Mpaka sasa CCM imepasuka, inasubiri ipasuke zaidi tu

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,224
3,290
Huo ndio ukweli. Ubaya ni kuwa kupasuka kwa CCM ni kupasuka kwa nchi. CCM imejitahidi kuhimili dhoruba kwa miaka tofauti lakini kidogo kidogo imeendelea kupasuka na sasa ni dhahiri.

Kuelekea uchaguzi wa 2015 CCM ilikaribia kutumbukia shimoni wote mnakumbuka kilichompata Lowasa Kada mkongwe na mwanamikakati wa zamani wa mtandao. Kupatikana Mgombea Mh Magufuli ni kwa ajali ambayo na sasa inakinyemelea tena chama hiki kikongwe. Tunapozungumza chama kimegawika tayari ingawa hawataki kukiri. Kuna CCM Masalia, CCM mpya na CCM majeruhi.

Hili kundi la Majeruhi ni kubwa linaingiza waliokuwepo madarakani kabla ya Mh Magufuli kuwa madarakani na ambao sasa wamepoteza nafasi zao serikalini na ushawishi kwenye chama. Hawa ni kundi la waliokipigania chama kuingia madarakani kwa hali na mali, 2015 . CCM masalia ni wale ambao hawakuwa na mirengo wakati wa kuelekea 2015 kwenye uchaguzi. Hawa ni wanachama wa kawaida na watiifu kwa chama. Kundi la Tatu ni CCM mpya. Hili ni zao la Magufuli baada ya kuingia madarakani. Hawa ni miongoni mwa waliokuwa wapinzani na CCM waliotupwa wakati wa Kikwete ambao sasa wanafaidi matunda. Hawa ni watetezi wa Magufuli na Serikali yake hata kama kuna udhaifu wowote. Ni wapiga filimbi na watetezi wa hali na mali. CCM ina makundi tayari na imepasuka kitambo.

Kinachoendelea kwa akina Musiba na wastaafu Kinana na Makamba ni ushahidi wa wazi wa kimazingira na maadili kuwa CCM imepasuka. Kwenye CCM kuna visasi na kulipizana.

CCM ZANZIBAR.
Kule kuna Anguko , inajulikana kuwa CCM ilipasuka na kunguka kuelekea 2015. Hasa pale waandamizi walipojiengua na kujiunga Upinzani. Hao walikuwa wana mikakati walioipa CCM ushindi kwa miaka ya 2000, 2005 na 2010. Mpasuko ule uliupa Upinzani nguvu za ajabu na kurahisisha kazi ya CCM kubwagwa kwenye uchaguzi wa 2015 uliofutwa na Jecha. Mzimu ule bado upo hasa kwenye Ajenda ya Zanzibar Huru.

Kuelekea 2020 CCM Zanzibar imegawanyika sana. Taarifa tulizonazo kuna fukuto la uraisi kuelekea 2020 na tayari kuna makambi na mnyukano mkali. Kuna mikakati ya kimya kimya waandamizi wanahujumiana serikalini. Kitendo cha aliyekuwa Waziri wa fedha Bwana Khalidi kuondolewa Uwaziri kunahusishwa na mnyukano huo. Zipo taarifa kule kwamba kambi za Uraisi zinatiliana fitna kwenye chama na kila anayeonekana adui anaundiwa zengwe ndani ya serikali na chamani.

Kitendo cha Musiba kuwahusisha viongozi wa SMZ na hujuma kwa Serikali ya Magufuli si chema na ni ishara kuwa kuna namna inaendelea kule ambayo wakubwa haiwapendezi.

Narudia kusema CCM imeasuka zamani na inasubiri kupasuka zaidi.

TATIZO.
Wakati mnyukano na visasi ukiendelea Vyombo vya Dola navyo vinapata shida katika kusimamia maadili ya kazi na hatima yake wananchi na raia wanaumizwa.Haki inapotea na visasi kuzidi. Mpasuko wa CCM unaiumiza Tanzania.

Bila CCM Tanzania inawezekana.

Kishada.
 
