Mpaka wa ukosoaji unaanzia na kuishia wapi?

kensh

JF-Expert Member
Jul 19, 2012
527
113
Ni ajabu sana katika nchi hii au kwangu mimi. Leo mtu akimkosoa Magufuli, anaonekana hafai na hapaswi kusikilizwa. Membe anashambuliwa sana badala ya kusikilizwa na kupingwa kwa hoja mbadala.

Nauliza, wapi mwanzao na mwisho wa ukosoaji?

Ninavyofahamu ni kwamba katika kukosoana ndipo hupatikana wazo bora zaidi la kufanyia kazi, lakini hapa Tz , kukosoa ni dhambi.
 
Kwa mfano ukimkosoa DC tu anatoa amri uswekwe ndani.Akikustahi anakufokea na wewe unaufyata yani huku vijijini ndo usiseme.
 
Ni ajabu sana katika nchi hii au kwangu mimi. Leo mtu akimkosoa Magufuli, anaonekana hafai na hapaswi kusikilizwa. Membe anashambuliwa sana badala ya kusikilizwa na kupingwa kwa hoja mbadala.

Nauliza, wapi mwanzao na mwisho wa ukosoaji?

Ninavyofahamu ni kwamba katika kukosoana ndipo hupatikana wazo bora zaidi la kufanyia kazi, lakini hapa Tz , kukosoa ni dhambi.
ebu jitie ufahamu kidogo. kinachogomba katika sakata la membe ni njia aliotumia kufikisha ujumbe kwa jpm ya media. wote ni wana ccm tena presidential materials, kwanini asingeenda kuonana nae?
katika familia yako ukipishana na kaka yako unaingia mitaani na kuanza kubwabwaja? utaonekana juha na kushambuliwa na wanafamilia. ndo yanayokuta membe.
 
membe as much namuona ni wale wale tu lakin at least alikua sahihi kukosoa kwan kupitia kukosoa ndio tunaenda mbele, sie wengine tutabaki upande wa kukosoa wanaotaka kusifia tu wakat tanzania ni ktk nchi maskini dunian waendelee tu kusifia
 
Huwezi kwenda kumsema mjomba wako dukani kwa mangi wakati mnaishi pamoja na unaweza mfikishia ujumbe moja kwa moja.
Zito alisemwa sana alivyokuwa PAC akakisema vibaya chama chake, Sita alikua kwenye mvutano na chama chake kwa mda mrefu kwasababu hizi hizi.
Kila mtu lazima atambue wajibu wake kwa nafasi aliyonayo, ukiona ulipo sipo basi toka uende penye nafasi
 
Kosoa vitu vipasavyo kukosolewa hakuna shida... si kukosoa mpaka kisichopaswa kukosolewa.

MFANO:

1. Safari za nje si kama zimezuiwa zote. Na rais hajasema kama hatasafiri. HILO NALO JOKA LA MDIMU LINAKOSOA

2. Vingine vinakosolewa kulingana na muda wenyewe si sawa kufanya hivyo. Rais ana miezi mitatu Mtu anataka awe amekamilisha ahadi zote. Mtu anakosoa ati hivyo VIWANDA VIPO WAPI??? ALISEMA KUTAKUWA NA KODI RAFIKI MBONA HATUONI..... ALISEMA ATABORESHA MASLAHI MBONA KIMYA


AAAAAH jamani.. tuvute subira panapostahili subira na tukosoe panapostahili
 
Back
Top Bottom