Mpaka mawe yataongea

technically

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2016
Posts
13,553
Reaction score
57,843
1: Alianza Ole Nasha kuzuia ngorongoro isiuzwe na wamasai kuuawa akapotezwa wakaibuka wengine

2: Akaja Job Ndugai akasema nchi itapigwa mnada akapotezwa

3: Akaja Ally Kibao akagoma kununuliwa na Abdul Mtoto wa Samia akapotezwa

4: Akaja Soka akakemea utekaji na mauaji akapotezwa

5: Akaja mdude akakemea uhuni na utekaji akapotezwa.

6: Polepole akaongea ukweli kuhusu nchi akapotezwa mpaka leo hajawai kurudi

7: Heche akapiga kelele akakamatwa na kuwekwa ndani

8: Akaja Gwajima akakemea utekaji akasumbuliwa Ila imeshindikana

9: Akaja Warioba akakemea uhuni utekaji na upuuzi wa Serikali akawekwa house of arrest lakini kashinda Sasa

10: Mwamba Tundu Lissu akawatoa tongo tongo Watanzania akapewa kesi ya uhaini lakini kesi imebuma imegonga mwamba

Hamjashutuka tu Wahuni Sasa wakina Mange, Ponda, Assad, mwandamo, Mwanaharakati mzalendo, Sativa, Maria wanaonekana kuchoka lakini kila kukicha wanaibuka watu wapya

Je, mtateka na kuua watu wangapi? Hamuoni mmefika mwisho Sasa hivi mpaka mabibi na mababu wa miaka 90 wanawakosoa, watoto wanawakosoa!

Mnafikiri mtawanyamazisha watu Tena walio onja democrasia kwa miaka 20 toka mwaka 1995 mpaka 2015?

Nawaambia hamtakaa mfanikiwe wanamtandao hii game mshapoteza

Mpaka mawe yataongea mpaka siku mtakapofurushwa .

Anguko lenu laja na halipo mbali.
 
Haijaisha mpaka iishe.cha kufurahisha watanzania sasa hivi wana chuki kubwa na serikali yao na hawaiogopi so ni mda wowote saa yoye tegemea watu kuwaona barabarani na hiyo siku ikifika hakuna wakuwazuia cause askari watakuwa hawajajindaa kukabiliana na wandamanaji
 
Sasa wamegeuka kuwa wafa maji! Ni mwendo wa kutapatapa tu. Hata hawaelewi wambebeshe nani gunia zito la anguko lao!
 
Endelea kuota ndg kwenye kitanda chako Cha teremka tukaze hiko. Ukija kuamka wenzako wanaingiza magunia ya mahindi ndani ya nyumba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…