MOSSAD most efficient assassins, hitmen and killers walivyoitesa dola la Iran. Kaa nao mbali.

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
1813787414.jpg

Siku ya tarehe 23 July mwaka 2011 saa kumi na nusu jioni, watu wawili wakiwa na bunduki ambazo walizificha kwenye majaketi waliyovaa, walishuka kutoka kwenye pikipiki katika mitaa ya Bani Hasheem kusini mwa Tehran na kumimina risasi kwa mtu ambaye alikiwa amesimama mlangoni mbele ya nyumba yake akiwa anajiandaa kuingia ndani akitokea kazini. Mara moja baada ya kufanta shambulio hili walitokomea kusikojulika kabla ya polisi kuwasili.
Mlengwa wa shambulio hili ambaye aliuwawa alikuwa ni Darioush Razaei Najad, Profesa mwanafizikia mwenye miaka thelathini na tano ambaye alikuwa ni moja wa wahusika wakuu katika mradi wa siri wa nyuklia wa nchi ya Iran. Jukumu lake kuu katika mradi huu ilikuwa ni kutengeneza ‘switches’ ambazo zinawekwa kwenye vichwa vya mabomu ya nyuklia (nuclear warheads).

Razaei Najad hakuwa mwanasayansi wa kwanza wa Iran kuwa na mwisho wa kifo cha kikatili kama hiki.

Kwa taarifa rasmi za serikali, Iran walidai kuwa walikuwa wanarutubisha nuclear kwa matumizi ya amani tu kama vile kuzalisha umeme, na walidai kuwa kinu cha Bus Hehr, moja ya vyanzo vikuu vya umeme nchini humo ambacho kilijengwa kwa msaada wa nchi ya Urusi ilikuwa ni moja ya uthibitisho wa kuonyesha kuwa hawakuwa na nia mbaya ya kurutubisha nyuklia.

Lakini pamoja na kinu cha Bus Hehr kutumika kwa matumizi ya kawaida ya kuzalisha umeme, bado kulikuwa na vinu vingine vya siri ambavyo viligundulika ambavyo vilikuwa na ulinzi mkali na hakukuwa na uwezekano wa yeyote asiyehusika kuweza kuingia.

Baada ya muda, Iran iliwapasa kuanza kukubali juu ya uwepo wa vinu hivi vya siri japo waliendelea kukanusha kuwa walikuwa wanarutubisha nyuklia kwa lengo la kutengeneza silaha. Lakini mpaka kufikia muda huu Idara za Intelijensia za nchi za magharibi pamoja na majasusi waliopandikizwa ndani ya Iran walikuwa wameshagundua juu ya uwepo wa maprofesa nguli wa sayansi kwenye vyuo vikuu kadhaa nchini Iran ambao walikuwa wamechaguliwa na serikali ya Iran kwa ajili ya kutumika katika mradi wa kutengeneza bomu la kwanza la nyuklia la Iran.

Lakini kwa kadiri ambavyo Iran walikuwa wanapiga hatua kufikia lengo hili la kuwa na silaha za nyuklia ndivyo ambavyo pia kulionekana juhudi kutoka kwa “watu wasiojulikana” kukwamisha uwezekano wa Iran kumiliki silaha za nyuklia.

Tukirudi nyuma kidogo, siku ya tarehe 29, Novemba mwaka 2010 majira ya saa moja na dakika arobaini asubuhi, maeneo ya kaskazini mwa Tehran, pikipiki iliyopakia watu wawili waliovalia helmet iliibuka kutoka nyuma ya gari la Dr. Majid Shahriyari, mwanasayansi kiongozi wa mradi wa nyuklia wa serikali ya Iran. Pikipiki ilikoleza mwendo ili kuipita gari ya Dr. Majid Shahriyari na walipokuwa wanaipita gari, mmoja wa wale waliopo kwenye pikipiki aligandisha kifaa fulani kwenye kioo cha dirisha la gari upande wa dereva.
Sekunde chache baadae gari lililipuka na kumuua Dr. Majid Shahriyari na kumjeruhi vibaya mkewe.

