Mpangaji Mmbea...!

rikiboy

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2017
Posts
22,163
Reaction score
43,988
Aisee kuishi na watu kazi sana.. Kuna mpangaji mwenzangu ni mdada lakini ni mmbea balaaa yani linasema mambo ya Kijinga sana kwa mama mwenye nyumba afu ubaya mama mwenye Nyumba ananiambia mpaka nashangaa.. Vipi ushawahi ishi na mpangaji mmbea?? Nifanyaje kuhusu hili lidada...??
 
Zaba makofiii
 
Muhim kutafuta njia ya kutokuwa na mazoea naye hasa huyo mmbea...wengine ukiwa na mgeni ndan ndo wanagonga mlango utasikia anaomba kitu from nowhere
Now simpi hata salam paka pori huyu... Kwanza anagombana na kila mtu ma mwenye nyumba soon anataka kumpa notice
 
mkuu naomba nieleweshe kwanza umbea wake ukoje maana kuna mmbea anayosema yaliyo ya kweli na mmbea anayosema si ya kweli

ila kama anasema yaliyo ya kweli na ni mabaya kwa upande wako uyafanyayo basi jirekebishe

ila kama anasema yaliyo si ya kweli basi muonye na kisha umpotezee tu kwa maana neno likisha semwa ni ngumu kulibadili kwenye akili ya mtu kwa hiyo utakuta tu unaumiza kichwa bure
 
Wewe nae utakuwa mmbea sasa hata kama ni ya kweli mambo ya mwingine yanakuhusu nini?
 
naomba maana ya neno mmbea.....tuanze kwanza hapo maana unaweza andika usichokijua na kukielewa
Mchongezi, mtu mwenye kusemea mambo ya uwongo kuelekea wengine.


But hata kama ni ya ukweli wewe unaenda kuyasemea kwa mwingine yanakuhusu nini?
 
Jaman issue ya umbea ni kutoa tarifa ya Mtu au watu bila kuambiwa ufanye hivyo


Sasa itakuwaje kama Mtu huy anatoa tarifa bila kutumwa but Zina mashiko kwa namna moja au nyingine?

Mfano wewe ume toka Kuna Mtu kaja kufanya jambo sio LA kiungwana kwako na Jamaa kaona ila jambo Hilo halimuhusu je akipiga kimya ni sahihi mana akisema tuu Tayar anakuwa mbea
 
Mchongezi, mtu mwenye kusemea mambo ya uwongo kuelekea wengine.


But hata kama ni ya ukweli wewe unaenda kuyasemea kwa mwingine yanakuhusu nini?
we jamaa tafuta kamusi ya kiswahili itakusaidia kuwa mchongezi hujui ni nani wala mmbea ni nani na je nikikuuliza msengenyaji ni nani utaweza niambia kweli?
hivi hata nikazungumza jambo zuri na lenye kukusifia kwa mtu ambalo halinuhusu je na mimi nitakuwa nani mmbea au?
 
Acha ukuda mkuu
 
mkuu ahsante kwa kusaidia watu maana ya neno mmbea yani akili ya wengi ukitamka tu mmbea basi wanafikiri ni mtu mbaya kumbe si kweli mmbea anaweza kuwa mwema
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…