Kila nyumba inastahili kuwa na sehemu maalum ya kulia chakula— haijalishi ukubwa wa nyumba yako!
Watanzania wengi tunaamini ili uwe na sehemu ya kulia, lazima uwe na nyumba kubwa yenye chumba maalum na meza ya viti 6 au 8. Matokeo yake? Tunajikuta tunakula kwenye makochi, kwenye coffee table tukiwa tumeinama, au chumbani kitandani!
Ukweli ni kwamba, dining haipimwi kwa ukubwa, inapimwa kwa mpangilio.
Kama unavyoona kwenye picha hii, hata kona ndogo ya sebule yako inaweza kubadilika kabisa ukiweka:
✅ Kameza kadogo (Round au Square) – Meza ya duara kama hii haichukui nafasi kubwa na haina kona kali za kukukwaza unapopita.
✅ Viti vichache kulingana na familia yako – Kama mpo wawili au watatu, viti 2 hadi 3 vinatosha kabisa. Sio lazima ununue seti kubwa inayojaza chumba.
✅ Kioo ukutani (Sio lazima)– Kuweka kioo juu ya meza ya dining kunafanya kona hiyo ionekane kubwa, yenye mwanga, na ya kisasa zaidi.
Kwa nini ni muhimu kuwa na sehemu hii?
1️⃣ Unakaa vizuri, mgongo ukiwa umenyooka badala ya kuinamia meza fupi ya sebuleni.
2️⃣ Ni sehemu nzuri ya kukaa pamoja, kupiga stori za siku, au hata sehemu ya mtoto mdogo kufanyia home work zake.
3️⃣ Inapendezesha nyumba: Inatenganisha eneo la kupumzika (makochi) na eneo la kula, na kuipa sebule yako muonekano wa smart na uliopangiliwa.
Hata fundi wako wa mtaani anaweza kukutengenezea meza ndogo kama hii kwa bajeti rafiki kabisa!
Wewe nyumbani kwako unalia chakula wapi mara nyingi kwenye dining, kwenye makochi, au mkeka?