FikraPevu
JF-Expert Member
- Jan 2, 2010
- 304
- 236
Utafiti wa taasisi ya Twaweza unaeleza serikali inapoteza bilioni 793 kila mwaka za mishahara ya walimu wa shule za msingi ambao hawatimizi majukumu yao ya kufundisha wanafunzi na kuhudhuria shuleni.
Akitoa matokeo ya utafiti huo uliobeba dhima ya ‘Kuwalipa walimu bahshishi kwa matokeo ya kujifunza’, Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya Twaweza, Aidan Eyakuze amesema katika uchunguzi walioufanya katika wilaya 10 za Tanzania wamebaini kuwa serikali inapoteza kiasi kikubwa cha fedha kutokana na baadhi ya walimu kutowajibika ipasavyo katika ufundishaji.
“ Tunapoteza kila mwaka bilioni 793 ya mishahara ya walimu ambao hawaingia shule au darasani. Ukilinganisha kiasi hiki na shilingi bilioni 306 zilizopotea mwaka 2014 katika kashfa ya IPTL Escrow na kuzua mtafuruku mkubwa nchini, upotevu wa fedha kupitia mishahara ya walimu wa shule za msingi ni mara mbili ya hasara iliyotokana na kashfa hiyo ya Escrow. Na kiasi hiki hupotea kila mwaka”, amesema Eyakuze.
Amesema mazingira yasiyoridhisha ya kujifunzia na kufundishia katika shule za msingi, yamekuwa kikwazo kwa walimu kuhudhuria shuleni . Hali hiyo inatajwa kuathiri wanafunzi kuelimika na kupata stadi muhimu za maisha.
“Mahudhurio ya walimu darasani ni changamoto nyingine . Mwaka 2015 asilimia 31 sawa na Mwalimu 1 kati 3 hayuko shuleni lakini imepungua kidogo hadi asimilia 27 mwaka 2016. Hapo tena mwaka 2016 mwalimu 1 kati ya watatu yuko shuleni lakini hayupo darasani anafanya mambo mengine ya kiutendaji halafu asilimia 41 wako darasani”, amesema Eyakuze.
Imebainishwa kuwa walimu wakipewa motisha ya fedha au ujuzi, mahudhurio yao shuleni yawaweza kuongezeka na kuwafaidisha wanafunzi kwa kupata matokeo mazuri katika masomo yao.
Zaidi, soma hapa => Serikali inapoteza bilioni 793 za walimu ‘watoro’ | FikraPevu