Mpanga ubaya mwisho humuumbua Polisi wa Zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mpanga ubaya mwisho humuumbua Polisi wa Zanzibar

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by abdul 28, Jun 6, 2012.

 1. a

  abdul 28 JF-Expert Member

  #1
  Jun 6, 2012
  Joined: May 29, 2012
  Messages: 325
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  [​IMG]Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohammed Aboud Mohammed akizungumza na waandishi wa habari huko kituo cha televisheni cha serikali (ZBC) Zanzibar

  Jabir Idrissa
  KUNA uhalifu umefanywa Zanzibar. Ni katika matukio mabaya yaliyoanza usiku wa tarehe 26 Mei 2012. Watu wamechochewa kupambana na dola. Hili halijaelezwa na serikali. Polisi wamevamia nyumba za viongozi wa Uamsho na kuvunja milango huku wakiwatukana matusi ya nguoni viongozi na familia zao sambamba na kuwatishia maisha. Polisi hawajalieleza hili. Amir (kiongozi) wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu (JUMIKI), Sheikh Farid Ahmed Hadi anasema usiku wa Jumamosi hiyo, akiwa kwake, alipata taarifa anafuatwa na polisi wa kuzuia fujo (FFU).[​IMG][​IMG]
  Akajiandaa. Mnamo saa 7.30 kweli wakafika. Wakataka mlango ufunguliwe. Hakuna aliyewatii. Wakarusha risasi hewani. Hakuna aliyetoka. Hakuna aliyepiga kelele kutokea ndani. Lakini, baada ya kuona vishindo vimezidi, Sheikh Farid akasema kwa sauti, “Nipo ndani na familia yangu tumepumzika. Kama mpo tayari, fanyeni chochote nje ila, ninaapa kwa jina la Allah, anayekuja ndani, tutakabiliana mimi sina bunduki.”
  Polisi hawakujali. Wakafyatua mabomu. Wakavunja mlango na kuvuruga walivyovikuta nje. Wakataka kuingia ndani. Wakakatazana, “hapana. Mnajua nani wamo ndani? Tuondokeni.” Wakaondoka, anasimulia Sheikh Farid. Amepata simulizi kama hizo kwa viongozi wenzake wa Uamsho. Lakini sokomoko kama lililomkuta, lilitokea nyumbani kwa naibu wake, Sheikh Azzan Khalid Hamdan, wakati mwenyewe akiwa nje ya nchi kwa matibabu.
  Sheikh Azzan aliporudi Ijumaa, akapewa taarifa na familia yake kuwa walifika polisi wa FFU na kufanya fujo. Walifyatua risasi nje, wakavunja mlango. Wakapiga mayowe ya kumtukana matusi yeye na familia. Wakaondoka. Hakutulia. Alikwenda kupiga ripoti kituo cha polisi Mfenesini, karibu na anapoishi. Wakuu wakakana kufika kwake. Wakasema askari waliomfuata walitoka Mwembemadema.
  Mwembemadema ni makao makuu ya polisi mkoa wa Mjini Magharibi.

