Umetokea ubishani mkali leo kati ya Katibu Mkuu wa UN, Ban Ki-moon, na Waziri wa mambo ya Nje wa Syria Bw. Waled Moalem katika mkutano unaojadili Amani ya Syria nchini Uswisi ambapo Bw. Ki-moon alijaribu kukatisha hotuba ya Moalem kwa madai ya kutumia muda mrefu, lakini Waziri huyo akagoma na kushinikiza kuwa ni lazima amalize hotuba yake! Lakini baada ya mabishano ya muda, hatimaye walikubaliana Waziri huyo amalizie hotuba yake!! Haikuonyesha 'picha' nzuri kwa kweli wakubwa kubishana dunia nzima ikiona "live"!!
NB: Hata hivyo, muda rasmi wa hotuba ulikuwa ni dakika 7 lakini Moalem alitumia muda mwingi zaidi ya dakika 20!
Source: Aljazeera International ("Live" punde tu):
NB: Hata hivyo, muda rasmi wa hotuba ulikuwa ni dakika 7 lakini Moalem alitumia muda mwingi zaidi ya dakika 20!
Source: Aljazeera International ("Live" punde tu):