Bado sana ww huijui ccm,ilishapita vizingiti zaidi ya hivi ,

Ilikuwa wezi wasafishwe mapema ila ndio kujivua gamba huko ,

Walioneemeka na ccm wakaifanya Mali yao na watoto wao sasa watakimbia hata wakikimbilia chadema poa tu,

Ccm hii sio ile ya akina guninita ,makamba,kinana na wezi wengine
 
Hili kundi la Majeruhi ni kubwa linaingiza waliokuwepo madarakani kabla ya Mh Magufuli kuwa madarakani na ambao sasa wamepoteza nafasi zao serikalini na kwenye chama. Hawa ni kundi la waliokipigania chama kuingia madarakani kwa hali na mali, 2015 . CCM masalia ni wale ambao hawakuwa na mirengo wakati wa kuelekea 2015 kwenye uchaguzi. Hawa ni wanachama wa kawaida na watiifu klwa chama. Kundi la Tatu ni CCM mpya. Hili ni zao la Magufuli baada ya kuingia madarakani. Hawa ni miongoni mwa waliokuwa wapinzani na CCM waliotupwa wakati wa kikwete ambao sasa wanafaidi matunda. Hawa ni watetezi wa Magufuli na Serikali yake hata kama kuna udhaifu wowote. Ni wapiga filimbi na watetezi wa hali na mali. CCM ina makundi tayari na imepasuka kitambo.

Kinmachoendelea kwa akina Musiba na wastaafu Kinana na Makamba ni ushahidi wa wazi wa kimazingira na maadili kuwa CCM imepasuka. Kwenye CCM kuna visasi na kulipizana.

CCM ZANZIBAR.
Kule kuna Anguko , inajulikana kuwa CCM ilipasuka na kunguka kuelekea 2015. Hasa pale waandamizi walipojiengua na kujiunga Upinzani. Hao walikuwa wana mikakati walioipa CCM ushindi kwa miaka ya 2000, 2005 na 2010. Mpasuko ule uliipa Upinzani nguvu za ajabu na kurahisisha kazi ya CCM kubwagwa kwenye uchaguzi wa 2015 uliofutwa na Jecha.

Kuelekea 2020 CCM Zanzibar imegawanyika sana. Taarifa tulizonazo kuna fukuto la uraisi kuelekea 2020 na tayari kuna makambi na mnyukano mkali. Kuna mikakati ya kimya kimya waandamizi wanahujumiana serikalini. Kitendo cha aliyekuwa Waziri wa fedha Bwana Khalidi kuondolewa Uwaziri kunahusishwa na mnyukano huo. Zipo taarifa kule kwamba kambi za Uraisi zinatiliana fitna kwenye chama na kila anayeoinekana adui anaundiwa zengwe ndani ya serikali na chamani.

Kitendo cha Musiba kuwahusisha viongozi wa SMZ na hujuma kwa Serikali ya Magufuli si chema na ni ishara kuwa kuna namna inaendelea kule ambayo wakubwa haiwapendezi.

Narudia kusema CCM imeasuka zamani na inasubiri kupasuka zaidi.

TATIZO.
wakati mnyukano na visasi ukiendelea Vyombo vya Dola navyo vinapata shida katika kusimamia maadili ya kazi na hatima yake wananchi na raia wanaumizwa.

Bila CCM Tanzania inawezekana.

Kishada.
Ukiwa na dola hakuna cha kupasuka, ila kuna watu wataangamia
 
Write your reply...ccm
Huo ndio ukweli. Ubaya ni kuwa kupasuka kwa CCM ni kupasuka kwa nchi. CCM imejitahidi kuhimili dhoruba kwa miaka tofauti lakini kidogo kidogo imeendelea kupasuka na sasa ni dhahiri.

Kuelekea uchaguzi wa 2015 CCM ilikaribia kutumbukia shimoni wote mnakumbuka kilichompata Lowasa Kada mkongwe na mwanamikakati wa zamani wa mtandao. Kupatikana Mgombea Mh Magufuli ni kwa ajali ambayo na sasa inakinyemelea tena chama hiki kikongwe. Tunapozungumza chama kimegawika tayari ingawa hawataki kukiri. Kuna CCM Masalia, CCM mpya na CCM majeruhi.

Hili kundi la Majeruhi ni kubwa linaingiza waliokuwepo madarakani kabla ya Mh Magufuli kuwa madarakani na ambao sasa wamepoteza nafasi zao serikalini na ushawishi kwenye chama. Hawa ni kundi la waliokipigania chama kuingia madarakani kwa hali na mali, 2015 . CCM masalia ni wale ambao hawakuwa na mirengo wakati wa kuelekea 2015 kwenye uchaguzi. Hawa ni wanachama wa kawaida na watiifu kwa chama. Kundi la Tatu ni CCM mpya. Hili ni zao la Magufuli baada ya kuingia madarakani. Hawa ni miongoni mwa waliokuwa wapinzani na CCM waliotupwa wakati wa Kikwete ambao sasa wanafaidi matunda. Hawa ni watetezi wa Magufuli na Serikali yake hata kama kuna udhaifu wowote. Ni wapiga filimbi na watetezi wa hali na mali. CCM ina makundi tayari na imepasuka kitambo.