  Hawa ndio waliotuma makachero Jumamosi ile wakamshike Ustadhi Mussa Juma Issa, mmoja wa wahadhir wakuu wa Uamsho, kipenzi cha wahudhuriaji wa mihadhara ya jumuiya hii inayohamasisha Wazanzibari kuukataa muungano.
  Wapo watu wamejitokeza kutoa ushahidi wa walivyoona polisi wanalipua nyumba na mali za vitegauchumi za raia wema, zikiwemo gari zilizoegeshwa Kisiwandui na Michenzani. Mwanamke anayefanya kazi shirika la ndege la Kenya Airways, gari yake iliteketezwa kwa bomu lililorushwa na polisi. Matukio yote hayo katika siku mbili – Jumamosi na Jumapili.
  Leo, taarifa zimepatikana za uhalifu wa Polisi uliofanywa Jumatatu, 28 Mei, muda mfupi baada ya watuhumiwa 30 wa fujo, walipoachiwa kwa dhamana na Mahakama ya Mwanakwerekwe, mjini Zanzibar. Kati yao wapo viongozi wawili, akiwemo Ustadhi Mussa, wa Uamsho.
  Wakati wakili wao, Abdalla Juma akiwa Mahakama ya Ardhi, Vuga, vijana wa FFU walivamia ofisi zake Amani, yapata kilomita tano kutoka Vuga. Wakapitisha mitutu ya bunduki madirishani na kufyatua risasi na mabomu ya machozi.
  Hawakujali wafanyakazi waliokuwa ndani. Ni mchana kweupe. Hapana, ni mchana wa mola muumba mbingu na ardhi siku ya kazi, Jumatatu. Ipo taarifa ya Chama cha Wanasheria wa Zanzibar (ZLS) kulalamikia kitendo hicho. Wamemtumia barua Kamishna wa Polisi wa Zanzibar, Mussa Ali Mussa, na kumtaka asake wahusika na kuwashitaki.
  ZLS wamekiita kitendo hicho cha makusudi kilicholenga kutisha mawakili wasiwe imara katika kazi yao ya kutetea wananchi wanaposhitakiwa. Polisi wanatuhumiwa sasa kushiriki vitendo vya uhalifu katika kipindi kilekile ambacho wao wanatuhumu Uamsho kuzusha ghasia mjini Zanzibar.
  Ninayaeleza haya ili kukumbusha historia ya kisiasa Zanzibar inayochefua. Siasa za maridhiano zilizoanza kustawi tangu 2010 mwishoni, zinachafuliwa kwa nguvu. Ni kama zilivyokuwa zikipandikizwa na kustawishwa siku zile za giza, mara tu mfumo wa siasa za vyama vingi, siasa za ushindani, uliporudishwa chini ya sheria ya Tanzania.
  Sasa wapo wasiotaka amani Zanzibar idumu. Wapo. Pengine wanampenda Amani Abeid Karume, kiongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), Maalim Seif Shariff Hamad, ambao walizijenga, bali wanachukia matunda ya maridhiano.
  Polisi. Polisi. Polisi. Polisi. Polisi. Polisi. Polisi. Polisi. Polisi. Hapana; si peke yao. Kwa jumla, vyombo vya dola, vya dola, vya dola. Dola, dola, dola, dola, dola, dola, dola, dola, dola. Vyote vilitajwa kupandikiza chuki kwa wananchi, mgongo ukiwa vyama vingi na uimara wa CUF. Visima vikapakwa kinyesi, ofisi za umma zikawashwa kwa viberiti na makanisa yakachomwa kiajizi. Kanisa linawashwa, dakika mbili tu hao walinzi wamefika.
  Ushetani ule ukakoma pale wananchi wa Shengejuu, kaskazini Pemba, walipovizia usiku kutafuta nani hasa wakihusika na vitendo vile vya kiharamia. Waliokutwa mpaka leo Polisi hawajawataja.
  Ni askari polisi na mashushushu ndani ya Landrover iliyosheheni madumu ya petroli, mapipa ya kinyesi na viberiti vya kuwashia mabomu ya chupa.

  Kutaka kuzubaisha umma wa Watanzania na ulimwengu, IGP Omari Mahita akaunda kikosi kuchunguza. Akamteua Robert Manumba, kachero aliyekuwa msaidizi mkuu wa DCI Adadi Rajabu, kukiongoza.
  Alitaka wachunguze chimbuko, sababu na wahusika wa milipuko ile ya kishetani pamoja na vitendo haramu vya kupaka kinyesi madarasa na kukimwaga kwenye visima vya maji wanayotumia wananchi.
  Tangu wakati ule, karibu miaka kumi sasa, si DCI Manumba ambaye sasa ndiye DCI, si IGP Mahita wala serikali iliyotoa ripoti ya uchunguzi huo. Wananchi waseme nini hapo? Lakini kwa sababu wahusika walijulikana na kufikia kukamatwa Shengejuu, zile fitna kuwa CUF walikuwa wahusika, zilifutika.

