Mpaka sasa CCM imepasuka, inasubiri ipasuke zaidi tu

Mpaka sasa CCM imepasuka, inasubiri ipasuke zaidi tu

Tunaposema CCM imepasuka wakereketwa wanafura kwa hasira. Chama hiki kilishapasuka mara nyingi lakini ile ya 2015 na kinachoendelea ni athari za mpasuko huo. Leo Miiko ya CCM imewekwa pembeni, kuna makundi na visasi.
 
Nani atabisha CCM sasa ina makundi ya kimaslahi? sasa hivi kuna CCM ya Magufuli na watu wake na kulikuwa na CCM ya Kikwete na watu wake. Huu ni mtondogoo wa Mpasuko.
 
Sina wasiwasi kwa kupasuka kwa ccm ni kawaida
lakini wanautaratibu wao kurekebishana kaonywa kwenye vikao vya ndani na mambo yakalia na kuwa kitu kimoja
 
Huo ndio ukweli. Ubaya ni kuwa kupasuka kwa CCM ni kupasuka kwa nchi. CCM imejitahidi kuhimili dhoruba kwa miaka tofauti lakini kidogo kidogo imeendelea kupasuka na sasa ni dhahiri.

Kuelekea uchaguzi wa 2015 CCM ilikaribia kutumbukia shimoni wote mnakumbuka kilichompata Lowasa Kada mkongwe na mwanamikakati wa zamani wa mtandao. Kupatikana Mgombea Mh Magufuli ni kwa ajali ambayo na sasa inakinyemelea tena chama hiki kikongwe. Tunapozungumza chama kimegawika tayari ingawa hawataki kukiri. Kuna CCM Masalia, CCM mpya na CCM majeruhi.

Hili kundi la Majeruhi ni kubwa linaingiza waliokuwepo madarakani kabla ya Mh Magufuli kuwa madarakani na ambao sasa wamepoteza nafasi zao serikalini na ushawishi kwenye chama. Hawa ni kundi la waliokipigania chama kuingia madarakani kwa hali na mali, 2015 . CCM masalia ni wale ambao hawakuwa na mirengo wakati wa kuelekea 2015 kwenye uchaguzi. Hawa ni wanachama wa kawaida na watiifu kwa chama. Kundi la Tatu ni CCM mpya. Hili ni zao la Magufuli baada ya kuingia madarakani. Hawa ni miongoni mwa waliokuwa wapinzani na CCM waliotupwa wakati wa Kikwete ambao sasa wanafaidi matunda. Hawa ni watetezi wa Magufuli na Serikali yake hata kama kuna udhaifu wowote. Ni wapiga filimbi na watetezi wa hali na mali. CCM ina makundi tayari na imepasuka kitambo.

Kinachoendelea kwa akina Musiba na wastaafu Kinana na Makamba ni ushahidi wa wazi wa kimazingira na maadili kuwa CCM imepasuka. Kwenye CCM kuna visasi na kulipizana.

CCM ZANZIBAR.
Kule kuna Anguko , inajulikana kuwa CCM ilipasuka na kunguka kuelekea 2015. Hasa pale waandamizi walipojiengua na kujiunga Upinzani. Hao walikuwa wana mikakati walioipa CCM ushindi kwa miaka ya 2000, 2005 na 2010. Mpasuko ule uliupa Upinzani nguvu za ajabu na kurahisisha kazi ya CCM kubwagwa kwenye uchaguzi wa 2015 uliofutwa na Jecha. Mzimu ule bado upo hasa kwenye Ajenda ya Zanzibar Huru.

Kuelekea 2020 CCM Zanzibar imegawanyika sana. Taarifa tulizonazo kuna fukuto la uraisi kuelekea 2020 na tayari kuna makambi na mnyukano mkali. Kuna mikakati ya kimya kimya waandamizi wanahujumiana serikalini. Kitendo cha aliyekuwa Waziri wa fedha Bwana Khalidi kuondolewa Uwaziri kunahusishwa na mnyukano huo. Zipo taarifa kule kwamba kambi za Uraisi zinatiliana fitna kwenye chama na kila anayeonekana adui anaundiwa zengwe ndani ya serikali na chamani.

Kitendo cha Musiba kuwahusisha viongozi wa SMZ na hujuma kwa Serikali ya Magufuli si chema na ni ishara kuwa kuna namna inaendelea kule ambayo wakubwa haiwapendezi.

Narudia kusema CCM imeasuka zamani na inasubiri kupasuka zaidi.

TATIZO.
Wakati mnyukano na visasi ukiendelea Vyombo vya Dola navyo vinapata shida katika kusimamia maadili ya kazi na hatima yake wananchi na raia wanaumizwa.Haki inapotea na visasi kuzidi. Mpasuko wa CCM unaiumiza Tanzania.

Bila CCM Tanzania inawezekana.

Kishada.
Ni suala la muda tu
 
Sina wasiwasi kwa kupasuka kwa ccm ni kawaida
lakini wanautaratibu wao kurekebishana kaonywa kwenye vikao vya ndani na mambo yakalia na kuwa kitu kimoja
Hako kautaratibu wanako na kamekuwa kakiwasaidi sana lakini sio kwa kipindi hiki ambacho wanatukanana hadharani kitu ambacho hatukuwahi kuona, pia kipindi hiki hakuna kubembelezana kila kiongozi amejaa ubabe.
Je unadhani wale wazee waliotukanwa wapumbavu hadharani unadhani wanakinyongo kiasi gani?
 
[/QUOT
Yaani mpaka imefika mahala Makatibu Wakuu wasataafu wakaomba ushauri kwa viongozi wa Dini, wastaafu wenzao, na wasomi juwa kwamba walishagonga mwamba. Hata Katibu wa Baraza la Wazee kuwashauri wajibu mapigo kwenye Media ni ushahidi kuwa CCM imepasuka na hakuna kinachofuatwa kuhusu itikadi na maadili ya chama.
 
Back
Top Bottom