Morogoro: Wanafunzi 500, walimu wao wajisaidia migombani

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,253
Wasaalam wakuu,
Kwa habari hii niliyokutana nayo leo, nimegundua Tanzania bado tuna safari ndefu.
Lakini nimegundua mambo yanakuwa magumu kwa sababu kila kitu tunaiachia serikali.
Nafikiri ifike mahali wananchi kwa umoja wetu tuisaidie serikali kwa baaadhi ya mambo yaliyo kwenye uwezo wetu.
Nawasilisha,
I stand to be corrected!

===============

dawa-620x308.jpg

Abiria wakijisaidia porini, hali hiyo hipo katika baadhi ya mashule hapa nchini

ZAIDI ya wanafunzi 500 na walimu watatu wa Shule ya Msingi Luholole kwenye Kata ya Kibuko, Wilaya ya Morogoro Vijijini, wako hatarini kukumbwa na magonjwa ya mlipuko kutokana na kukosa vyoo, anaandika Christina Raphael.

Utafiti uliofanywa na Mtandao wa Habari za Kijinsia (TGNP) kwa kushirikiana na wanahabari mjini hapa umebaini kuwa, jumla ya wanafunzi 535 pamoja na walimu wao watatu wanajisaidia kwenye migomba iliyopo pembeni mwa shule hiyo kutokana na kukosa vyoo shuleni hapo.

Obed Simkanzya, Mwalimu Mkuu wa shule hiyo amekiri kuwa walimu na wanafunzi wake wanajisaidia kwenye migomba kutokana na kukosa vyoo.

Anasema, tangu shule hiyo ianzishwe mwaka 1973, imekuwa inakabiliwa na ukosefu wa vyoo, na hivyo wanafunzi, walimu na wa
fanyakazi wengine hujisaidia kwenye migomba hiyo.

Kutokana na hali hiyo wanafunzi wamekuwa wakiugua mara kwa mara.

Vile vile, wanakabiliwa na ukosefu wa maji, madawati na samani za ofisi; wana miundombinu duni na upungufu mkubwa wa walimu.

“Uwezekano wa watoto kupata magonjwa ya milipuko ni mkubwa sababu wengine hucheza kwa kufukua michanga jirani na vilipo vinyesi vilivyokauka,” amesema.

Mtandao huu ulishuhudia watoto wasiovaa viatu wakicheza michezo mbalimbali na kuchimba udongo jirani na maeneo hayo bila tahadhari.

Shiwa Chalo, Mwenyekiti wa Kamati ya shule hiyo, anasema, matatizo ya vyoo yanatokana na wananchi kukatishwa tamaa na serikali kwa kushindwa kusaidia nguvu za wananchi kwenye shule hiyo.

Chanzo: Mwanahalisi Online
 
Hiyo shule ni ya mjini au kijijini? miaka hii bado watu wanajisaidia hovyo?
 
Huyo mwl mkuu wa kufuta kazi na kamati ya shule....choo hata tundu 2 ameshindwa kushughulikia!!!
 
Swala pia wananchi kwa umoja wao wanaweza kuungana na kujenga vyoo, mbona kuna maeneo mengine wanafanya hivyo. Ifike mahala tuache kubweteka na kutegemea serikali tuu!
 
Ndio maana nimesema mwl mkuu na kamati wafutwe, kazi ya mkuu wa shule ni kuita kamati ya shule na kuileza matatizo au mapungufu na kamati kazi yake ni kupeleka serikali ya kijiji ili kuomba nguvu au michango toka kwa wananchi, hili linafanyika nchi nzima, kwanin wao wasiwajibike?
 
Na kwa uongozi wa awamu hii mtakunya maporini mpk muumwe na Nyoka kwenye makalio.
Si mlikuwa mnashangilia?

Tulieni sasa dawa iingie
 
Back
Top Bottom