Mpango Huu wa Lowassa ulifanikiwa vipi?

Mpango Huu wa Lowassa ulifanikiwa vipi?

SERIKALI imeweka bayana mkakati mpya wa muda mfupi na mrefu utakaosaidia kupunguza msongamano wa magari katika Jiji la Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jana baada ya kumaliza kikao na viongozi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Waziri Mkuu, Edward Lowassa, alisema barabara za Morogoro na Ali Hassan Mwinyi, zitagawanywa ili kupunguza msongamano nyakati za asubuhi na jioni.

Lowassa, alisema nyakati hizo magari katika Barabara ya Morogoro yatakayokuja mjini, yatatumia barabara tatu na moja itatumika kwa magari yanayotoka katikati ya mjini kwenda nje ya mji, na kuongeza kuwa utaratibu huo utafanyika pia kwenye Barabara ya Alli Hassan Mwinyi.

.....

Serikali ilikurupuka kutekeleza mpango huu....
Tatizo la kwanza kabisa ni makutano ya barabara zetu....ndipo inafuatia na barabara zenyewe.....na ilishindikana kutumia njia tatu kwenye makutano.

La msingi, wakati wenzetu Kenya wanamalizia 'fly overs' zao jijini Nairobi, sisi bado tunapiga porojo za alinacha..
 
Namkumbuka kamanda SACP Kombe alivyohangaika na mpango huu bila mafanikio. Watu wakagongwa sana tu. Makutano ya barabara yakaleta kero nyingine. Askari wakahitajika wengi sana. Madereva wetu wengi hawakuuelewa kabisa. Ukafa wenyewe.
 
hapa inaonyesha kuwa viongozi wetu wanaongea sana utekelezaji ni 0..sasa badala ya kuleta plan za long time wao wanafikiria shortcut tu
 
Mwanakijiji; Huu mpango wa Lowassa wala haukufanikiwa ndio maaana wadau wakaupiga chini fasta sana ! Alitaka pia kuleta issue yake ya Mvua kutoka Thailanda inyeshe kwenye mabwawa ya yanayozalisha umeme lakini Wadau wakaona anawazingua tu ! Mwisho akamaliza na Dowans na jamaa zake wakina JK na Rostam wakamaliza game kabisaaa !
Sasa hivi ndio naskia huko Tanzania mnataka awe Rais sijui mnafikiria kwa kutumia " MASABURI " ???
 
Hivi tatizo la watanganyika ni lipi hasa?! Uzi huu umewekwa hapa saa nne, hutegemei kuwa watu wana pombe vichwani mwao wala uchovu wa kazi! Lakini majibu yanayotoka ni mazingaombwe tupu... Sijui ni uvivu, ulevi, uwezo mdogo wa kusoma na kuelewa, kutokuelewa kiswahili, laana kwenye vichwa vya watu au nini?! Ikiwa miaka mitano iliyopita serikali ilikuwa tayari kutoa 10bn, World Bank ilikuwa INA-fadhili mradi huo... mikakati mbalimbali ikawekwa... hadi leo hakuna kinachoonekana, bado hamuoni mantiki ya uzi huu?!
 
kwa nilivyomuelewa mwanakijiji ameuliza mpango huu wa lowassa ulifanikiwa vipi?kwa kipindi kile jamani mpaka leo hii foleni zetu ni za kutupa. huo mfano umeigwa na nchi nyingine vile vile, algeria or somewhere. mi naona ulikuwa mpango mzuri ila mapolisi na watembea kwa miguu walikuwa hawaja elimishwa vizuri lakini ilipunguza sana foleni, na iliwafanya police wafanye kazi ya kuongoza magari sana sio kama sasa ivi.

nadhani walitoa iyo plan kama emergency kupunguza foleni kwasababu bado hatuna uwezo wa kurekebisha barabara zetu zote kwa mpigo. kuna nchi zingine wanapunguza foleni kwa kuruhusu aina ya namba flani za magari kutembea kwa siku flani au wanakataza magari makubwa kuingia mijini au kama wenzetu wa uingereza kuna hadi congestion charges kuingia mjini.

mimi nadhani the idea was good, we ddnt take time to implement it, kwa kweli ilitupunguzia foleni na mda wa kukaa bar sana tukawa tunawahi kwa wife. lowassa is a visionary bana, huwezi ku compare na uncle wako huyo sasa ivi..

prove me wrong mwanakijiji
 
Mpango wa njia tatu uliongeza ajali kwa waenda kwa miguu hasa wakti wa kuvuka barabara, ulianza bila elimu kwa waeanda kwa miguu, watu walivuka bila kuangalia kama kuna magari mengine

Insurance companies walikataa kulipa magari yaliyopata ajali kwenye njia TATU.
 
Mkuu tatizo hata hiyo OPRAS wanaoiratibu ambao ndio Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma ndio hawana habari kabisaaaaa!!! Sasa nani atamshika mwenzake uchawi?

hebi nikumbushe hiyo ofisi/Wizara inaongozwa na nani vile?
No wonder haifanyi lolote.
 
pimeni uzito jamani, sio kuongea tu, iyo dowans iko wapi? mi nilikaa ikaniuma sana nikifikiri huyu kiongozi niliyokua nampenda kweli ameharibu. iyo dowans sasa ivi imewashwa vile vile, ikabadilishwa jina, na inazalisha umeme. kama kweli huyu mzee angekua kausika na dowans, na kwa jinsi walioko kwenye system wanavyomchukia, wangesha mlyumba huyu mzee.. lakini leo wako wapi.

juzi kama ulifuatilia kikao cha ccm, lowassa alisema yote juu ya dowans, na akamuuliza rais ni lipi ambalo halijui.

kama ni kuwa rais, mimi ningetaka hata leo awe rais
 
Mwanakijiji; Huu mpango wa Lowassa wala haukufanikiwa ndio maaana wadau wakaupiga chini fasta sana ! Alitaka pia kuleta issue yake ya Mvua kutoka Thailanda inyeshe kwenye mabwawa ya yanayozalisha umeme lakini Wadau wakaona anawazingua tu ! Mwisho akamaliza na Dowans na jamaa zake wakina JK na Rostam wakamaliza game kabisaaa !
Sasa hivi ndio naskia huko Tanzania mnataka awe Rais sijui mnafikiria kwa kutumia " MASABURI " ???