Wakati huo huo mjini Atas, kusini mwa Tehran, waendesha pikipiki wasiojulikana walifanya kitu hicho hicho kwenye gari aina ya Peugeot 206 inayomilikiwa na Dr. Fereydoun Abas si-Davani na kumjeruhi vibaya yeye na mkewe.

Mara moja baada ya kutokea kwa milipuko hii, serikali ya Iran ilinyooshea kidole Mossad na kuwatuhumu kuendesha mauaji haya ya wanasayansi wake.

Hata baada ya vifo vyao wanasayansi hawa wawili, majukumu yao ambayo walikuwa wanayafanya kwenye miradi ya nyuklia ya Iran iliendelea kuwa ni siri kubwa. Lakini Ah Akbar, kiongozi wa mradi huu wa urutubishaji wa nyuklia alieleza kuwa wanasayansi hao waliouwawa ni mashujaa wa taifa na vifo vyao vimeacha pengo lisilozibika katika timu ya wanasayansi wanaohusika kwenye mradi huu.

Rais wa Iran wa kipindi hicho, Ahmadinejad kama ilivyo hulka yake alionyesha kukasirishwa na vitendo hivi vya mauaji kwa namna ya kipekee kabisa. Moja ya wale wanasayansi walioshambuliwa, Dr. Fereydoun Abas si-Davani ambaye yeye na mkewe walijeruhiwa vibaya lakini hawakufa, Rais Ahmadinejad alimfanya kuwa Makamu wa Rais.

Wale waendesha pikipiki waliotekeleza mauaji haya hawakuwai kujulikana kamwe.

Tukiruditena nyuma kidogo siku ya tarehe 12 January mwaka 2010 majira ya saa moja na dakika hamsini asubuhi, Profesa Masoud Al Mohammadi alikuwa anatoka nyumbani kwake maeneo ya Shariati mitaa ya Gheytarihe kaskazini mwa Tehran. Asubuhi hii alikuwa anaelekea kazini kwenye maabara ya chuo kikuu cha Sharif (Sharif University of Technology).
Alipojaribu kufungua mlango wa gari yake mlipuko mkubwa ulitokea na kuondoa ukimya uliotawala mitaa hii tulivu. Vyombo vya ulinzi licha ya kuwahi eneo la tukio lakini waliambulia tu kukuta vipande vipande vya mwili wa Profesa Masoud.

Uchunguzi ulibaini kuwa gari la Profesa Masoud liletegwa bomu na watu waliofika usiku nje ya nyumba yake wakiwa kwenye pikipiki.

Vyombo vya habari vya Iran vilikuwa vya kwanza kuripoti kwamba tukio hilo lilionyesha kila dalili kwamba lilitekelezwa na Idara ya ujasusi ya Mossad. Rais Ahmadinejad alitoa kauli kusema kwamba tukio hilo “linakumbusha udhalimu wa kizayoni!”

Profesa Masoud alikuwa ni nguli wa Quantum Physics na mshauri katika mradi wa nyuklia wa nchi ya Iran. Pia vyombo vya habari vya magharibi vililipoti kuwa Profesa Masoud aliwahi kuwa mwanachama wa Revolutionary Guards.
Maisha ya Profesa Masoud kabla ya kifo chake yaligubikwa na usiri mkubwa. Marafiki zake na familia walidai kuwa ndugu yao alikuwa anajihusisha na tafiti za kinadharia tu (theoretical research) na kamwe hakuwahi kujihusisha na miradi ya kijeshi wala kuwa mwanachama wa Revolutionary Guards.

Lakini ajabu ni kwamba katika mazishi yake karibia nusu ya wahudhuriaji walikuwa ni mwanachama wa Revolutionary Guards na hata jeneza lake lilibebwa na maafisa wa Revolutionary Guards. Pia tafiti za kina zilikuja kubaini kuwa Profesa Masoud alikuwa ni moja ya watu muhimu zaidi kwenye mradi wa nyuklia wa nchi ya Iran.

