Moyo wangu wakupenda peke yako!!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Moyo wangu wakupenda peke yako!!!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by NasDaz, Jul 1, 2009.

 1. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #1
  Jul 1, 2009
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  Wala sina hakika kama nipo sahii, lakini nahisi MAPENZI NA SIASA ni dugu ya nasaba moja!! Kote ni FULL UWONGO, UASI, USALITI, UZANDIKI NA UNAFIKI PIA!!Hata hivyo, ajabu ni kwamba, a well structured uovu huu ndio unaojenga MAPENZI NA SIASA!! Hebu fikiria, mpenzio anakuambia anakupenda kuliko kitu chochote na kwamba MOYO WAKE HAUNA NAFASI KWA MTU MWINGINE BALI NI WEWE PEKE YAKO!!!! Ataendelea kusema eti BILA WEWE NI HERI KUFA, na kwamba mkiachana kwa namna yeyote ile BASI ATAISHI BILA MPENZI MAISHA YAKE YOTE!!! Je, inawezekana jambo hilo?! Ni kweli moyo umeumbwa hivyo? Hebu chukua mfano huu: Mwanamke na mwanume wanapokutana kwa tendo la ndoa halafu Mbegu za Mwanaume zikakutana na yai la mwanamke na kutungisha mimba, basi ndani ya muda mfupi mfuko wa uzazi unafunga na hakuna mbegu nyingine ya kiume itakayoingia tena!! Je, moyo nao upo hivi? Kwamba pendo la fulani likishaingia moyoni mwako basi moyo hufunga na kutoruhusu upendo/penzi kwa mwingine?! Na kama moyo upo hivyo, mbona unampenda baba yako na mama yako na kinachotofautina ni kiasi tu cha upendo!!! Sasa kwanini kwenye mapenzi tudanganyane kwamba upo peke yako?
  Kwa kifupi, labda niseme kwa mtizamo wangu, kauli sawa na hiyo ni unafiki na uwongo katika mapenzi. Hata kama mpenzi wako unampenda vipi, ni matumaini yangu ipo room kwa ajili ya mwingine somewhere else. Unakuta mtu anamtumia msg za mapenzi mpenzi wake huku akijifanya ni mtu mwingine kwa ajili ya kumtega ajue kama kweli anampenda!!! Hii ni kuchanganya MAPENZI NA UAMINIFU!!! Hivi ni vitu viwili tofauti. KAMA UNAAMINI KWAMBA AKUPENDAE KWA DHATI HAWEZI KUKUSALITI, basi wewe kalagha bao!! Anaweza kukupenda kwa moyo wote, lakini bado moyo wake unaacha room ya kupenda mwingine zaidi hata kama si kwa kiwango akupendacho wewe!!! Na kweli inapatikana hii room, ndipo usaliti unapotokea!! Ninachosema ni kwamba, mpenzio asikudanganye kwamba atakupenda wewe peke yako maisha yote hata baada ya kufa!!!! Akikuambia hivyo, mtemee mate usoni!! Mpenzi huyo ni mwongo sawa na mwanasiasa anayeahidi kujenga mabomba yatakayotoa maziwa bongo!! Mpenzi mkweli ni yule atakayekuambia kwamba bado moyo wake una nafasi ya kupenda mwingine na wengine zaidi lakini atahakikisha HAKUSALITI! MOYO, NI FREE ENTRY FREE EXIT ZONE!!!

  NAJENGA HOJA!!
   
 2. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #2
  Jul 1, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,644
  Likes Received: 1,470
  Trophy Points: 280
  Hiyo hoja yako mkuu ina hoja nyingi sana ndani yake!

  common narratives zinatuelekeza kuwa huwezi kumemwambia mwenzio eti 'hauko peke yako'! sijawahi kusikia hicho kitu, na lau kama tungeruhusiwa kusema hivyo, ni nani angekuwa kwenye mahusiano?

  Ideally, huwezi kumpenda mtu zaidi ya mmoja kwa wakati huo huo...kama unashindwa kuwa mwaminifu hizo ni tamaa na sio mapenzi, plus upendo haugawanyiki, hauhusudu, hauna kiburi, hau......
   
 3. The Farmer

  The Farmer JF-Expert Member

  #3
  Jul 1, 2009
  Joined: Jan 7, 2009
  Messages: 1,581
  Likes Received: 433
  Trophy Points: 180
  Kwani wewe hufahamu kuwa mapenzi ya Baba na Mtoo ni tofauti na Mapenzi ya Mume na Mke??
   
 4. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #4
  Jul 1, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Hapo kidogo pananipa shida.

  Nina mke,watoto, mama, baba,dada na kaka. Wote hawa najihisi kuwapenda kwa nafasi zao! Naweza kujitolea mmojawapo ya figo zangu kwa ajili ya yeyote kati ya hao niliowataja ili kuokoa maisha yao. Kwangu mimi kutoa ni kipimo muhimu cha mapenzi.

  Kwa nini unadhani mtu hawezi kupenda zaidi ya mtu mmoja?
   
 5. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #5
  Jul 1, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Tofauti yake ni nini?
   
 6. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #6
  Jul 1, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,644
  Likes Received: 1,470
  Trophy Points: 280
  Mkuu SMU hapa kinachoongelewa sio ile "agape love" bali ni kupenda kwa mwanamke/mwanaume...nadhani hapo ndo ilipo tofauti!
   
 7. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #7
  Jul 1, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  No, kupenda ni kupenda hakuna tofauti. Mahusiano ndio yanaweza kuwa tofauti.
   
