Mpaka uzeeni nikikosa hiki kitu nitaumia sana,ipo sababu ya kukipigania sana.Karibu tuelimishane!

Aliomba hekima kwa kuwa ku control wake 700 na bado akawa na masalia 300 si mchezo,, hekima muhimu mzee


Hii lazima Bavicha watapinga,,
 
Bora wewe umechagua fungu jema, hekima.
Kuna chizi mmoja yuko humu, yeye kazi yake ni kutukananana na watu, na anatukana hadi watu wenye heshima zao, watu ambao wanaheshimika ki-taifa na kimataifa. Ningekuwa na mamlaka, huyu mtu angetakiwa arudi hapa Tanzania in 24 hours na bila kujali kama kuna corona. Mtu hawezi kuwa anatukana tu kila mahali kisa yuko mtandaoni.
 
hahah
sawa sawa mkuu nataka kujifunza zaidi

Ila pole sana mkuu nahisi kakuuzi,matatizo ya kibinadamu hayo,yanachosha kweli kweli! Hamna jinsi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
aliomba ka sababu vingine vyote alisha kabidhiwa zamani sana......
sasa mkuu ukichunguza kwenye kisa cha biblia kinasema hivi:-

Usiku ule Mungu akamtokea Sulemani, akamwambia, Omba utakalo nikupe. Sulemani akamwambia Mungu, Umemfanyia baba yangu Daudi fadhili kuu, nawe umenimilikisha mimi badala yake. Basi sasa, Ee BWANA Mungu, na limyakinie baba yangu Daudi neno lako; maana umenitawaza niwe mfalme juu ya watu wengi kama mavumbi ya nchi.

Sulemani akasema hivi

Basi sasa nipe hekima na maarifa,

Na Mungu akamwambia Sulemani, Kwa sababu neno hili lilikuwamo moyoni mwako, wala hukujitakia mali, wala utajiri, wala utukufu, wala maisha za wakuchukiao, wala hukujitakia maisha ya siku nyingi;


unaona inaonyesha kuwa alikuwa hana utajiri wala nini hukujitakia mali, wala utajiri, wala utukufu


Bali umejitakia hekima na maarifa, upate kuwahukumu watu wangu, niliokutawaza juu yao; basi hekima na maarifa umepewa;




Alafu inaonyesha sasa baada ya kupewa Hekima Mungu akamwambia hivi


Nami nitakupa mali, na utajiri, na utukufu, kupita walivyokuwa navyo wafalme wote waliokuwa kabla yako, wala baada yako hapatakuwa na mtu atakayekuwa navyo.


Sasa Narudi tena kule mwanzo,ni kwa nini hakuhitaji kitu kingine?!?????

Na baada ya kepewa vyote hivi akazidishiwa utajiri na Mali na maarifa juu????

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…