Morrison akubali kubaki Simba, umafia wafanyika usiku huu, Yanga hawaamini macho yao

Mwishokambi

JF-Expert Member
Nov 23, 2020
303
1,158
Kama ulidhani Simba ni paka basi andika umeumia, Simba imefanikiwa kumbakisha Morrison ambaye alikuwa tayari amesainishwa mkataba Leo na yanga, kikao kilichofanyika usiku wa Leo na kumalizika usiku huu kikiongozwa na mamafia wa usajili Simba kiliamua kwa kauli moja Morrison aendelee kutumikia klabu, Morrison alieleza yake ya moyoni na uongozi ukaeleza yao na hatimaye wamekubali kuanza moja, wale waliomsainisha mkataba Morrison wameliwa mzigo wao.

Kwa kweli penye miti hakuna wajenzi, mafia wa Simba walikula timing baada ya kuona Yanga wamemwaga mpunga na kumpa kandarasi ya miaka 2 wakaona kwa vile bado mkataba wao na Morrison haujakwisha, wamekaa naye Leo usiku na kuyamaliza.

Morrison aliwaambia viongozi hao kuwa anaipenda sana Simba, alilazimika kurudi yanga kwa sababu hakuwa na jinsi lkn anaipenda Simba from the bottom of his heart na ndio maana aliomba mashabiki wampe jezi 100 azipeleke kwao akaage.

Simba walimwambia hawakutaka kumuaga kwa sababu bado wana mipango naye, poleni sana yanga, nyie endeleeni na Chico Ushindi tu, Morrison amekubali kubaki Simba.
 
Yaani vitu ambavyo washabiki wa Simba wanashabikia msimu huu hadi aibu. Kwahiyo hapo mnaona mmeweeeeza wenyewe. Msimu mliopita si mlikuwa nae Morrison, aliwasaidia Nini?

Yanga walitaka kumchukua Morison sababu ya revenge tu ila sio kipaumbele Chao kabisa na isitoshe kwann Simba mnachezeshwa gwaride kwenye usajili na Yanga hivi? Alafu mnafatisha tu wakati wenzenu wanawaingiza Chaka. Simba kiuhalisia hamumuitaji Morison ila Kwa kuwa Yanga kawatisha kumsajili mmejaa kingi mmevaba, poleni sana.
 
Yaani vitu ambavyo washabiki wa Simba wanashabikia msimu huu hadi aibu. Kwahiyo hapo mnaona mmeweeeeza wenyewe. Msimu mliopita si mlikuwa nae Morrison, aliwasaidia Nini?

Yanga walitaka kimchukua Morison sababu ya revenge tu ila sio kipaumbele Chao kabisa na isitoshe kwann Simba mnachezeshwa gwaride kwenye usajili na Yanga hivi? Alafu mnafatisha tu wakati wenzenu wanawaingiza Chaka. Simba kiuhalisia hamumuitaji Morison ila Kwa kuwa Yanga kawatisha kumsajili mmejaa kingi mmevaba, poleni sana.
Yaan uto mwenzangu umepovuka kweli
 
Attachments

  • 20220623_152502.jpg
    20220623_152502.jpg
    50.7 KB · Views: 7
Yaani vitu ambavyo washabiki wa Simba wanashabikia msimu huu hadi aibu. Kwahiyo hapo mnaona mmeweeeeza wenyewe. Msimu mliopita si mlikuwa nae Morrison, aliwasaidia Nini?

Yanga walitaka kimchukua Morison sababu ya revenge tu ila sio kipaumbele Chao kabisa na isitoshe kwann Simba mnachezeshwa gwaride kwenye usajili na Yanga hivi? Alafu mnafatisha tu wakati wenzenu wanawaingiza Chaka. Simba kiuhalisia hamumuitaji Morison ila Kwa kuwa Yanga kawatisha kumsajili mmejaa kingi mmevaba, poleni sana.
daah ila nyie mashabiki ni nomaaa, si ndo wee ulosema kuwa morisson atawafikisha mbali, na ngao ya jamii atatuua, uwiiiiih
 
Nilistaajabishwa na uamuzi wa Simba kumwacha Morrison. Yule jamaa mbona kimataifa ametubeba mara nyingi sana? Mmesahau zile faulo zake za haraka haraka kabla wapinzani hawajapanga ukuta?

Yale matatizo mengine yanavumilika.Mbona AC Milan ilimvumilia Gennare Gattuso?
Tatizo ya morrison ni sio team player. Wachezaji wapo watukutu lakini akiingka uwanjani ni team first yeye second. Hao unaweza wavumilia
 
Nilistaajabishwa na uamuzi wa Simba kumwacha Morrison. Yule jamaa mbona kimataifa ametubeba mara nyingi sana?

Mmesahau zile faulo zake za haraka haraka kabla wapinzani hawajapanga ukuta?

Yale matatizo mengine yanavumilika. Mbona AC Milan ilimvumilia Gennare Gattuso?
Hilo halina ubishi,ila tatizo unaishi na mchezaji anakuweka roho juu juu. Na hawezi kubadilika
 
Viongozi wa Simba acheni upuuzi.Umafia ndio nini?
Maana naona ni upumbavu tu.Kwa nini mwanzo mlimuaga Morrison halafu leonajidai eti mmefanya.umafia?

Hizi ndizo habari za kipumbavu ambazo mimi sizipendi.
Kwa nini mjidai mnashindana na yanga ambayo kwenye ranking za CAF ni ya 80 huko na ninyi ni wa 12?

Morrison ni muhimu sana kwa Simba lakini acheni kufanya mambo ya kishamba.Lazima mkue
 
Upuuzi mtupu, who is Morrison by the way?
Angekuwa siyo wa maana Kwenu akina Haji Manara, Mohammed Bhinda na Injinia Hersi Said wangekuwa kutwa Wanamuita pale Slip Way na kumpa Ahadi nyingi kama akirejea Yanga SC?

Huna unachokijua na uwe Unanyamaza tu. Siyo nyie mliokuwa mkifurahi mliposikia kuwa Morisson anarejea Yanga SC? Yaani leo baada ya kusikia hapa kuwa Simba SC imembakisha ndiyo mnasema wa nini?

Wanafiki na Majuha wakubwa nyie.
 
Viongozi wa Simba acheni upuuzi.Umafia ndio nini?
Maana naona ni upumbavu tu.Kwa nini mwanzo mlimuaga Morrison halafu leonajidai eti mmefanya.umafia?

Hizi ndizo habari za kipumbavu ambazo mimi sizipendi.
Kwa nini mjidai mnashindana na yanga ambayo kwenye ranking za CAF ni ya 80 huko na ninyi ni wa 12?

Morrison ni muhimu sana kwa Simba lakini acheni kufanya mambo ya kishamba.Lazima mkue
Mbona Mapovu Mkuu? Imewakereni sana au? Poleni na hapo bado.....!!!!
 
Back
Top Bottom