Mpambe mpya wa rais

SAIZI YANGU

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2013
Posts
381
Reaction score
83
Wana JF hivi kuna mtu ana CV ya mpambe mpya wa rais? Kama ipo tuwekeeni hewani kuanzia jina na sifa nyingine maana hapa mtaani wanadai jamaa ni Komando.
 
Wana JF hivi kuna mtu ana CV ya mpambe mpya wa rais? Kama ipo tuwekeeni hewani kuanzia jina na sifa nyingine maana hapa mtaani wanadai jamaa ni Komando.

Hakuna haja ya CV yake kwani Mpambe wa Rais yeye si Mlinzi wa moja kwa moja , wapo walinzi wengine wa TISS ambao wana Mafunzo maalum yakiwemo ya Ukomandoo na hao ndio hubeba siraha ndani ya Suti ,tambua walinzi wa Rais ni kikosi maalum ambacho kimeandaliwa kiulinzi haswaa . Kazi ya Mpambe wa Rais ni usaidizi wa kikakamavu Pia ikumbukwe Rais ni Amiri Jeshi Mkuu hivyo lazima awe na mpambe mwanajeshi kwa ajili ya kumsaidia .
 
Yule unaemuona nyuma ya mhe. rais ni ADC yaani aide de camp. walinzi wenyewe utawaona wamesimama kihasara hasara na miwani za jua na kaunda suti au suti. Ila ukitaka kuwajua vizuri na utendaji wao. hebu jifanye unamsogelea rais au ingilia msafara wake. hapo utawaona first hand
 
Wana JF hivi kuna mtu ana CV ya mpambe mpya wa rais? Kama ipo tuwekeeni hewani kuanzia jina na sifa nyingine maana hapa mtaani wanadai jamaa ni Komando.

Mkuu, naomba CV ya yule mpambe kabla ya huyo.
 
Sijui kama ni siasa au uhuru wa vyombo vya habari ila ninachokiona siku hizi ni kama vile raia wanakosa imani au wanachukulia poa sana masuala ya usalama haswa wa viongozi!!!!!

Yaani PSU inachukuliwa kiwepesi sana ndio maana unaona watu wanadhani Rais akiwa na ADC ambaye ni Commando basi ndio inakuwa kila kitu ingawa ni kweli pia akiwa hivyo pale mziki unakuwa kamili sana!!!!

Labda inahitajika some tips kwa watu kujua kuwa Rais analindwa kwa maana ya kulindwa achilia mbali suala la kiuchumi na teknolojia pamoja na umuhimu wake !!!
 

Nimeipenda Hii Mkuu. Tunahitaji Vichwa Kama Hivi Humu JF!!! Mkuu Nimekukubali na Umemaliza Kila Kitu, Akhsante.
 
Rekebisha lugha yako:
siraha =silaha
SHIEKA, kny #TeamRekebishaLugha
cc charminglady, Kibo10 nevergiveup.
 
Last edited by a moderator:
tpatie picha mi cjawahi ona mpambe naonaga tu yule mlinzi ama ndo huyo?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…