 8. The Farmer

  The Farmer JF-Expert Member

  #8
  Jul 1, 2009
  Joined: Jan 7, 2009
  Messages: 1,581
  Likes Received: 433
  Trophy Points: 180
  Kuna tofauti kubwa sana, Mapenzi ya mke na mume yanatokana urafiki wao. Lakini mapenzi ya baba na mtoto au mama na mtoto yanatokana na udugu wao.
   
 9. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #9
  Jul 1, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Mahusiano! Refer to my post above(#7).
   
 10. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #10
  Jul 1, 2009
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  Then jaribu kunishawishi, ukishapenda moyo wako unafunga na kutoa "no more room" sawa na mfuko wa uzazi? Wakati unajibu hili usisahau hofu yangu ya unasaba wa siasa na mapenzi!!!
   
 11. M

  Msindima JF-Expert Member

  #11
  Jul 1, 2009
  Joined: Mar 30, 2009
  Messages: 1,018
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  NASDAZ elewa hili Moyo ni mdanganyifu.

  Na upendo wa dhati hauko katika maneno uko katika vitendo,naweza kwambia kuwa nakupenda ni wewe tu kumbe moyoni mwangu wala sina hata mpango na wewe,na pia naweza nisikwambie kuwa nakupenda lakini vitendo vyangu vikaeleza upendo wangu.
   
 12. GP

  GP JF-Expert Member

  #12
  Jul 1, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  mada inaongelea upendo wa MKE na MUME only, so kuna tofauti kubwa kati ya hao watu
   
 13. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #13
  Jul 1, 2009
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Mtoa mada, ujue kwamba kuna upendo wa aina nyingi. Wataalamu wanatofautisha kati ya upendo wa eros, philia, na agape. Mtu ni yuleyule na moyo ni uleule lakini jinsi ya kupenda makundi mbalimbali ya watu kunatofautina kama wengine walivoeleza hapo juu. Lakini upendo wa kindoa ni exclusive love, hauruhusu mtu mwingine kumpenda upendo wa kindoa baada ya watu wawili kufungana kwa upendo. Upendo huu hauruhusu mtu wa tatu au wa nne, nk. Ndo maana anasema ni wewe tu. Lakini watu walewale wanaruhusiwa kuwapenda watu wengine kwa upendo mwingine toafuti na ule wa kindoa. Huu ni upendo halali kabisa kwa nafasi yake
   
  Last edited: Jul 1, 2009
 14. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #14
  Jul 1, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,644
  Likes Received: 1,470
  Trophy Points: 280
  Mkuu SMU nadhani hapo utakuwa umeridhika na context ya tunachoongelea hapa!
   
 15. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #15
  Jul 1, 2009
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,918
  Likes Received: 2,068
  Trophy Points: 280
  Kaizer, mwanzo kabisa issue yangu ilikuwa hapo. Na nilisema hii inanipashida kuikubali. Kama kwa mfano mtu hawezi kupenda wake wawili, anawezaje kupenda watoto wawili? Kupenda ni nini?

  Kwa maana ya kutotoka nje ya mada, nadhani inatosha tukiishia hapo.
   
 16. fiksiman

  fiksiman JF-Expert Member

  #16
  Jul 1, 2009
  Joined: May 17, 2008
  Messages: 402
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Mapenzi hutokea kwa mtu mmoja tu, na hayo mengine ni matokeo ya utamaduni wetu hasa sisi waafrika....unajua zamani wazee wetu walikuwa wanadonoa sana, utakuta kibabu kinawanawake mtaa mzima ni familia yake. Sasa kile kitendo kimezaa utamaduni wa kupenda wanawake wengi si kwa mapenzi bali kwa kazi moja tu ya kudonoa tu.

  Kitu kingine nikusaidie, unajua sisi wanaume wa kiafrika tuna sifa moja kubwa, tuwe barani afrika, ulaya, amerika ama popote sifa hii haiwezi kukwepeka....TUNATAMANI KABLA YA KUPENDA. Hutaki sikulazimishi. Hii ni tofauti kidogo na wanawake, wao wakishapenda basi ni ngumu kumpa mwingine nafasi japo wapo ambao wanaongozwa na mapenzi yao binafsi ya tendo la ngono...na usiombe ukikutana na watu wa aina hiyo. Sasa jambo la msingi hapa ni kuvumiliana tu, mambo ya kufuatiliana yapunguzwe kwenye mahusiano ndo tunaweza kuwa na amani. TUACHE WIVU JAMANI LOOH!
   
 17. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #17
  Jul 1, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Jamani post hii ni nzuri sana lakini selection ya rangi ni poor, wengine macho yetu sio kivile. Nashauri tutumie black colour au kama vipi basi blue au nyingine isiyoumiza macho. Tuwajali na wengine, JF ni kwa watu wa rika zote
   
 18. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #18
  Jul 1, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,644
  Likes Received: 1,470
  Trophy Points: 280
  Sawa sawa mkuu, nadhani hilo linahitaji mjadala unaojitegemea kabisa
   
 19. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #19
  Jul 2, 2009
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  Theoretically u are right, lakini nawe utake usitake moyo haujaumbwa hivyo!!! Hata ukipenda mahali, usidanganyike kwamba hutapenda tena sehemu nyingine!!! Binafsi mpenzi wangu asinidanganye kwamba hawezi mpenda mwingine, this's not true. Nitamkubalia endapo ataniambia hawezi kunisaliti (Ingawaje practically sasa isha-prove failure) lakini sio kwamba hawezi penda mwingie!!!
   
Loading...