Mpaka uzeeni nikikosa hiki kitu nitaumia sana,ipo sababu ya kukipigania sana.Karibu tuelimishane!

Aliomba hekima kwa kuwa ku control wake 700 na bado akawa na masalia 300 si mchezo,, hekima muhimu mzee


Hii lazima Bavicha watapinga,,
 
Nimejaribu kudadavua kwa kiasi suala la Hekima haswa Hekima ya Sulemani/Suleimani kupitia vyanzo mbalimbali ili nipate muafaka wa maswali niliyoyauliza mwishoni.

Pia nimejaribu kuweka mpangilio mzuri ili kutokukufanya kukata tamaa kusoma makala hii,kwa sabbu akili zetu tunazijua kwenye masuala ya kusoma

KARIBUNI!

tunaona kuwa HEKIMA: ni hali bora ya mtu katika kutambua ukweli wa binadamu, vitu, matukio na mazingira mbalimbali hata kuchagua vizuri la kufanya.

Katika dini mbalimbali inatokana na imani kwa Mungu.

Katika Ukristo inatajwa pengine kati ya vipaji vya Roho Mtakatifu vinavyokamilisha maadili ya kiutu na maadili ya Kimungu vilevile.

Hapa nitaelezea kisa cha Sulemani kikristo na Suleimani kwa upande wa Kiislamu

Katika Biblia kuna kisa kimoja cha Sulemani aliomba hekima kuliko mali, wala utajiri, wala utukufu, wala maisha ya ajabu ajabu, wala hukujitakia maisha ya siku nyingi.

Tunaona Usiku ule Mungu akamtokea Sulemani, akamwambia, Omba utakalo nikupe. Sulemani akamwambia Mungu, Umemfanyia baba yangu Daudi fadhili kuu, nawe umenimilikisha mimi badala yake. Basi sasa, Ee BWANA Mungu, na limyakinie baba yangu Daudi neno lako; maana umenitawaza niwe mfalme juu ya watu wengi kama mavumbi ya nchi.

Basi sasa nipe hekima na maarifa, nijue kutoka na kuingia mbele ya watu hawa; kwa kuwa ni nani awezaye kuwahukumu watu wako hawa walio wengi?

Naye Mungu akamwambia Sulemani, Kwa sababu neno hili lilikuwamo moyoni mwako, wala hukujitakia mali, wala utajiri, wala utukufu, wala maisha za wakuchukiao, wala hukujitakia maisha ya siku nyingi;

Bali umejitakia hekima na maarifa, upate kuwahukumu watu wangu, niliokutawaza juu yao; basi hekima na maarifa umepewa;

Nami nitakupa mali, na utajiri, na utukufu, kupita walivyokuwa navyo wafalme wote waliokuwa kabla yako, wala baada yako hapatakuwa na mtu atakayekuwa navyo.


KWA UPANDE WA KIISLAMU



nilijaribu kufuatilia sana baadhi ya maeneo bila kufanikiwa lakini nilipata somo kubwa sana kwenye upande huu wa pili.

Na Suleiman alimrithi Daud.

Daud (a.s.) ni katika kizazi cha Ya’qub bin Is-haq bin Ibrahim. Mwenyezi Mungu alimtukuza kwa utume, akamteremshia Zabur, akamfanya ni khalifa katika ardhi, akamuhusisha kuwa na sauti nzuri zaidi na akamlainishia chuma. Yeye ni mfalme wa pili wa dola ya kiyahudi.

Alipewa jina la Mfalme Daud. Mfalme wa kwanza alikuwa ni Talut, kama alivyosema Mwenyezi Mungu:

Tunaona kuwa maneno yanasema Hakika Mwenyezi Mungu amewachagulia Talut kuwa mfalme.” Juz. 2 (2:247).

Mwanawe Suleiman (a.s.) alikuwa ni mtume vile vile. Naye Mwenyezi Mungu alimpa neema nyingi, zikiwemo kurithi ufalme wa baba yake. Historia inasema kuwa ufalme wao uliendelea kwa miaka sabini.

Hakika tulimpa Daud na Suleiman elimu, iliyowaongoza kwenye utiifu wa Mwenyezi Mungu na manufaa ya watu. Wala hawakujivuna nayo kwa waja wa Mungu au kuvumbua nayo silaha za maangamizi ili kuwakandamiza wanyonge wawanyonye nyenzo zao.

Bali hawa wawili walimtii Mwenyezi Mungu katika maamrisho yake na makatazo yake na wakamshukuru kwa neema ya elimu ambayo hailinganishwi na chochote na wakasema: Sifa njema zote (alhamdu lillah) ni za Mwenyezi Mungu ambaye ametufadhilisha kuliko wengi katika waja wake waumini.

Makusudio ya kufadhilishwa (kufanywa bora) hapa, ni kufadhilishwa kwa elimu yenye manufaa. Maana ya kuiliko wengi katika waumini ni wale wasiofikia cheo chao cha elimu.

Hapo kuna ishara kuwa katika waumini wako waliofadhilishwa zaidi yao. Na hivyo ndivyo ilivyo.

Kwa vyovyote iwavyo ni kuwa ubora mbele ya Mwenyezi Mungu haupimwi kwa elimu wala kwa kuupeleka upepo au kulainisha chuma; isipokuwa ni kwa manufaa ya watu na masilahi yao.

Kisa cha nabii suleiman a.s

Nabii suleiman a.s ni mtoto wa nabii daud a.s,M/Mungu aliwatuma wote hao wawili kwa watu wa banii israail.