Turudi nyuma zaidi, mwaka 2007 mwezi January, Dr. Ardashir Hossein inaaminika kuwa aliuwawa kwa ‘sumu’ za radioactive.
Taarifa za Intelijensia zinadai kwamba Dr. Hossein alikuwa ni moja ya washauri wakuu wa mradi wa siri wa silaha za nyuklia wa nchi ya Iran. Japokuwa baada tu ya taarifa hizi kuanza kuandikwa kwenye vyombo vya habari serikali ya Iran ilijitokeza na kupinga vikali mambo yote mawili.

Kwanza walipinga taarifa ya Dr. Hossein kuuwawa kwa ‘radioactive materials’ wakidai kuwa Mossad hawana uwezo wa kutekeleza jambo hilo ndani ya ardhi ya Iran lakini pia walidai kuwa Dr. Hossein hakuwa anahusika kwenye mradi wowote wa siri wa nyuklia wa nchi ya Iran. Walidai kwamba Dr. Hossein alikuwa ni mjuzi tu wa kawaida wa Electromagnetism na hakuhusika na masuala yoyoye ya miradi ya siri ya serikali.

Lakini uchunguzi wa kina baadae ulikuja kuonyesha kwamba Dr. Hossein aliwa muajiriwa wa serikali katika vinu vya siri vya kugeuza madini ya Uranium kuwa gas ambayo hii gas hutumika katika urutubishaji kwenye ‘centrifuges’ nyingine zilizopo katika kinu cha siri cha ardhini maeneo ya Natanz.

Lakini pia upo ushahidi mwingine wa kuonyesha kwamba Dr. Hossein alikuwa na mafungamano na serikali. Mwaka 2006 Hossein alitunukiwa tuzo ya juu kabisa na serikali ya Iran ihusuyo masuala ya Sayansi na teknlojia na miaka miwili kabla alitunukiwa tuzo ya juu kutokana na tafiti za sayansi za kijeshi.

Japokuwa serikali ya Iran ilikuwa inakanusha katakata kwamba mfululizo wa mauaji haya ya manguli wa sayansi nchini mwao hayakuwa yakihusiana na miradi yao ya nyuklia lakini ukweli ni kwamba suala hili lilikuwa linawanyima usingizi mno.

Kwanza walikuwa wanakuna vichwa na kupandwa na hasira wakijiuliza ni namna gani Mossad walikuwa wanatekeleza mashambulio haya kwa ufanisi wa hali ya juu licha ya kujitahidi kufanya ulinzi wa kishushushu wa wanasayansi wao ambao walikuwa na maslahi nao katika miradi yao ya siri ya nyuklia.

Lakini Wlwakati ambao walikuwa wanaumiza vichwa kufikiria haya, hawakujua kwamba kama ni mvua basi hizi zilikiwa ni rasha rasha tu.
Degana na vijana wake wa Mossad baada ya miaka mingi ya kujipenyeza kwa siri ndani ya Iran sasa ndio ilikuwa wakati wao sahihi ambao walikuwa wamepanga kutekeleza lengo lao kuu walilokuwa wameliazimia.
Walikuwa na mkakati madhubuti wa kijasusi… Assault Force, double agents, hit team, saboteurs pamoja na ‘front companies’!

MSIBA MKUBWA SANA ULIKUWA MLANGONI MWA TEHRAN.....!!!!!!

3206479997.jpg
 
Ebana eeh huu uzi ni mtamu mpaka hauishiwi na hamu ya kuusoma
Mkuu hao revolutionary group ndo wa kina nani hasa
 
Unajua kwa nini Mossad waliacha kuwauwa wanasayansi wa Iran ? walionjeshwa dawa hiyo hiyo na tangu siku hiyo hukusikia tena mtu kauwawa Iran sababu walijua hakuna nchi ina miliki ugaidi peke yake - ukifanya utafanyiwa -
dawa ipi hio mkuu?

.
 
Sizani kama patakaa atokee rais mwenye msimamo mkali kama mohamoud ahmednejad!!

Swali nnalo jiuliza kwanini marekani anamiliki silaha za nyuklia lakini hawataki wawe nazo??

Kwanini Israel pamoja na kuwa na inteligency agency makini kama MOSSAD lakin bado wanawategemea marekani??

Kwanini na sisi kama tanzania tusianzieshe tafiti za nyuklia au wataalamu hatuna??
 
