Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 16,954
- 26,048
Usiku ni danguroView attachment 3630096
Motel Agip iliyopo Posta jijini Dar es Salaam ilifungwa rasmi tarehe 18 Desemba 1998 kutokana na mgogoro mkubwa wa kimkataba wa upangaji na ukodishaji kati ya uongozi wa hoteli hiyo na mmiliki wa jengo, kampuni ya mafuta ya Agip Tanzania Limited. Hoteli hiyo yenye vyumba 57 ilikuwa kitovu kikuu cha burudani na diplomasia nchini.
Mpaka leo , 16-7-2026 Hotel imekuwa gofu, wanalala mateja na vibaka Posta, haizalishi na imekuwa uchafu katikati ya Jiji.
Kuanzishwa kwa Motel Agip:-
- Mwaka wa Ufunguzi: Hoteli ilikamilika na kuanza huduma rasmi mwaka 1964.
- Waasisi: Ilijengwa na kampuni ya mafuta ya Kiitaliano ya Agip (Azienda Generale Italiana Petroli)kupitia shirika mama la ENI.
- Lengo la Mradi: Ilikuwa sehemu ya mpango mkakati wa Italia uliorubuniwa kama "disegno africano"kupanua soko la nishati na huduma barani Afrika.
- Upekee wake: Ilikuwa kielelezo cha usanifu wa kisasa wa Kiitaliano na ilijumuisha ukumbi wa mazoezi ghorofa ya sita ukiangalia Bahari ya Hindi.
- Umaarufu: Ilikuwa maskani ya wanadiplomasia, wafanyabiashara, na wasafiri. Pia ilitamba sana kutokana na Disco la Mawingu lililokuwa likiongozwa na Ma-DJ nguli kama DJ Bonny Love.
Kufungwa kwa Hoteli (1998)
- Sababu Kuu: Mgogoro wa mkataba wa kodi na upangaji uliokuja juu kati ya uongozi wa uendeshaji (chini ya Mkurugenzi Emmanuel Mantheakis) na wamiliki wa jengo (Agip Tanzania).
- Athari: Zaidi ya wafanyakazi 150 walipoteza kazi ghafla usiku wa tarehe 18 Desemba 1998.
- Uamuzi wa Wanahisa: Waendeshaji waliamua pia kuelekeza nguvu zao kwenye hoteli mpya ya Sheraton Dar es Salaam iliyofunguliwa mwaka 1995.
Kwanini Haifunguliwi Hadi Sasa?
Pamoja na kupita kwa miongo kadhaa, jengo hilo limeendelea kusimama bila kufanya kazi kwa sababu zifuatazo:
- Mivutano ya Umiliki na Wawekezaji: Mwaka 2011, kampuni ya Wellworth Group of Companiesilitangaza kununua hoteli hiyo pamoja na Embassy Hotel kwa lengo la kuzikarabati. Hata hivyo, miradi hiyo ilisuasua kutokana na urasimu wa kisheria na mabadiliko ya mipango ya uwekezaji.
- Migogoro ya Kisheria na Kifedha: Majengo mengi ya zamani ya Posta (ikiwemo Embassy iliyo jirani) yalikumbwa na kesi za madai ya wafanyakazi na migogoro ya umiliki wa hisa za serikali na sekta binafsi, hali iliyofanya mali hizo kubaki "frizoni" kisheria.
- Uchumi wa Matengenezo: Miundombinu ya jengo hilo imechakaa sana baada ya kukaa miaka mingi bila matengenezo. Wawekezaji wengi huona gharama ya kubomoa au kukarabati majengo ya kizamani katikati ya jiji kuwa kubwa mno ikilinganishwa na kujenga mapya.
Ma tycoon wanalitaka, pale mjini kati, parking kuliko New Africa, bonge la kumbi za sinema na mazoezi yaani linaozea pale, labda tunahitaji wakoloni waje kutupa akili nini cha kufanya.Vipi Tena, Kuna MTU analitaka Hilo jengo, maana sehemu Nzuri sana
Jiulizw kuna watu wanalala pale miaka zaidi ya 30 hawalipi kodi, wanaficha m,ali, hivi hata kama ingefunguliwa kulala iwe laki moja tu, ingejaa vyumba vyote na watalii wangejaa maana wanapenda majengo yenye historia.Usiku ni danguro
iko siku magenge watajimilikisha tu.....View attachment 3630096
Motel Agip iliyopo Posta jijini Dar es Salaam ilifungwa rasmi tarehe 18 Desemba 1998 kutokana na mgogoro mkubwa wa kimkataba wa upangaji na ukodishaji kati ya uongozi wa hoteli hiyo na mmiliki wa jengo, kampuni ya mafuta ya Agip Tanzania Limited. Hoteli hiyo yenye vyumba 57 ilikuwa kitovu kikuu cha burudani na diplomasia nchini.
Mpaka leo , 16-7-2026 Hotel imekuwa gofu, wanalala mateja na vibaka Posta, haizalishi na imekuwa uchafu katikati ya Jiji.
Kuanzishwa kwa Motel Agip:-
- Mwaka wa Ufunguzi: Hoteli ilikamilika na kuanza huduma rasmi mwaka 1964.
- Waasisi: Ilijengwa na kampuni ya mafuta ya Kiitaliano ya Agip (Azienda Generale Italiana Petroli)kupitia shirika mama la ENI.
- Lengo la Mradi: Ilikuwa sehemu ya mpango mkakati wa Italia uliorubuniwa kama "disegno africano"kupanua soko la nishati na huduma barani Afrika.
- Upekee wake: Ilikuwa kielelezo cha usanifu wa kisasa wa Kiitaliano na ilijumuisha ukumbi wa mazoezi ghorofa ya sita ukiangalia Bahari ya Hindi.
- Umaarufu: Ilikuwa maskani ya wanadiplomasia, wafanyabiashara, na wasafiri. Pia ilitamba sana kutokana na Disco la Mawingu lililokuwa likiongozwa na Ma-DJ nguli kama DJ Bonny Love.
Kufungwa kwa Hoteli (1998)
- Sababu Kuu: Mgogoro wa mkataba wa kodi na upangaji uliokuja juu kati ya uongozi wa uendeshaji (chini ya Mkurugenzi Emmanuel Mantheakis) na wamiliki wa jengo (Agip Tanzania).
- Athari: Zaidi ya wafanyakazi 150 walipoteza kazi ghafla usiku wa tarehe 18 Desemba 1998.
- Uamuzi wa Wanahisa: Waendeshaji waliamua pia kuelekeza nguvu zao kwenye hoteli mpya ya Sheraton Dar es Salaam iliyofunguliwa mwaka 1995.
Kwanini Haifunguliwi Hadi Sasa?
Pamoja na kupita kwa miongo kadhaa, jengo hilo limeendelea kusimama bila kufanya kazi kwa sababu zifuatazo:
- Mivutano ya Umiliki na Wawekezaji: Mwaka 2011, kampuni ya Wellworth Group of Companiesilitangaza kununua hoteli hiyo pamoja na Embassy Hotel kwa lengo la kuzikarabati. Hata hivyo, miradi hiyo ilisuasua kutokana na urasimu wa kisheria na mabadiliko ya mipango ya uwekezaji.
- Migogoro ya Kisheria na Kifedha: Majengo mengi ya zamani ya Posta (ikiwemo Embassy iliyo jirani) yalikumbwa na kesi za madai ya wafanyakazi na migogoro ya umiliki wa hisa za serikali na sekta binafsi, hali iliyofanya mali hizo kubaki "frizoni" kisheria.
