Moto wa Majaliwa kuhamia Geita

Moto wa Majaliwa kuhamia Geita

diana chumbikino

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2018
Posts
428
Reaction score
368
1569061301351.png

Baada ya kumaliza ziara ya siku tano mkoani Morogoro na kuwasimamisha kazi watendaji zaidi ya 10 wa Serikali, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Jumamosi Septemba 21, 2019 ameanza ziara ya siku mbili mkoani Geita Mtendaji mkuu huyo wa Serikali atatembelea wilaya ya Chato na Geita.

Akiwa wilayani Chato atatembelea kiwanda cha pamba, kufanya ukaguzi na kuzungumza na wakulima na wanunuzi. Katika wilaya ya Geita, Majaliwa atatembelea kata ya Chikobe jimbo la Busanda kisha, jimbo la Geita Vijijini kukagua ujenzi wa Hospitali ya wilaya hiyo inayojengwa kata ya Nzera.

Pia, atatembelea jimbo la Geita Mjini kata ya Kasamwa na kukagua kiwanda cha pamba kilichopo eneo la Kanyala mjini Geita Kesho katika siku ya pili ya ziara yake, Majaliwa atazindua maonyesho ya teknolojia ya madini yaliyowawahusisha washiriki zaidi ya 260 yenye kauli mbiu, ‘madini ni chachu ya ukuaji wa uchumi wa viwanda tuwekeze kwenye teknolojia bora ya uzalishaji na tuyatumie masoko ya madini’.
 
Jamaa wanakazana na wenzao wanakazana hivyo hivyo

Kimahesabu unaweza ukafanya hivi;
Let
Kutengua = x
Kuteua = y

Sasa kama unatafuta equliblium point, means
x = y

Sasa ukitia constant term upande wa kushoto
x = Ky

Ukiiweka K kama baba yao
K = x / y

Ukiipa kwenye proportional ndio tunapoteza
~ K = ~ x / y

Maana yake, kutabakia vile vile hata kama teua tongue zitaendelea. Maana yake jamii ni ile ile
Sasa hapo lazima utafute 'exogenic factor' zinazoathiri huyo equation
Hapo ndio unawakuta wanyama sasa, wasaliti, wazandiki, wala rushwa, waramba miguu ili wapatie vyeo uwezo hawana, waganga na wachawi wanaotishia wenye uwezo wasigombee, vyuma kukaza na utashi wa kisiasa kuona wengine hawafai
 
Nawapa hongera waliokuelewa.
 
nadhani kule nyanhwale watu wanajambiana tu.

bora magufuli atakutukana tyu hadharani, na ukawa mpole lakini akikuuliza msifie tu na mamiradi kibao atakuacha kuliko Maja. Maja hacheki na nyani yaani ukijaa "anamshauri kwa hekima" jpm kisha beteri inachomokewa.

piga kazi majaliwa
 
..ziara za viongozi wakuu kutembelea mikoa na wilaya mbalimbali mbona hazina uwiano?

..mbona kama kuna maeneo yanatengwa ktk kutembelewa na viongozi wakuu ukizingatia idadi ya ziara hizo?
 
Engineer yuko smart mnooo....hana skendal trust me ataondoka na kusifia....
 
Back
Top Bottom