View attachment 559492

View attachment 559504
View attachment 559505

Siku ya tarehe 23 July mwaka 2011 saa kumi na nusu jioni, watu wawili wakiwa na bunduki ambazo walizificha kwenye majaketi waliyovaa, walishuka kutoka kwenye pikipiki katika mitaa ya Bani Hasheem kusini mwa Tehran na kumimina risasi kwa mtu ambaye alikiwa amesimama mlangoni mbele ya nyumba yake akiwa anajiandaa kuingia ndani akitokea kazini. Mara moja baada ya kufanta shambulio hili walitokomea kusikojulika kabla ya polisi kuwasili.
Mlengwa wa shambulio hili ambaye aliuwawa alikuwa ni Darioush Razaei Najad, Profesa mwanafizikia mwenye miaka thelathini na tano ambaye alikuwa ni moja wa wahusika wakuu katika mradi wa siri wa nyuklia wa nchi ya Iran. Jukumu lake kuu katika mradi huu ilikuwa ni kutengeneza ‘switches’ ambazo zinawekwa kwenye vichwa vya mabomu ya nyuklia (nuclear warheads).

Razaei Najad hakuwa mwanasayansi wa kwanza wa Iran kuwa na mwisho wa kifo cha kikatili kama hiki.

Kwa taarifa rasmi za serikali, Iran walidai kuwa walikuwa wanarutubisha nuclear kwa matumizi ya amani tu kama vile kuzalisha umeme, na walidai kuwa kinu cha Bus Hehr, moja ya vyanzo vikuu vya umeme nchini humo ambacho kilijengwa kwa msaada wa nchi ya Urusi ilikuwa ni moja ya uthibitisho wa kuonyesha kuwa hawakuwa na nia mbaya ya kurutubisha nyuklia.

Lakini pamoja na kinu cha Bus Hehr kutumika kwa matumizi ya kawaida ya kuzalisha umeme, bado kulikuwa na vinu vingine vya siri ambavyo viligundulika ambavyo vilikuwa na ulinzi mkali na hakukuwa na uwezekano wa yeyote asiyehusika kuweza kuingia.

Baada ya muda, Iran iliwapasa kuanza kukubali juu ya uwepo wa vinu hivi vya siri japo waliendelea kukanusha kuwa walikuwa wanarutubisha nyuklia kwa lengo la kutengeneza silaha. Lakini mpaka kufikia muda huu Idara za Intelijensia za nchi za magharibi pamoja na majasusi waliopandikizwa ndani ya Iran walikuwa wameshagundua juu ya uwepo wa maprofesa nguli wa sayansi kwenye vyuo vikuu kadhaa nchini Iran ambao walikuwa wamechaguliwa na serikali ya Iran kwa ajili ya kutumika katika mradi wa kutengeneza bomu la kwanza la nyuklia la Iran.

Lakini kwa kadiri ambavyo Iran walikuwa wanapiga hatua kufikia lengo hili la kuwa na silaha za nyuklia ndivyo ambavyo pia kulionekana juhudi kutoka kwa “watu wasiojulikana” kukwamisha uwezekano wa Iran kumiliki silaha za nyuklia.

Tukirudi nyuma kidogo, siku ya tarehe 29, Novemba mwaka 2010 majira ya saa moja na dakika arobaini asubuhi, maeneo ya kaskazini mwa Tehran, pikipiki iliyopakia watu wawili waliovalia helmet iliibuka kutoka nyuma ya gari la Dr. Majid Shahriyari, mwanasayansi kiongozi wa mradi wa nyuklia wa serikali ya Iran. Pikipiki ilikoleza mwendo ili kuipita gari ya Dr. Majid Shahriyari na walipokuwa wanaipita gari, mmoja wa wale waliopo kwenye pikipiki aligandisha kifaa fulani kwenye kioo cha dirisha la gari upande wa dereva.
Sekunde chache baadae gari lililipuka na kumuua Dr. Majid Shahriyari na kumjeruhi vibaya mkewe.

Wakati huo huo mjini Atas, kusini mwa Tehran, waendesha pikipiki wasiojulikana walifanya kitu hicho hicho kwenye gari aina ya Peugeot 206 inayomilikiwa na Dr. Fereydoun Abas si-Davani na kumjeruhi vibaya yeye na mkewe.