Nabii suleiman a.s alirithi utume pmj na ufalme kutoka kwa baba ake nabii daud a.s

Utawala wao ulikuwa ni utawala wenye uadilifu pmj na hekma wakiwaongoza walio chini yao kwa kuwahurumia.

Nabii suleiman a.s aliendeleza kuwaongoza viumbe wa M/Mungu baada ya baba ake nabii daud a.s

Kwa uwezo wa M/Mungu nabii suleiman a.s aliweza kuwaongoza viumbe wengi wakiwemo binadamu majini ndege upepo pmj na kutambua lugha zao

Kwa ushahidi qur,an Surat sabai aya 12-13.

Kama M/Mungu alivyomfahamisha nabii suleiman a.s lugha ya ndege pmj na wanyama.

M/Mungu alimdhalilishia majeshi ya binadamu majini ndege akiwaongoza na wakimsikiliza kwa lile alisemalo.

Siku moja nabii suleiman a.s alikuwa akitembea pmj na majeshi yake ya binadamu majini pmj na makundi ya ndege wakiwa angani.

Mara nabii suleiman a.s akasikia sauti ya sisimizi ikisema.

"Enyi sisimizi wenzangu ingieni ktk mashimo yenu,asije akawakanyaga suleiman a.s pmj na majeshi yake ilihali wao hawajui."

Kwa ushahidi qur,an surat namli aya ya 18.

Nabii suleiman a.s aliposikia maneno ya sisimizi huyo akatabasamu na kuinua mikono yake juu akimshukuru M/Mungu kwa neema aliyompa.

Pia nabii suleiman a.s alikuwa na hekma pmj na busara tokea utotoni mwake.

Siku moja nabii daud alipokuwa amekaa pmj na mtoto wake nabii suleiman a.s mara wakaja watu wawili.

SASA WAKUU MIMI NINATAKA KUJUA NI KWA NINI SULEMANI/SULEIMANI ALIOMBA ZAIDI HEKIMA?? NA MAARIFA?? Kuliko chochote?

Na jee!? Kwenye Hekima kumejificha siri gani?

Na Jee? Kwa nini kuna msemo kuwa Hekima hainunuliwi!? Maana yake mtu anazaliwa nayo automatic???

Mimi naamini humu ndani kuna wachambuzi wazuri na wabobezi wa haya masuala mtatupa muafaka wa hili jambo KARIBUNI SANA.

ONYO! kama huna la kujibu usilete masihara kwenye kazi

NAWASILISHA



Sent using Jamii Forums mobile app
Bora wewe umechagua fungu jema, hekima.
Kuna chizi mmoja yuko humu, yeye kazi yake ni kutukananana na watu, na anatukana hadi watu wenye heshima zao, watu ambao wanaheshimika ki-taifa na kimataifa. Ningekuwa na mamlaka, huyu mtu angetakiwa arudi hapa Tanzania in 24 hours na bila kujali kama kuna corona. Mtu hawezi kuwa anatukana tu kila mahali kisa yuko mtandaoni.
 
Bora wewe umechagua fungu jema, hekima.
Kuna chizi mmoja yuko humu, yeye kazi yake ni kutukananana na watu, na anatukana hadi watu wenye heshima zao, watu ambao wanaheshimika ki-taifa na kimataifa. Ningekuwa na mamlaka, huyu mtu angetakiwa arudi hapa Tanzania in 24 hours na bila kujali kama kuna corona. Mtu hawezi kuwa anatukana tu kila mahali kisa yuko mtandaoni.
hahah
sawa sawa mkuu nataka kujifunza zaidi

Ila pole sana mkuu nahisi kakuuzi,matatizo ya kibinadamu hayo,yanachosha kweli kweli! Hamna jinsi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
aliomba ka sababu vingine vyote alisha kabidhiwa zamani sana......
sasa mkuu ukichunguza kwenye kisa cha biblia kinasema hivi:-

Usiku ule Mungu akamtokea Sulemani, akamwambia, Omba utakalo nikupe. Sulemani akamwambia Mungu, Umemfanyia baba yangu Daudi fadhili kuu, nawe umenimilikisha mimi badala yake. Basi sasa, Ee BWANA Mungu, na limyakinie baba yangu Daudi neno lako; maana umenitawaza niwe mfalme juu ya watu wengi kama mavumbi ya nchi.

Sulemani akasema hivi

Basi sasa nipe hekima na maarifa,

Na Mungu akamwambia Sulemani, Kwa sababu neno hili lilikuwamo moyoni mwako, wala hukujitakia mali, wala utajiri, wala utukufu, wala maisha za wakuchukiao, wala hukujitakia maisha ya siku nyingi;


unaona inaonyesha kuwa alikuwa hana utajiri wala nini hukujitakia mali, wala utajiri, wala utukufu


Bali umejitakia hekima na maarifa, upate kuwahukumu watu wangu, niliokutawaza juu yao; basi hekima na maarifa umepewa;




Alafu inaonyesha sasa baada ya kupewa Hekima Mungu akamwambia hivi


Nami nitakupa mali, na utajiri, na utukufu, kupita walivyokuwa navyo wafalme wote waliokuwa kabla yako, wala baada yako hapatakuwa na mtu atakayekuwa navyo.


Sasa Narudi tena kule mwanzo,ni kwa nini hakuhitaji kitu kingine?!?????

Na baada ya kepewa vyote hivi akazidishiwa utajiri na Mali na maarifa juu????

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom