Motel Agip Dar Inaoza!

Posta hakuna starehe tena, sasa ni Tabata, Sinza kidogo na buza au Masaki.
 
Posta hakuna starehe tena, sasa ni Tabata, Sinza kidogo na buza au Masaki.
Niliona mkuu, nilikuja 2024, jiji limekufa kifo cha mende halafu wabongo ukute wanajitanua kujilinganisha na Nairobi wakati jiji linaonekana kijiji kwa Nairobi. Kwa mfano mtu atoke mamtoni aje Dar kutembea sidhani kama atarudi tena, maana ataona jiji limepoa pale kati hamna kitu ni wahindi tu. Ukisikia Paris, London na New York ni majiji ya wasiolala hawaongelei vitongojini wanaongelea pale kati hamna kitu kinafungwa watu wapo macho 24/7 pako moto. Na hii ndio inaleta foleni, maana ikifika saa 11 watu wote wanaenda vitongojini wakati majiji mengine ndio muda wa kwenda downtown kwenye biashara. Sijui ni nani kaua jiji langu pendwa Daslamaa.😎😎😎
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…