Kinachoendelea kwa akina Musiba na wastaafu Kinana na Makamba ni ushahidi wa wazi wa kimazingira na maadili kuwa CCM imepasuka. Kwenye CCM kuna visasi na kulipizana.

CCM ZANZIBAR.
Kule kuna Anguko , inajulikana kuwa CCM ilipasuka na kunguka kuelekea 2015. Hasa pale waandamizi walipojiengua na kujiunga Upinzani. Hao walikuwa wana mikakati walioipa CCM ushindi kwa miaka ya 2000, 2005 na 2010. Mpasuko ule uliupa Upinzani nguvu za ajabu na kurahisisha kazi ya CCM kubwagwa kwenye uchaguzi wa 2015 uliofutwa na Jecha. Mzimu ule bado upo hasa kwenye Ajenda ya Zanzibar Huru.

Kuelekea 2020 CCM Zanzibar imegawanyika sana. Taarifa tulizonazo kuna fukuto la uraisi kuelekea 2020 na tayari kuna makambi na mnyukano mkali. Kuna mikakati ya kimya kimya waandamizi wanahujumiana serikalini. Kitendo cha aliyekuwa Waziri wa fedha Bwana Khalidi kuondolewa Uwaziri kunahusishwa na mnyukano huo. Zipo taarifa kule kwamba kambi za Uraisi zinatiliana fitna kwenye chama na kila anayeonekana adui anaundiwa zengwe ndani ya serikali na chamani.

Kitendo cha Musiba kuwahusisha viongozi wa SMZ na hujuma kwa Serikali ya Magufuli si chema na ni ishara kuwa kuna namna inaendelea kule ambayo wakubwa haiwapendezi.

Narudia kusema CCM imeasuka zamani na inasubiri kupasuka zaidi.

TATIZO.
Wakati mnyukano na visasi ukiendelea Vyombo vya Dola navyo vinapata shida katika kusimamia maadili ya kazi na hatima yake wananchi na raia wanaumizwa.Haki inapotea na visasi kuzidi. Mpasuko wa CCM unaiumiza Tanzania.

Bila CCM Tanzania inawezekana.

Kishada.
[/QUOTEAisee hili li chama la mashetani naona linaelekea kaburini , vyombo vya dola wanachotakiwa kufanya ni kulinda maslahi ya nchi sio watu ,tatizo lao wanalinda mpaka wehu .
 
Write your reply..

Hili li chama la mashetani naona linaelekea kaburini ,tatizo vyombo vya dola badala ya kulinda maslahi ya nchi vinalinda watu tena wagonjwa wa akili .
 
Kwa lipi hasa mpka unasema hivyo?
Kweli vijana mliojukia siasa mtandaoni mnashida sana
 
Bado sana ww huijui ccm,ilishapita vizingiti zaidi ya hivi ,

Ilikuwa wezi wasafishwe mapema ila ndio kujivua gamba huko ,

Walioneemeka na ccm wakaifanya Mali yao na watoto wao sasa watakimbia hata wakikimbilia chadema poa tu,

Ccm hii sio ile ya akina guninita ,makamba,kinana na wezi wengine

Nani amuwajibishe nani ndani ya CCM. Ni suala la muda tu hao waliopo madarakani leo wakioondoka tu utasikia madhambi yao yanafichuliwa na watakaokuwepo madarakani wakati huo.
 
Bado sana ww huijui ccm,ilishapita vizingiti zaidi ya hivi ,

Ilikuwa wezi wasafishwe mapema ila ndio kujivua gamba huko ,

Walioneemeka na ccm wakaifanya Mali yao na watoto wao sasa watakimbia hata wakikimbilia chadema poa tu,

Ccm hii sio ile ya akina guninita ,makamba,kinana na wezi wengine
Kujivua gamba ilhali mapacha watatu wamerudi kwenye nafasi zao,wewe kumbe mtoto kwenye hizi sakata za chama chakavu.
 
Sote tunajua ccm ilishakufa tangu 2010 bara na visiwani tangu 1990 ipo madarakani kwa msaada vyombo vya dola tu
 
Bado sana ww huijui ccm,ilishapita vizingiti zaidi ya hivi ,

Ilikuwa wezi wasafishwe mapema ila ndio kujivua gamba huko ,

Walioneemeka na ccm wakaifanya Mali yao na watoto wao sasa watakimbia hata wakikimbilia chadema poa tu,

Ccm hii sio ile ya akina guninita ,makamba,kinana na wezi wengine

Hakuna wa kukimbia bali kichaa ataondoka na sijui ataenda wapi
 
endeleeni kuota ccm mara zote migogoro hutatuliwa kwa hekima na mtashangaa uchaguzi unakuja ccm wapo pamoja mtabaki midomo wazi
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom