Moto wa Chadema wawatesa ' vigogo' CCM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Moto wa Chadema wawatesa ' vigogo' CCM

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by hans79, Jun 10, 2012.

 1. h

  hans79 JF-Expert Member

  #1
  Jun 10, 2012
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  10th June 2012

  Wimbi la `wanaojivua gamba` wavaa magwanda:
  Moto wa siasa uliowashwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwenye mikoa ya Mtwara na Lindi, umedhihirika kuwatesa ‘vigogo’ wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), hususan wabunge wa majimbo yaliyopo katika mikoa hiyo.
  Chadema ilianza ziara ya Operesheni Okoa Kusini tangu Mei 27, mwaka huu kwa kuanzia mkoani Mtwara, ambapo viongozi, wabunge na makada wa chama hicho wamekuwa wakisambaa kata za majimbo yote kwa wakati mmoja.
  “Mtindo huu tunaoutumia kujigawa kwenye kata, tunakuwa mfano wa jeshi linaloshambulia ili kupata ushindi….na ushindi huo tunauona,” anasema Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbrod Slaa.
  Wanapokuwa kwenye kata, viongozi, wabunge na makada wa Chadema wanafika ngazi za vijiji ambapo wanahutubia mkutano, wanafungua matawi na kusimamia uchaguzi wa viongozi wa muda hususan kwenye maeneo ambayo hawakuwepo.
  Dk Slaa anasema Chadema ilifika kwenye mikoa hiyo mwaka 2004, ambapo ilipanda mbegu ya mageuzi, lakini baadaye ikakiachia Chama Cha Wananchi (CUF) kiendeleze kazi ya kuleta mabadiliko kwa vile kilijiridhisha kuwa na ngome yake.
  “Tulikubaliana tusije huku kusini mwa nchi kwa sababu wenzetu wa CUF walisema wana ngome, na ilikuwa kweli, kwa maana wakati huo CUF walikuwa na nguvu kubwa sana,” anasema Dk Slaa.
  Lakini Dk Slaa anasema baada ya CUF kuingia katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar, viongozi na wabunge wake wameonyesha dalili za kutokuwa wapinzani wenye lengo la kuiondoa CCM madarakani, hivyo Chadema imerejea kuendeleza vuguvugu la mabadiliko (M4C) kwa maslahi ya umma.
  Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, anasema kuwemo kwa CUF katika serikali ya visiwani Zanzibar, kunakifanya chama hicho kisijulikane kama ni cha upinzani ama kinatawala.
  “Tujiulize, hivi leo hii Katibu Mkuu wa CUF ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, anaweza kuinyooshea kidole serikali ya CCM ambayo mimi ni mmoja wa watendaji wake,” anahoji Mbowe.
  Hata hivyo, katika hali inayoweza kutafsiriwa kuwa ni kuchochea chuki ya wananchi dhidi ya watawala, Mbowe na Slaa wamekuwa wakisisitiza kwenye mikutano yao, kuwa Chadema haina matatizo na viongozi, wanachama na wafuasi wa CUF kwenye ngazi za wilaya, kata na vijijini.
  Badala yake wanasisitiza kuwa kasoro wanazozikemea zipo kwa viongozi wa kitaifa, walioingia katika ushirikiano na watawala pasipo ridhaa ya wananchi wao.
  Kauli hizo zimekuwa kivutio kwa wanachama na wafuasi wa CUF walio wengi, kupata ujasiri wa kukihama na kujiunga Chadema.
  Dalili zinaonekana zaidi, ikiwemo kwa viongozi wa Chadema wanapofika kwenye ngome za CUF na CCM, hawapati mapokezi mazuri ingawa idadi ya watu inakuwa kubwa.
  Lakini wanapohutubia, wananchi huwashangiliana na kuwapongeza, kisha (mkutano unapomalizika) hujipanga kwenye mistari mirefu wakinunua kadi za uanachama.
  KUUNDA UONGOZI WA MATAWI
  Chadema kupitia na Mbowe na Dk Slaa, inathibitisha kwamba haikuwepo katika mikoa hiyo, na kwamba hivi sasa kinachofanyika ni kuhamasisha watu wajiunge, kisha kupata uongozi wa muda.
  Hivyo kila wanapomaliza kuhutubia mikutano ya hadhara na kuanza kutoa kadi za uanachama, viongozi, wabunge na makada wa Chadema husimamia kufanyika kwa uchaguzi wa viongozi wa muda kwenye ngazi ya tawi na kata.
  Kisha viongozi wawili kutoka kila kata, wanasafirishwa hadi Makao Makuu ya wilaya husika ambapo wanapewa semina fupi itakayowawezesha kuendeleza vuguvugu la M4C kwenye maeneo yao, kabla ya kufanyika kwa uchaguzi rasmi baadaye mwaka huu.
  Tayari Chadema kwa kutambua umuhimu wa kukiweka chama katika ngazi ya msingi (ubalozi), kimetumia ibara ya 7.1.1 ya Katiba yake kimeweka tarehe ya kufanyika uchaguzi nchi nzima.
  Mbali na ngazi ya ubalozi, Chadema imetumia ibara ya 7.1.3 kutangaza uchaguzi wa chama hicho ngazi ya tawi, ambapo awali kilionekana kutokuwepo katika maeneo mengi ya nchi.
  Maelezo yaliyochapishwa na Chadema yanaonyesha kuwa Septemba Mosi hadi Oktoba 5, mwaka huu kuwa siku za uchaguzi ngazi za msingi wakati ule wa matawi utafanyika kati ya Desemba 5 hadi Januari 8, mwaka ujao.
  Chaguzi nyingine na ngazi zake kwenye mabano zitafanyika Februari 8 hadi Machi 14, mwaka ujao (kata), Aprili 14 hadi Mei 23, mwaka ujao (jimbo), Juni 23 hadi Julai Mosi, 2013 (wilaya) na Agosti 2 hadi Septemba 11, mwakani (mkoa).
  Chaguzi zote hizo zitafanyika zikihusisha pia mabaraza tofauti ya Chadema, lile la vijana (Bavicha), wanawake(Bawacha) na Wazee.

  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

  Kwa mbinu hizo M4C ipo juu, wazee wa mipacho wanahaha.

  Nawasilisha.
   
 2. K

  Kassim Awadh JF-Expert Member

  #2
  Jun 10, 2012
  Joined: Mar 12, 2012
  Messages: 887
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  sijapata picha kamili ya unachotaka kuainisha,but the good part ni kwamba unazungumzia changes,,mabadiliko,,kuanguka kwa ccm
   
 3. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #3
  Jun 10, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,004
  Likes Received: 325
  Trophy Points: 180
  Safi sana hapo hakuna kulala mpaka kieleweke kazi kwa kwenda mbele, Jana kwenye mkutano wa ccm Chadema Square baada ya blabla eti watu wacheze muziki ha haa.
   
 4. a

  andrews JF-Expert Member

  #4
  Jun 10, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 1,680
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  CCM HAWAACHI KUOTA MCHANA KWEUPE,KATIKA KAMPENI ZAO ZA KUWAPUUZA WATANZANIA WAMEANDAA ULAGHAI MWINGINE ILI WAPATE KURA ZA WAPUMBAVU.
  1.KUANZISHWA BENKI YA WAKULIMA
  2.KUANZISHA BENKI YA VIJANA
  KATIKA UANZISHWAJI BENKI HIZO SERIKALI INA MPANGO WA KUWAHADAA WATZ KWA KUWAAMBIA WATAWAKOPESHA MIKOPO YENYE RIBA NAFUU,KUANZIA MILLION 1MPAKA 15.LAKINI KATIKA UOMBAJI HUO UNAHUSISHA WAJUMBE WA NYUMBA KUMI KAMA MAWAKALA WAO ILI UPATE MKOPO,CHA KUCHEKESHA ZAIDI INAAMINIKA CCM IMEJIPANGA KUTUMIA KITAMBULISHO CHA URAIA NA HASA CHA KUPIGIA KURA KAMA MTAJI WA KUWAPATA HAO WALENGWA.NA KUHAKIKISHA WANAOCHUKUA MIKOPO WOTE WATAIPIGIA CCM UCHAGUZI KUANZIA UDIWANI WA 2014 NA UCHAGUZI MKUU 2015.LAKINI WAJUMBE WENGI WANA WASIWASI KUWA VIJANA WALIO WENGI WAMEELEVUKA SANA NA WATAKULA PESA ZAO NA KUWAPIGIA WAPINZANI.CCM ILITUMIA MKUTANO WA JANGWANI KAMA KIPIMA JOTO SASA WAMEANZA KUINGIWA NA WASIWASI MAANA MKUSANYIKO ULE HAUKUKAMILIKA BILA YA PESA SASA WANAJIULIZA BILA VIKINDI VYA SANAA KWELI WATAKUBALIKA,MJUMBE ALIYE KARIBU NA NAPE KASEMA CHADEMA INAWANYIMA USINGIZI KULIKO HATA MAGONJWA YA WAZAZI WAO AU WANANDOA WAO.
  BINTI MREMBO LUMUMBA CCM
  :confused2:
   
 5. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #5
  Jun 10, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Wakubwa!...Huwa najivunia kuwa mwanachadema...hakika haya ndio maamuzi sahihi kwa wakati sahihi,wewe je?......
   
 6. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #6
  Jun 10, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,838
  Trophy Points: 280
  nlishasema mwaka huu kuna vigogo wengi sana wa ccm watakufa na STROKE hasa yule jamaa wa mausingizi wa pale bunda aliyezomewa juzi juzi
   
 7. h

  hans79 JF-Expert Member

  #7
  Jun 10, 2012
  Joined: May 4, 2011
  Messages: 3,802
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 145
  Watatughalimu wakifa na stroke bora wafe bila kuumwa, sababu wwataka matibabu nje ya nchi hata kama wataumwa jino.
   
 8. m

  matawi JF-Expert Member

  #8
  Jun 10, 2012
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Unamsema jamaa wa Bunda mwenye asili ya Gombe? Yule aliyesema walioihama ccm arusha ni watu watatu tu akiwemo James Milya?
   
 9. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #9
  Jun 10, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,838
  Trophy Points: 280
  yes huyo huyo..you are so intelligent
   
 10. B

  Bob G JF Bronze Member

  #10
  Jun 10, 2012
  Joined: Oct 5, 2011
  Messages: 2,354
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Mipango mizuri imepata watekelezaji makini M4C
   
Loading...