mpaka wa Holili kilimanjaro Tabu tupu

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
MAMLAKA YA Mapato Tanzania (TRA), imepewa changamoto ya kufanya utafiti wa bidhaa zinazoingia nchini kutoka Kenya kupitia mpaka wa Holili, Mkoa wa Kilimanjaro ni nyingi tofauti na zinazopelekwa Kenya.
Changamoto hiyo imetolewa mwishoni mwa wiki iliyopita na Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, alipozungumza na wafanyakazi wa TRA, Idara ya Uhamiaji na Polisi wa kituo cha mpakani cha Holili.

Mkullo alipewa taarifa kuwa eneo la mpakani na Kenya kuna njia haramu za kuingiza na kusafirisha bidhaa kwenda nchi jirani zipatazo 450, taarifa ambayo ilimshtua waziri na kuahidi kushughulikia suala hilo kuongeza mapato ya serikali.
“Ni vigumu kwa serikali kujua mapato yake halisi kama mianya ya kukwepa ulipaji kodi stahili haitazibwa,” alisema Mkullo na kuongeza kuwa, tatizo la njia haramu za kutoa na kuingiza bidhaa ni kubwa linalopaswa kushughulikiwa kwa pamoja na nchi zote za mipakani, hususan Jumuiya ya Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki.
Awali, Meneja wa TRA mkoani Kilimanjaro, Patience Minga, alimweleza Mkullo kuwa Kenya imeingiza nchini, kupitia Kituo cha Holili, bidhaa mbalimbali zenye thamani ya Sh16,735,365,150.

Baadhi ya bidhaa hizo ni mafuta ya kupikia, bati, sabuni za kufulia, chumvi, mablanketi na sufuria.
“Ukilinganisha uingizaji bidhaa wa mwaka 2008 ilikuwa sawa na thamani ya Sh9,405,714,285 na usafirishaji bidhaa kwenda Kenya zilikuwa na thamani ya Sh823,340,984,” alisema Minga.

Alisema hivi sasa bidhaa hizo zinalipiwa Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwa mujibu wa uhalisia wake na kwamba, kwa Afrika ya Mashariki Ushuru wa Forodha ni asilimia sifuri kuanzia Januari mwaka huu.
Pia, alimjulisha waziri kuwa TRA imezindua mfumo wa Central Data Processing Office Makao Makuu ya Forodha, Dar es Salaam ili kurahisisha utengenezaji nyaraka zote za bidhaa na makadirio ya ushuru wa forodha.

Wakati huo huo, TRA mkoani Kilimanjaro imekusanya mapato ya Sh56.8 bilioni kutoka Idara ya Forodha na Idara ya Kodi za ndani, hivyo kufikia lengo la asilimia 99.6 ya makadirio ya Sh57 bilioni kwa mwaka wa 2009/10.
Kwa kipindi cha bajeti ya mwaka huu, Julai hadi Novemba TRA Kilimanjaro imekusanya Sh25 bilioni ambazo ni asilimia 83.6 ya Sh30 bilioni zinazokadiriwa kukusanywa.
 
Back
Top Bottom