''KAMA UNAWEZA KUMWONA HUYO ULIYENAE AKIKUFUNGIA VIFUNGO VYA BLAUZI UZEENI WAKATI WEWE HUWEZI TENA, BASI HUYO NDIE''.Kwahiyo kama unaweza kuona mkiwa pamoja miaka mingi baadae, wakati nguvu za kufanya mambo unayofanya mwenyewe huna tena na mwenzako akikusaidia basi ujue umempata mtu ambae anakufaa, moyo wako umemkubali.
Dah!Lizzy tatizo ni kwamba watu wengi wako selfish. wanataka wafungiwe vifingo vya shati wenyewe, ila wenyewe wasifungiani...
Kuna mtu alinambia kua from the moment alikua 35 years (10 years baada ya ndoa) alikua hana tena hisia na mume wake ila aliendelea kubaki ndani kwa kuogopa stigma ya mwanamke alie achika. then from miaka 45 (20 years baada ya ndoa) akawa na uwezo wa kuomba divorce but she refrained sababu alikua na hope kua mume wake (who was almost 60 by then) atakufa na kumuachia mali yote...
Alipo nihadithia alikua almost 50, na mume wake bado alive, nguvu tele. Maybe anaweza kufa yeye kabla...Dah!
Kwahiyo miaka yote hiyo akavumilia kwa woga na matumaini ya mume kutangulia kabla yake mwisho akajikuta hana kitu?Inasikitisha kweli, hapo mzee wa watu si ajabu alikua anampenda mama bila kipimo kumbe mwenzie anamwombea kifo.
Hahahahaha, simnapumzishana kila baada ya mida bana?Hamna haja ya kugandana siku zote 365, mnapeana hizo 65 kwaajilia ya kukosana kidogo ili mapenzi yenu yaendelee kunoga.Inatisha, till death do us part.
Amka, sinzia, safiri, nuna, cheka duh mtu yupo tu
ila mkizeeshana kuna raha yake.
Yote hiyo ni kwasababu watu wanaingia kwenye ndoa bila kujua wanachofuata, watakayopata na watakayokosa.Matokeo yake ndio hapo vijana ndoa zinavunjikia ujanani, kwa kutojua na kutokua tayari kupambana na vikwazo vinavyoweza kujitokeza. Unakuta watu wanaingia ili maisha yawe mazuri (nyumba, magari, pesa), ili wapate sifa (sura , maumbo, fame vya hao watarajiwa wao) n.kNi maneno mazuri saana hasa kama yangekua yanawezekana.... Lizzy dear... Haya ni mafundisho kuhusiana na ndoa ambayo miaka nenda rudi hayabadiliki, ni maneno ambayo yametolewa kama muongozo wa watu kujua/kutafuta ama kupata mchumba; Pamoja na yale ya jinsi ya kuhakikisha unampata mtu ambae anafaa kua mwenza mara nyingi ikisukwa na dini.... Uzuri ni kwamba pamoja na kusema dini zatofautiana, katika mambo kama haya zafanana sababu culture plays it role hasa with its elements katika marriage institution.
However hayo mafundisho hayajazingatia kubadilika kwa maisha na life circumstances.... Most importantly hata watu wenyewe.... Kijana wa leo sio kijana wa kale... Walau wanaume kidogo wapo constant (thou nao wapungua at a pace kubwa) kuliko wadada. Hii inafanya kua vijana wanapo kutana... Hope ya kusema watafika hapo kwenye picha toka ujanani ni very minimal.... Labda waje waoane utu uzima, kila mmoja aliachika na kupata second chance....
Hapo alikua akimaanisha mabadiliko ya kimuonekano ama?...Nilishawahi kusoma mahali: Kijana alimwambia mama yake mzazi kuwa amepata mchumba. Mama mtu akamuuliza kijana wake: "Umeshawahi kumuona mama yake huyo binti?" Kijana akasema bado na kumuuliza ***** kisa cha kutaka akumuone mama ya binti kwanza. Mama yake akajibu: "Kwa kuwa baada ya muda huyo malaika wako atakuwa jinsi alivyo mama yake leo. UTAENDELEA KUMPENDA BADO?"
Leo kuna mwalimu wetu ametuambia ushauri aliopewa kuhusu ndoa , na nani?Hakutwambia.
