Mpangaji atupiwa Vitu Vyake Nje | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mpangaji atupiwa Vitu Vyake Nje

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mnhenwa Ndege, Jul 16, 2009.

 1. Mnhenwa Ndege

  Mnhenwa Ndege JF-Expert Member

  #1
  Jul 16, 2009
  Joined: Dec 5, 2007
  Messages: 243
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
  Rose akikagua vyitu vyake vilivyotupwa nje na mwenye nyumba wake
  [​IMG]
  Kijana huyu anakagua kama CD zote vipo. Sipati picha kama ingekuwa Kinondoni ingekuwaje, hata sisi tusingeweza kupiga picha maana pasinge kuwa na vitu
  [​IMG]
  Hili ndilo Kanisa lililo pangishwa, wenyewe wanajiita the Mega Church.

  Mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Rose ambaye alikuwa amepanga katika nyumba namba 104 iliyoko katika mtaa wa Nyuma Mikocheni B, amejikuta katika wakati mgumu baada ya mwenye nyumba wake kumtolea vitu vyake vya thamani nje bila ya taarifa wala ridhaa yake.

  Rose alimuaga mama mwenye nyumba wake (Joyce Mbuga) kuwa anaenda Mbeya kumuangalia mwanawe aitwaye Jennifer (14) mwanafunzi wa kidato cha tatu katika shule ya secondary ya Elimuladi ambaye alikuwa amevunjika mguu na alihitajika ahamishwe kutoka hospitali ya Wemba Mission kuja Muhumbili kwa matibabu zaidi. Wakati akiwa Mbeya mama mwenye nyumba alikuwa akimpigia simu Rose aje atoe vitu vyake katika chumba chake.

  Rose akiongea na mwandishi wa habari hizi alisema tayari walikuwa na makubaliano ya kupanga katika nyumba hiyo ambapo kwa muda wa miezi minne tayari alikuwa amesha mlipa mama mwenye nyumba hiyo kiasi cha Tsh. 400,000. jambao ambalo walikuwa wamekubaliana awali lakini mama mwenye nyumba huyo alipata wateja wengine waliopenda kupanga katika eneo hilo kwa nia ya kufanya kanisa. Mpaka sasa chumba hicho tayari kimepangishwa watu ambao sio raia wa Tanzania na wameanzisha kanisa linalojulikana kwa jina la Kanisa la Kimataifa la Light House Chapel likiwa na ujumbe usema The Mega Church (Kanisa Kubwa). Baada ya mama huyo kupangisha nyumba hiyo kwa watu wa kanisa, alimtolea mpangaji wake Rose vitu vyake vyote nje na kufanya viibiwe pasipo yeye kujua wakati akiwa hospitalini Muhimbili.

  Kutokana na tatizo hilo mjumbe wa nyumba kumi katika eneo hilo alipata taarifa na kusema kuwa kitendo alichofanya mama Joyce si chakiungwana. Hadi sasa dada Joyce ameswekwa ndani katika kituo cha polisi Oyster Bay jijinii.

  Source: Pwani Raha
   
 2. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #2
  Jul 16, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Hizi picha zina ruhusa ya wenyewe au wamepigwa kiwizi tu? Watu wengine hawapendi kupigwa picha katika hali isiyo dignity kama hii, hii eviction ilikuwa dehumanizing vya kutosha, je hizi picha zina ruhusa?
   
 3. Mnhenwa Ndege

  Mnhenwa Ndege JF-Expert Member

  #3
  Jul 17, 2009
  Joined: Dec 5, 2007
  Messages: 243
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Mwenye hizi picha ndio alimwita cameraman ili stori ifike kwa jamii, Ukiangalia tu hapo kwenye picha unadhani hawa watu hawamuoni mwenye kamera. It does not need a rocket scientist to figure that out. Siku nyengine ukitaka kuuliza maswali mwanzo jiulize wewe mwenyewe hayo maswali. Wewe unadhani hii stori yote ya kuwa mpangaji alienda Mbeya akarudi, mwanawe alivunjika mguu and so on mwandishi aliipata wapi kama sio kwa huyu mama.
   
 4. Mwenda_Pole

  Mwenda_Pole JF-Expert Member

  #4
  Jul 17, 2009
  Joined: Jul 5, 2008
  Messages: 260
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Ndio maana najibana nijenge nyumba yangu.... ushenzi kama huu sikubaliani nao hata kidogo... kama ningekuwa mimi nafikiri ni mimi ndio ningekuwa ndani huko kituoni kwa kuvuruga kabisa sura ya huyo mama mwenye nyumba, ila dah.. bei za viwanja nazo zipo juu...!!!!!!
   
 5. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #5
  Jul 17, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Kwanza "mwenye picha" ni nani? au unakusudia huyu mpangaji aliyepigwa picha? Kama unakusudia huyu mpangaji sema hivyo, kuwa coherent kwanza, uweze kuwasiliana.

  Pili hii habari ya huyu mpangaji kumuita cameraman umeipata wapi? Ni fact au ni speculation tu? What does a rocket scientist have to do with this? Mambo mengine unayoweza kufikiri unayajua kwa kusema "it does not take a rocket scientist" yanaweza kukuingiza mkenge.Kwa kuangalia picha hizi na kusoma story hii mtu yeyote rational hawezi kujua kwamba hizi picha zilipigwa kwa ridhaa ama la, hata point yako ya "hawamuoni mwenye kamera" iko moot, kwani hakuna picha inayomuonyesha mtu akiiangalia camera directly, which could mean the pictures may have been taken in stealth.Na hata kama wangekuwa wanaangalia kamera hujui makubaliano yalikuwa vipi, pengine walikubali picha zichukuliwe kama ushahidi katika kesi lakini zisitolewe mitandaoni.

  Kwa hiyo mpaka sasa hujaweza kuonyesha kwamba huyu mpangaji alitoa ridhaa picha hizi zitolewe humu, kitu ambacho kilikuwa msingi wa swali langu.

  Hiyo story ilijitosheleza,hizo picha zinaondoa dignity na kupalilia sadists' schadenfreude. wanakuwa kama vituko vya kikatuni fulani hivi in the midst of their misfortune, for all the world to see.

  Lakini I also wouldn't be surprised kama wabongo hawajali personal privacy na dignity na wanafikiri kutoa mipicha ya eviction for the word to see kutaleta sympathy zaidi kwao na ku build up their case, the sacrifice of privacy was totally unnecessary.But different folks have different life experiences and different levels of sense of privacy.

  Lakini swali langu kama privacy advocate halijajibiwa.
   
Loading...