Mara moja baada ya kutokea kwa milipuko hii, serikali ya Iran ilinyooshea kidole Mossad na kuwatuhumu kuendesha mauaji haya ya wanasayansi wake.

Hata baada ya vifo vyao wanasayansi hawa wawili, majukumu yao ambayo walikuwa wanayafanya kwenye miradi ya nyuklia ya Iran iliendelea kuwa ni siri kubwa. Lakini Ah Akbar, kiongozi wa mradi huu wa urutubishaji wa nyuklia alieleza kuwa wanasayansi hao waliouwawa ni mashujaa wa taifa na vifo vyao vimeacha pengo lisilozibika katika timu ya wanasayansi wanaohusika kwenye mradi huu.

Rais wa Iran wa kipindi hicho, Ahmadinejad kama ilivyo hulka yake alionyesha kukasirishwa na vitendo hivi vya mauaji kwa namna ya kipekee kabisa. Moja ya wale wanasayansi walioshambuliwa, Dr. Fereydoun Abas si-Davani ambaye yeye na mkewe walijeruhiwa vibaya lakini hawakufa, Rais Ahmadinejad alimfanya kuwa Makamu wa Rais.

Wale waendesha pikipiki waliotekeleza mauaji haya hawakuwai kujulikana kamwe.

Tukirudi tena nyuma kidogo siku ya tarehe 12 January mwaka 2010 majira ya saa moja na dakika hamsini asubuhi, Profesa Masoud Al Mohammadi alikuwa anatoka nyumbani kwake maeneo ya Shariati mitaa ya Gheytarihe kaskazini mwa Tehran. Asubuhi hii alikuwa anaelekea kazini kwenye maabara ya chuo kikuu cha Sharif (Sharif University of Technology).
Alipojaribu kufungua mlango wa gari yake mlipuko mkubwa ulitokea na kuondoa ukimya uliotawala mitaa hii tulivu. Vyombo vya ulinzi licha ya kuwahi eneo la tukio lakini waliambulia tu kukuta vipande vipande vya mwili wa Profesa Masoud.

Uchunguzi ulibaini kuwa gari la Profesa Masoud liletegwa bomu na watu waliofika usiku nje ya nyumba yake wakiwa kwenye pikipiki.

Vyombo vya habari vya Iran vilikuwa vya kwanza kuripoti kwamba tukio hilo lilionyesha kila dalili kwamba lilitekelezwa na Idara ya ujasusi ya Mossad. Rais Ahmadinejad alitoa kauli kusema kwamba tukio hilo “linakumbusha udhalimu wa kizayoni!”

Profesa Masoud alikuwa ni nguli wa Quantum Physics na mshauri katika mradi wa nyuklia wa nchi ya Iran. Pia vyombo vya habari vya magharibi vililipoti kuwa Profesa Masoud aliwahi kuwa mwanachama wa Revolutionary Guards.
Maisha ya Profesa Masoud kabla ya kifo chake yaligubikwa na usiri mkubwa. Marafiki zake na familia walidai kuwa ndugu yao alikuwa anajihusisha na tafiti za kinadharia tu (theoretical research) na kamwe hakuwahi kujihusisha na miradi ya kijeshi wala kuwa mwanachama wa Revolutionary Guards.

Lakini ajabu ni kwamba katika mazishi yake karibia nusu ya wahudhuriaji walikuwa ni mwanachama wa Revolutionary Guards na hata jeneza lake lilibebwa na maafisa wa Revolutionary Guards. Pia tafiti za kina zilikuja kubaini kuwa Profesa Masoud alikuwa ni moja ya watu muhimu zaidi kwenye mradi wa nyuklia wa nchi ya Iran.

Turudi nyuma zaidi, mwaka 2007 mwezi January, Dr. Ardashir Hossein inaaminika kuwa aliuwawa kwa ‘sumu’ za radioactive.
Taarifa za Intelijensia zinadai kwamba Dr. Hossein alikuwa ni moja ya washauri wakuu wa mradi wa siri wa silaha za nyuklia wa nchi ya Iran. Japokuwa baada tu ya taarifa hizi kuanza kuandikwa kwenye vyombo vya habari serikali ya Iran ilijitokeza na kupinga vikali mambo yote mawili.

