SERIKALI imeweka bayana mkakati mpya wa muda mfupi na mrefu utakaosaidia kupunguza msongamano wa magari katika Jiji la Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jana baada ya kumaliza kikao na viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Waziri Mkuu, Edward Lowassa, alisema barabara za Morogoro na Ali Hassan Mwinyi, zitagawanywa ili kupunguza msongamano nyakati za asubuhi na jioni.
Lowassa, alisema nyakati hizo magari katika Barabara ya Morogoro yatakayokuja mjini, yatatumia barabara tatu na moja itatumika kwa magari yanayotoka katikati ya mjini kwenda nje ya mji, na kuongeza kuwa utaratibu huo utafanyika pia kwenye Barabara ya Alli Hassan Mwinyi.
.....
Mpango wa njia tatu uliongeza ajali kwa waenda kwa miguu hasa wakti wa kuvuka barabara, ulianza bila elimu kwa waeanda kwa miguu, watu walivuka bila kuangalia kama kuna magari mengine
Mkuu tatizo hata hiyo OPRAS wanaoiratibu ambao ndio Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma ndio hawana habari kabisaaaaa!!! Sasa nani atamshika mwenzake uchawi?
Mwanakijiji; Huu mpango wa Lowassa wala haukufanikiwa ndio maaana wadau wakaupiga chini fasta sana ! Alitaka pia kuleta issue yake ya Mvua kutoka Thailanda inyeshe kwenye mabwawa ya yanayozalisha umeme lakini Wadau wakaona anawazingua tu ! Mwisho akamaliza na Dowans na jamaa zake wakina JK na Rostam wakamaliza game kabisaaa !
Sasa hivi ndio naskia huko Tanzania mnataka awe Rais sijui mnafikiria kwa kutumia " MASABURI " ???
kwa nilivyomuelewa mwanakijiji ameuliza mpango huu wa lowassa ulifanikiwa vipi?kwa kipindi kile jamani mpaka leo hii foleni zetu ni za kutupa. huo mfano umeigwa na nchi nyingine vile vile, algeria or somewhere. mi naona ulikuwa mpango mzuri ila mapolisi na watembea kwa miguu walikuwa hawaja elimishwa vizuri lakini ilipunguza sana foleni, na iliwafanya police wafanye kazi ya kuongoza magari sana sio kama sasa ivi.
nadhani walitoa iyo plan kama emergency kupunguza foleni kwasababu bado hatuna uwezo wa kurekebisha barabara zetu zote kwa mpigo. kuna nchi zingine wanapunguza foleni kwa kuruhusu aina ya namba flani za magari kutembea kwa siku flani au wanakataza magari makubwa kuingia mijini au kama wenzetu wa uingereza kuna hadi congestion charges kuingia mjini.
mimi nadhani the idea was good, we ddnt take time to implement it, kwa kweli ilitupunguzia foleni na mda wa kukaa bar sana tukawa tunawahi kwa wife. lowassa is a visionary bana, huwezi ku compare na uncle wako huyo sasa ivi..
prove me wrong mwanakijiji