Kutoka........
....mpaka.....
Neway ushauri wenyewe unasema hivi ''KAMA UNAWEZA KUMWONA HUYO ULIYENAE AKIKUFUNGIA VIFUNGO VYA BLAUZI UZEENI WAKATI WEWE HUWEZI TENA, BASI HUYO NDIE''.Kwahiyo kama unaweza kuona mkiwa pamoja miaka mingi baadae, wakati nguvu za kufanya mambo unayofanya mwenyewe huna tena na mwenzako akikusaidia basi ujue umempata mtu ambae anakufaa, moyo wako umemkubali.
That got me thinking, hivi ni wangapi waliopo kwenye uchumba na walioingia ndoani tayari wanafikiria hata kuwa pamoja na wenzi wao miaka minne mitatu mbele huku wakiwa na furaha? Hapo ulipo, unamwonaje mwenzi wako,Akizeeka, au hata akipata matatizo tu ambayo yatamfanya akutegemee wewe kwa kiasi kikubwa will you be there for him/her completely?No regrets or complaints? Utamsaidia kwa fahari? Au ndio utatamani Mungu amchukue mapema???
I hope the answers are YES, DEFINATELY, ABSOLUTLY NO REGRETS, YES and GOD NO!
Kama sio pole kwa kuwa kwenye ndoa na mtu ambae hajaziteka hisia zako kikamilifu. Naomba Mungu wale ambao bado wapo wapo siku wakiamua kuuga ukapera watatafuta watu ambao wanakubalika mioyon, nafsini na akilini mwao ili wimbi wa ndoa zinazovunjika ama zile zinazozaa manyanyaso/dharau/udanganyifu na mengineyo yapungue.
Yote hiyo ni kwasababu watu wanaingia kwenye ndoa bila kujua wanachofuata, watakayopata na watakayokosa.Matokeo yake ndio hapo vijana ndoa zinavunjikia ujanani, kwa kutojua na kutokua tayari kupambana na vikwazo vinavyoweza kujitokeza. Unakuta watu wanaingia ili maisha yawe mazuri (nyumba, magari, pesa), ili wapate sifa (sura , maumbo, fame vya hao watarajiwa wao) n.k
Wanachofikiria ni namna gani watauza majina mjini, gari gani ataendesha miaka mitatu mbeleni, ataenda wapi vacation, nyumba ya aina gani wataishi, wara ngapi watakula hotelini na sio nini kitatokea iwapo hivyo vinavyomshawishi kuingia ndoani vitakua havipo tena.Umbo la mke likikongoroka baada ya kuzaa, sura ikichoka kidogo, pesa za mume zikiisha, akifukizwa kazi, mmoja akipata ulema and so on.
Najua wapo wanaokua tricked ,makucha yanafichwa
alafu baada tu ya ndoa ghafla bin vooom mwenzi
kabadilika. Kwa style hiyo hata wakioana uzeeni kuna nafasi kubwa sana ya hiyo ndoa kufa iwapo mambo yatabadilika tofauti na matarajio yao.
Till death do us part is not reality for many people. It's not easy getting to the finish line in marriage. In fact, it can be extremely difficult to finish the line.
Someone has said, not PAW or Invisible "Marriage is an institution that simplifies life but complicates living.
Well mabadiliko hayawezi kutokea kama wahusika hawatokua wanajua athari za kuingia kwenye ndoa kwaajili ya vitu badala ya mtu, na bila kujiandaa kifikra na kihisia. Kwahiyo tunachoweza kufanya ni kujifunza na kuelimishana kutokana na makosa ya wale ambao yameshawakuta tayari. Mf. Kwasababu mimi najua(kwa kusikia na kuona) matatizo wanayopata wale waliokosea step ntajitahidi na mimi nisiishie huko, hivyo kinachohitajika ni ufahamu na uelewa wa ndoa kiundani.Hii post umeeleza hapa hasa ndio hivo Lizzy, Labda swali naomba kujua how do you think inaweza kua controlled? Kwamba watu waweze jitambua na hii system ya sasa inayokua kwa kasi iweze badilika walau kuweza pata ndoa ambazo ni quality zenye hope of a better future?
Salama kabisa kakondoo,
Siku ukipata mtihani kwenye hili somo alafu ukafeli ntakucharazaaa.