  Tungalinao wakorofi wasiopenda maridhiano. Wahafidhina ndani ya CCM wameibuka upya wakitaka kuharibu amani na utulivu. Hawawezi kuitaja CUF moja kwa moja maana wanashirikiana nacho kuendesha serikali.
  Wametafuta pa kuingilia – Uamsho. Kwa kuwa taasisi hii imechukua jukumu la kupigania haki za wananchi wasioridhishwa na mwenendo wa muungano, wanawapakazia kuwa wanavunja amani.
  Kumbe bado kuujadili Muungano wa Tanzania ni uhaini. Pamoja na serikali kuruhusu Watanzania watoe maoni yatakayotumika kuandika katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, watawala hawapendi watu wafikiri tofauti na wao.

  Tunaona kila viongozi wa polisi wanavyojitahidi kupotosha ukweli wa kilichotendeka mjini Zanzibar, ile dhamira yao ya kupotosha inawarudia. Wanatajwa baada ya kuonekana wazi wakivamia na kuharibu mali ikiwemo ofisi za wanasheria.
  Mpanga ubaya mwisho humrudia. Hawajajisafisha, wamejiumbua. Na ndiyo matokeo ya polisi nchini kushabikia siasa. Wanasubiriwa watamshika nani mchoma makanisa. Bado watafute ushahidi kuthibitisha kesi ya watu 30, pamoja na wafadhili wa Uamsho.


   
 2. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #2
  Jun 6, 2012
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Very good boy. Sema kweli japo kuwa inauma.
   
 3. promiseme

  promiseme JF-Expert Member

  #3
  Jun 7, 2012
  Joined: Mar 15, 2010
  Messages: 2,715
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 135
  Mwenyezi Mungu hamfichi dhalim..
   
 4. l

  lost account Member

  #4
  Jun 7, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mambo yale yale ya Mungiki!
   
 5. Officer2009

  Officer2009 JF-Expert Member

  #5
  Jun 7, 2012
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 563
  Likes Received: 63
  Trophy Points: 45
  Hawa uamsho kwa nini wasipigwe bakora hadharani? Ikibidi wawekwe detention without trial kwa miaka minne, ndo watashika adabu.
   
 6. R

  Rebel volcano JF-Expert Member

  #6
  Jun 7, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 404
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  nimeelewa kinachoendelea.
   
 7. kwamwewe

  kwamwewe JF-Expert Member

  #7
  Jun 8, 2012
  Joined: Jul 15, 2010
  Messages: 1,313
  Likes Received: 118
  Trophy Points: 160
  amri kama hizo ndizo wanazitoa maaskofu na kuitishia serikali kuwa ikiwa hawakuzuia mihadhara wataifanya wao hiyo kazi kama vile wao ndio serikali kweli tutafika
   
 8. E

  Etairo JF-Expert Member

  #8
  Jun 8, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 244
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Huu ndo uandishi wa habari bwana, hakuna kuogopa madhara, tetea jamii, elemisha jamii na furahisha na kusoa jamii pale inapobidi hata kama ni kugharimu maisha. Jeshi na polisi na usalama wa taifa -hawafanyi kazi isipokuwa kwa maslahi yao, acheni hizo, fanyeni kazi kwa maslahi ya umma. hamjui, leo ni ccm kesho ni nani basi? msjie kugeuka na kuanza kukimbia vivuli vyenu wenyewe.

  NASEMA TENA TENDENI HAKI, ACHENI UPUUZI
   
 9. E

  Etairo JF-Expert Member

  #9
  Jun 8, 2012
  Joined: Jan 17, 2012
  Messages: 244
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ndo mfumo wenyewe huo-kanisa kutawala kupitia mlango wa nyuma-maamuzi yote yao, wanafanya kimya, hatimaye wanafanya wazi. Mwisho wake untafika tu kwani HAKUNA DHULUMA ISIYO NA MWISHO-ubainifu umeanza na NECTA
   
 10. S

  Saracen Senior Member

  #10
  Jan 12, 2018 at 2:16 PM
  Joined: Apr 14, 2011
  Messages: 147
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  TULIKOTOKA

  WAKAJA JUUU

  WAKO WAPI?
   
Loading...