kibaravumba
JF-Expert Member
- Dec 21, 2012
- 6,635
- 7,005
Ili nchi zetu hizi maskini zisonge mbele,zinahitaji aina ya viongozi wenye maamuzi magumu yanayozingatia uhalisia wa mazingira tuliyo nayo na si kukopi maamuzi kwa kuangalia wakoloni wetu wanafanyaje.
Changamoto pekee ambayo naona Rais wa sasa hajaigusa,ni eneo la elimu.
Alichofanya pekee ni kumwaga pesa za elimu bure na mikopo ya vyuo vikuu bila kijiuliza hiyo elimu unayowekeza pesa hizo ni elimu gani!
Kwa sasa anatakiwa rais ambaye atakuja kufumua kabisa mfumo huu wa elimu unaozalisha watu wajinga wengi wenye vyeti vikubwa.
Inahitaji aina fulani ya ukichaa kubadili mambo.
Kuna watu wanajiita maprofesa na madaktari wenye mawazo mgando sana.
Kwa maoni yangu,mambo yafuatayo ni ya kuangalia upya:
1. Elimu ya msingi -kwa nini miaka saba,nini wanajifunza huko?Yana msaada gani katika jamii yetu ya sasa kama mtu anaweza kumaliza shule asione umuhimu wa kutochafua mazingira yake mwenyewe?
2. Elimu ya sekondari kwa nini miaka sita?Kwa nini miaka miwili ya advanced certificate?Wanasoma nini katika elimu ya sekondari?Je miaka minne mbona ina mambo machache ambayo ni kama kupoteza muda tu iwapo mtu anaweza kuyasoma miaka miwili?
3. Elimu ya vyuo vya kati.Mitaala ni halisi ama ni ya kibabaishaji tu?Kwa nini haisaidii nchi kuzalisha bidhaa zinazotumika sana kwenye mazingira yetu?Vinaitwa Technical Institutions ni ufundi upi?Je unakidhi kweli?Kwa nini hakuna ubunifu kama ilivyo nchi kama china?
4. Elimu ya vyuo vikuu.Je lengo lake ni nini iwapo tunaona wahitimu wengi hawana mwelekeo na wasomi wanapigana vikumbo kwenye siasa tu?
Wangapi wanasoma mambo meengi sana ambayo hawayafanyii kazi hadi wanakufa?Kuna haja ya kulazimisha kusoma kila kitu kwa ajili tu ya kupata ugumu wa kupata degree?Au ni muhimu kusoma vitu ili kusaidia akili iweze kuwa na ubunifu?Leo nikisikiliza kipindi cha njiapanda,nimesikia mhitimu wa udom aliyesoma memkwa hadi kupata degree yake ya ualimu eti hakumbuki kirefu cha memkwa!
5. Malipo ya mshahara,posho,marupu rupu lazima yawe makubwa kuliko kada nyingine yoyote ili kuvutia ushindani wa watu wenye akili kuingia kwenye kada hii.
6.Kuwekeza sana kwenye elimu ya IT kwa kiwango kinachoweza kuwashangaza wengi na kupuuza masomo yanayopoteza muda kama uraia,historia(ambayo ni feki) na kuyafanya kama vitabu vya hadithi tu,ila kwa mtu anayeomba kazi yanakuwa kama added advantage.Ama yanafundishwa jeshini tu k.v jkt
Nchi hii haitasonga kwa hizi elimu za kukariri na kuwaita wale wenye uwezo wa kukariri eti "wenye akili" na kupata vyeti na GPA nyingine za kuhonga ngono.