Kwanza walipinga taarifa ya Dr. Hossein kuuwawa kwa ‘radioactive materials’ wakidai kuwa Mossad hawana uwezo wa kutekeleza jambo hilo ndani ya ardhi ya Iran lakini pia walidai kuwa Dr. Hossein hakuwa anahusika kwenye mradi wowote wa siri wa nyuklia wa nchi ya Iran. Walidai kwamba Dr. Hossein alikuwa ni mjuzi tu wa kawaida wa Electromagnetism na hakuhusika na masuala yoyoye ya miradi ya siri ya serikali.

Lakini uchunguzi wa kina baadae ulikuja kuonyesha kwamba Dr. Hossein aliwa muajiriwa wa serikali katika vinu vya siri vya kugeuza madini ya Uranium kuwa gas ambayo hii gas hutumika katika urutubishaji kwenye ‘centrifuges’ nyingine zilizopo katika kinu cha siri cha ardhini maeneo ya Natanz.

Lakini pia upo ushahidi mwingine wa kuonyesha kwamba Dr. Hossein alikuwa na mafungamano na serikali. Mwaka 2006 Hossein alitunukiwa tuzo ya juu kabisa na serikali ya Iran ihusuyo masuala ya Sayansi na teknlojia na miaka miwili kabla alitunukiwa tuzo ya juu kutokana na tafiti za sayansi za kijeshi.

Japokuwa serikali ya Iran ilikuwa inakanusha katakata kwamba mfululizo wa mauaji haya ya manguli wa sayansi nchini mwao hayakuwa yakihusiana na miradi yao ya nyuklia lakini ukweli ni kwamba suala hili lilikuwa linawanyima usingizi mno.

Kwanza walikuwa wanakuna vichwa na kupandwa na hasira wakijiuliza ni namna gani Mossad walikuwa wanatekeleza mashambulio haya kwa ufanisi wa hali ya juu licha ya kujitahidi kufanya ulinzi wa kishushushu wa wanasayansi wao ambao walikuwa na maslahi nao katika miradi yao ya siri ya nyuklia.

Lakini Wlwakati ambao walikuwa wanaumiza vichwa kufikiria haya, hawakujua kwamba kama ni mvua basi hizi zilikiwa ni rasha rasha tu.
Degana na vijana wake wa Mossad baada ya miaka mingi ya kujipenyeza kwa siri ndani ya Iran sasa ndio ilikuwa wakati wao sahihi ambao walikuwa wamepanga kutekeleza lengo lao kuu walilokuwa wameliazimia.
Walikuwa na mkakati madhubuti wa kijasusi… Assault Force, double agents, hit team, saboteurs pamoja na ‘front companies’!

Msiba ulikuwa mlangoni mwa Tehran.!!
What a wonderful knowledge

Sent using Jamii Forums mobile app
 
America kumiliki silaha za atomic/ nyukilia si leo,yeye anazo tangia miaka ya 1940 huko ,hivyo kusema kuwa yeye anamiliki ni tofauti na wewe unavyosema kuwa yatakiwa Iran na nchi zingine waanze kutengeneza silaha za nyukilia leo,ni vigum sana amerca na jamaa zake wakubali kwa sababu kuhudumia silaha za nyulilia ni gharama sana.

Hivyo si kila nchi inayojisikia kumiliki silaha hizo itakubalika na hao wakubwa. Kwanza wataangalia mwenendo wa nchi husika kuwa silaha hizi wanazitengeneza kwa ajili ya kumlenga nani? Pia waangalia uwezo wa wewe kuziudumia silaha hizo forever? Tambua kuwa silaha za nyukilia hazina limit ya kinaisha useme kuwa nitakaa nazo miaka10-50 kisha nitazitupa/kuteketeza kule jalalan *"HAPANA"* kamwe hauwezi ni gharama kubwa sanasana,hivyo kumiliki silaha hizo s jambo la sport-sport hata kidogo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom