Majs
JF-Expert Member
- Dec 21, 2012
- 232
- 497
Baada ya mwanamziki Ben Pol kuchangia na kuhamasisha uchangishaji wa fedha kwa ajiri ya upasuaji wa Moyo kwa watoto 100 kupitia kampeni ya [HASHTAG]#rudishatabasamu100moyo[/HASHTAG] Uongozi wa Taasisi ya Moyo ya Dr. Jakaya Kikwete uliwaalika leo yeye na Lameck Ditto kuwapa elimu zaidi juu ya namna wanavyofanya kazi.
Pia wamepata nafasi ya kuwaona baadhi ya watoto, na wamepewa Watoto wawili ambao watawafuatilia kwa ukaribu zaidi ili kujua maendeleo yao zaidi. Wamewashukuru Uongozi wa Taasisi pamoja na timu nzima ya Wafanyakazi kwa ukarimu na elimu waliyowapatia.