Wont be the same
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 1,565
- 2,484
Kufuatia wananchi wa kitongoji cha Bogini juu Halmashauri ya wilaya ya Moshi kufunga Barabara ya Mabogini-Kahe kwa madai ya mitaro yake kusababisha mafuriko kwenye makazi yao, Mkuu wa wilaya ya Moshi Godfrey Mnzava amefanya ziara ya kujionea chanzo cha mafuriko hayo na kutoa maelekezo.
Wakizungumza katika eneo hilo wananchi hao wamedai kuwa chanzo cha mafuriko hayo ni baada ya Mkandarasi anaye jenga Barabara ya mabogini-Kahe kuziba baadhi ya mitaro hali iliyopelekea maji kukosa mwelekeo na kwenda kuingia katika makazi ya watu.
Akizungumza mara baada ya kutembelea eneo hilo Mkuu wa Wilaya ya Moshi Godfrey Mnzava amesema kuwa mitaro hiyo inayolalamikiwa na wananchi siyo iliyo changia mafuriko hayo na kuwa wamebaini maji hayo yanatoka milimani kupitia mto Njoro.
Kufuatia hali hiyo ametoa maagizo kwa TARURA kuhakikisha kuwa mitaro ya Barabara ya spekoni-Mabogini km 31 kuhakikisha wanatengeneza mitaro hiyo ili kuachia maji kuingia katika mkondo wake,aidha amewataka wananchi kuendelea kuchukua tahadhari hasa wanaokaa maeneo hatarishi.
Kwa upande wake Kaimu Meneja wa TARURA Wilaya ya Moshi Curthbert Swai amesema kuwa wameshatembelea maeneo mbalimbali na kuangalia mifereji iliyoziba na kusafisha ili kuruhusu maji kupita bila kuacha adha kwa wananchi.