Alvin Slain
JF-Expert Member
- Aug 30, 2011
- 6,375
- 3,655
Jimbo la Moshi vijijini ni moja ya majimbo yenye historia ndefu sana katika halmashauri za mji wa moshi nk Likiwa na utajiri wa kutisha, lakini raia wa jimbo hili wameendelea kuwa katika mazingira yasiyoridhisha kutokana na kukosa muwakilishi sahihi katika kipindi chote ambacho Chaguzi zimekuwa zikifanyika
Mwanzoni kabisa jimbo hili kabla halijatoholewa na kupatikana jimbo la Vunjo lilikua chini ya Augustine Mrema kipindi hicho akiwa NCCR-Mageuzi, Katika mambo mengi ambayo yalifanyika katika jimbo hili, baadhi ni mradi wa KIDEFU, Mradi huo ulikua na lengo la kutengeneza barabara za kibosho,kirima,mpaka Ubwe kwa kiwango cha lami, Raia wa maeneo haya wakaletewa progam maalum ambayo iliwalazimu kukatwa shilingi 20 kila wanapoenda kuuza kahawa KNCU.
Asilimia 90 ya raia wa jimbo hili ni wakulima wa kahawa, ikumbukwe mradi huu uliifanyika Mrema akiwakilisha jimbo la Moshi vijijini na baadaye Thomas Ngawaiya akafuatia Cyril Chami na Antony Komu wote hawa walishindwa kulisemea jimbo la Moshi vijijini na hivyo mradi ule wa kidefu ukaishia njiani mpaka leo matank hayo yaliyoletwa chini ya Mrema kwa ajili ya kutengeza barabara yapo kati ya Usagara Kirima na hakuna kikichoendelea kutoka hapo, Sasa tunataka msemaji kule Bungeni.
Mtu anaelewa anaefahamu changamoto zilizopo ndani ya jimbo hili, Hatuwezi kuchagua Mbunge ambae anakuja kutembea wakati wa kampeni, Hivyo mgombea atoke chama chochote, ila cha msingi na kilicho na mbolea awe msemaji wa changamoto za raia kule Bungeni.