haki hii ya msingi basi ni vizuri wakaliangalia hilo na uandikishwaji huo ukarudiwa tena katika vituo maalum hasa vyuoni mara baada ya vyuo kufungiliwa ili kila mtanzania apate haki yake.
Ahsante,
Michael Litanda,
Safari ya matumaini, Inaendelea.....