Moto wateketeza Kiwanda cha Nguo cha 21st Century cha Morogoro asubuhi

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,701
71,034
Moto unateketeza Kiwanda cha Nguo cha 21st Century cha Morogoro asubuhi hii, chanzo na hasara hivijajulikana.

Kiwanda hiki kipo kinajulikana kwa jina lingine la polister, kipo eneo la Kihonda Viwandani.

⁠⁠⁠Kiwanda hicho ni moja ya viwanda vichache vinavyofanya kazi ambapo kwa sasa kilikua kinatengeneza khanga na vitenge vilivyoanzishwa na baba wa taifa Mwalimu Julias nyerere kimeungua moto asubuhi ya leo.

WhatsApp-Image-20160719(1).jpeg


WhatsApp-Image-20160719(2).jpeg


WhatsApp-Image-20160719.jpeg


WhatsApp-Image-20160719(3).jpeg
 
Mmiliki wa sasa ni nani? ...hawa 'wawekezaji' siwaamini kabisa. Isije kuwa kama zile hotel za Bagamoyo hapo kitambo!
 
Mtambue sasa kuwa hii ni nchi ya madini, mafuta gas. TUMEPEWA BURE kwavyo tutapata maziwa na asali.

Habari ya viwanda ndio matanuru yenyewe hayo ya jehanamu.
 
Mmiliki wa sasa ni nani? ...hawa 'wawekezaji' siwaamini kabisa. Isije kuwa kama zile hotel za Bagamoyo hapo kitambo!
It is very true.

Kuna 'harufu' ya mchezo mchafu hapo.....

Tukumbuke kuwa wengi waliouziwa viwanda hivyo vya Umma, wana asili ya Bara Asia na viwanda hivyo badala ya kuviendeleza kwa kutengeneza nguo wao wakavigeuza maghala ya kutunzia vitu vyao!

Inawezekana moto huo Ukawa kama 'sabotage' kwa kuwa wale ambao walikuwa hawajivendeleza viwanda hivyo wishaambiwa wavirejeshe serikalini...
 
Back
Top Bottom