Uzuri wetu wataznania ni uwezo wetu wa kusahau haraka!
 
This was an excellent idea. But was implemented without any planning and the consequences was DISASTROUS! Madreva ndo walikuwa wanaamua muda gani watumie njia ya tatu hata askari hawakuwa na clue nini kifanyike. Matokeo yake watu wengi sana waligongwa na folleni zikazidi. Ajali zilizotokea njia ya tatu zikakutana na resistance ya insurance companies na pole pole mpango ukafa.

Kuutekeleza mpango ule ilitakiwa planning ya hali ya juu. Ilitakiwa zifanyike simulations za computer models kujua askari wakae wapi na muda gani, wayaelekeze wapi magari. Kila junction ilitakiwa iwe na askari, na askari wale ilitakiwa wawe wanawasiliana kwa karibu sana. Ilitakiwa kuwe na CCTV za ku-monitor bara bara zilizokuwa katika mpango na kuwe na central control ya kuamua ni muda gani njia ya tatu itumike na itumikeje.

Planning ya namna hii ingeweza kufanyika katika kipindi cha miezi mitatu kabla ya implementation. Implementation ilitakiwa ianzae na bara bara moja moja; halafu uzoefu uwe transfered kwenye bara bara zingine. Yote haya hayakufanyika. Mtu alikaa ofisini akaamua tu na VURUGU NDO ZILIFUATA.

It was completely cheotic and the system died a natural death without any official announcement. Hatuwezi kuendesha nchi kienyeji hivyo! Inatakiwa watu wajipange, na wenye utaalam katika traffic control and management ilitakiwa waumize vichwa kabla ya kukurupuka.

Wazo lilikuwa zuri. Mawazo mazuri ni mengi tu. Inatakiwa planning na implementation. Hapa ndo penye siri kuuu. Hiki ndo kinachotofautisha nchi na nchi. Mawazo tu, vichwa havitofautiani sana katika ku-generate mawazo mazuri. Kupanga na kuyaweka mawazo kwenye uhalisia (Reality) ndo siri kubwa inayomtofautisha mtu mmoja na mwengine.
 
kwa nilivyomuelewa mwanakijiji ameuliza mpango huu wa lowassa ulifanikiwa vipi?kwa kipindi kile jamani mpaka leo hii foleni zetu ni za kutupa. huo mfano umeigwa na nchi nyingine vile vile, algeria or somewhere. mi naona ulikuwa mpango mzuri ila mapolisi na watembea kwa miguu walikuwa hawaja elimishwa vizuri lakini ilipunguza sana foleni, na iliwafanya police wafanye kazi ya kuongoza magari sana sio kama sasa ivi.

nadhani walitoa iyo plan kama emergency kupunguza foleni kwasababu bado hatuna uwezo wa kurekebisha barabara zetu zote kwa mpigo. kuna nchi zingine wanapunguza foleni kwa kuruhusu aina ya namba flani za magari kutembea kwa siku flani au wanakataza magari makubwa kuingia mijini au kama wenzetu wa uingereza kuna hadi congestion charges kuingia mjini.

mimi nadhani the idea was good, we ddnt take time to implement it, kwa kweli ilitupunguzia foleni na mda wa kukaa bar sana tukawa tunawahi kwa wife. lowassa is a visionary bana, huwezi ku compare na uncle wako huyo sasa ivi..

prove me wrong mwanakijiji

Mkuu tuko pamoja hapa. Mpango ulikuwa mzuri lakini utekelezaji na usimamizi ulikuwa mbaya. Umezungumzia Algeria, lakini pia pale Khartoum, Sudan mpango huu unatumika na unasaidia sana kupunguza traffic jam wakati wa peak hours.

Tiba
 
Mpango hauwezi kuwa ulikuwa mzuri kama haukupangwa vizuri! Ili uweze kupanga vizuri unatakiwa ufikiri kwa usahihi, upime uwezekano wa mambo mbalimbali kutokea (planning for contingencies) n.k Kwa ufupi Lowassa ambaye tunasukumiziwa kuwa alikuwa anafanya maamuzi magumu alijionesha kuwa alifanya maamuzi ya kihisia siyo ya kufikiria kwa kina. Hili linajirudia alipoamua kuunda ile timu ya GNT kwenye Richmond hakuwa na nguvu ya kufanya vile na matokeo yake ni Richmond.
 
mmj rudi bongo utusaidie jamani. nimecheka sana hii topic yako umeturudisha nyuma ambako watanzania wengi walishasahau lol tanzania yangu viongozi wanashindwa kufikiri na kufanya research kabla hawajafanya maamuzi wanayoyaita magumu?
 
Dah, Manakijiji na wewe bana. Hivi ulitegemea kweli serikali ya kibabaishaji kama hii ifanikishe mpango wowote? Btw, serikali yetu imefanikiwa sana kwenye mpango wa kuiba kura kwa kushirikiana na ccm.
 
Back
Top Bottom