- Uchumi wa Matengenezo: Miundombinu ya jengo hilo imechakaa sana baada ya kukaa miaka mingi bila matengenezo. Wawekezaji wengi huona gharama ya kubomoa au kukarabati majengo ya kizamani katikati ya jiji kuwa kubwa mno ikilinganishwa na kujenga mapya.
Kama Biafra?iko siku magenge watajimilikisha tu.....
Jangwani BRT station gang member mmoja kaweka bandari kavu tayarKama Biafra?
Magomeni Mviringo pale Kanisani wakapiga ka-garden ka geresha eneo lililobaki wamejipigia permanent Bar, Fremu za wamasai na Car Wash, ndio imeenda hiyo.Jangwani BRT station gang member mmoja kaweka bandari kavu tayar
Biafra ilianza taratibuuuuuuu imeishaaaa
Jiji halina sehem za wazi za watoto kucheza au watu kupumzika....jiji liko hovyooo
| Mkoa |
|---|
| Dar es Salaam |
| Pwani (Coast Region) |
Wee lile eneo la wazi hapo ubalozini limechukuliwa tayari ?😲Magomeni Mviringo pale Kanisani wakapiga ka-garden ka geresha eneo lililobaki wamejipigia permanent Bar, Fremu za wamasai na Car Wash, ndio imeenda hiyo.
Jngwani ile yard ndio kwaheri mwenywe atakuwa na hati anajichukulia mkopo hela za maskini wanaotunza benki wakiamini watapata riba.
vipi Oysterbay viwanja vya farasi na pale njia Panda kwenda ubalozi wa Marekani walipokuwa wanauza majiko ya mkaa na maua?
Pamehapigwa mabati, hutaona media wala blog inanyanyua mdomo, hata JF kwenye instagram haiwezi nyanyua mdomo.Wee lile eneo la wazi hapo ubalozini limechukuliwa tayari ?😲
Daa aisee, nilikuwa nakuja hapo kufanya mazoeziPashapigwa mabati, hutaona media wala blog inanyanyua mdomo, hata JF kwenye instagram haiwezi nyanyua mdomo.
Wasije wakajenga msikiti, maana watatusumbua kwa makelele yao .Pashapigwa mabati, hutaona media wala blog inanyanyua mdomo, hata JF kwenye instagram haiwezi nyanyua mdomo.
viwanja vya Farasi kwishaaaMagomeni Mviringo pale Kanisani wakapiga ka-garden ka geresha eneo lililobaki wamejipigia permanent Bar, Fremu za wamasai na Car Wash, ndio imeenda hiyo.
Jngwani ile yard ndio kwaheri mwenywe atakuwa na hati anajichukulia mkopo hela za maskini wanaotunza benki wakiamini watapata riba.
vipi Oysterbay viwanja vya farasi na pale njia Panda kwenda ubalozi wa Marekani walipokuwa wanauza majiko ya mkaa na maua?
WORLD CUP 2030 TUTAINGIA KUTOKEA WAPI, MAANA ndio hivyo?viwanja vya Farasi kwishaaa
Jangwan pale jamaa atavuta mikopo ya billions
central imebaki posta watu wanaenda kuishi jiran na msitu MabwepandeIliokua Embassy Hotel, vipi na yenyewe panaendeleaje?? Ila uwa nikikaa na kufikiria sana naona Jiji la Dar linarudi nyuma badala ya kwenda mbele. Miji yote duniani pale katikati ya jiji uwa ndio sehemu haswa ya starehe, mahoteli na ma restaurant ya nguvu, ma night clubs, mabebez usiku. Yaani watu wanatoka vitongojini wanaenda "central" kula bataz. Lakini Dar eti bataz zipo huko vitongojini ndio maana foleni haziishi. Zamani tulikua tunatoka vitongojini tunaenda ma movie Avalon, New Chox, Empress n.k na night clubs zilikua mjini. Usiku mji umechangamka, siku mjini wamebaki wahindi tu. Jiji linakufa hilo.