barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,866
MOYO WA NGURUWE KUANZA KUTUMIWA KUOKOA MAISHA YA BINADAMU
MAJARIBIO YA KUPANDIKIZA MOYO WA NGURUWE KWA NYANI YAMEFAULU
Wanasayansi wanasema kuwa wameuweka moyo wa nguruwe katika nyani kwa zaidi ya miaka miwili. Wanasayansi wanasema kuwa, muda si mrefu wataanza kutumia Moyo wa Nguruwe kuokoa maisha ya binadamu ambao wanahitaji moyo ili kuishi.
Matokeo yake yanaweza kupiga jeki matumaini ya upandikizaji wa viungo vya wanyama katika binaadamu huku kukiwa kuna upungufu wa binadamu wanaotoa viungo vyao.
Upandikazi wa viumbe tofauti husababisha mmenyuko wa kinga na kusababisha kukataliwa kwa kiungo hicho na mwili unaofanyiwa upasuaji huo.
Lakini wanasayansi kutoka Marekani na Ujerumani walitumia muundo wa jeni pamoja na dawa zinazopunguza kinga.
Kazi yao imeelezea katika jarida la mawasiliano ya kiasilia.
Ni muhimu kwa sababu inaleta uwezekano wa kutumia viungo hivyo kwa binaadamu,kulingana na mwandishi mwenza Muhammad Mohiuddin,kutoka kwa taasisi ya kitaifa ya Moyo ,Pafu na Damu huko Maryland,alikiambia chombo cha habari cha AFP.
Upandikizaji wa kutumia viumbe tofauti unaweza kuokoa maisha ya wengi kila mwaka ambayo hupotezwa kutokana na ukosefu wa viungo vya binaadamu kwa upandikizaji.
Pigs with human hearts, and other wild tales from the future of organ donation
Pig Heart Transplants For Humans Are On The Way