Omuregi Wasu
JF-Expert Member
- May 21, 2009
- 749
- 148
Duhh! Sokomoko umenifurahisha kweli.... kwamba Chadema kinashutumiwa kuongozwa na watu wa ukoo umoja na udini sasa CCM kukoje?Mimi ninawasiwasi Chadema wanahusika na hiyo msg sidhani kama CCM wanaweza kufanya hivyo kwakuwa CCM ni chama kikongwe na wamekomaa kwenye siasa. Sisemi kama hawana mbinu za kisiasa lakini sio za namna hiyo.
Chadema ni chama kinachopigiwa kelele kwa maswala ya udini na ukoo ( watu wa familia moja kuongoza chama na kupeana ubunge wa viti maanlum ) pengine wameamua kutumia hii mbinu ili watu wahamishe mawazo yao kuwa chama hiki kina harufu ya udini.
Haya ni mawazo yangu binafsi maana sote tumeumbwa na akili zetu na sitegemei kwakuwa sipo na baadhi ya watu kwenye hili mkanichukia.\
Ahsanteni sana kwa kunisikiliza.
Kikwete ni mwenyekiti, Salma ni mjumbe, Ridhiwan ni mjumbe, Mtoto wa miaka 10 ni mwenyekiti.... hii ni familia ya Kikwete in usultani siyo ukoo ndani ya CCM. Udini tuna Kikwete, Makamba, Kinana, Karume, Shein hao ni dini gani hivi??
Acha kuchafua hali ya hewa ..... sema maneno hayo kwa wajinga siyo kwa watanzania wenye elimu ya kati na ya juu kama watu wa JF.