MOROGORO: Polisi aua watu wawili akijihami

MOROGORO: Polisi aua watu wawili akijihami

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,303
Morogoro. Watu wawili wamekufa kwa kupigwa risasi na askari polisi baada ya kuibuka mzozo kuhusu ng’ombe waliokamatwa katika Kijiji cha Nyalutanga wilayani Morogoro.

Pia, imeelezwa mtu mmoja amejeruhiwa kwa risasi kwenye makalio na ng’ombe 35 wameuawa na zaidi ya 40 kujeruhiwa katika mzozo huo.

Hata hivyo, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Dk Stephen Kebwe ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa amethibitisha vifo

vya watu hao wawili, akisema hana taarifa kuhusu aliyejeruhiwa.

Dk Kebwe amesema mzozo huo umeshapatiwa ufumbuzi na waliokufa katika tukio hilo wamezikwa leo Jumanne, huku uchunguzi ukiendelea kuhusu wananchi waliojichukulia sheria mkononi na kumshambulia kwa mawe askari aliyefika kutuliza mzozo huo.

Mkuu wa mkoa amesema ameunda kamati kuchunguza tukio hilo ambalo lilisababisha askari kufyatua risasi hewani kuwatawanya wananchi waliokuwa wamemzonga na kwa bahati mbaya risasi ziliwapata watu wawili.

Amesema watakaobainika watachukuliwa hatua za kisheria. Pia, amewaonya wafugaji wanaoacha mifugo ikizurura ovyo.

Akizungumzia tukio hilo, Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Nyalutanga kilichopo Kata ya Kisaki, Said Masongele amesema mzozo huo ulitokea jana saa saba mchana katika eneo la ofisi za serikali ya kijiji.

Masongele amewataja waliofariki dunia kuwa ni Ramadhan Kiwenge na Kibwana Msipwile.

Amesema mkazi mwingine Ismail Msagule amejeruhiwa kwa kupigwa risasi kwenye makalio na amelazwa katika zahanati hiyo.

Mwenyekiti huyo amesema hilo lilitokea baada ya mifugo kuingia shambani kwenye bonde la Kikwato na kukamatwa na mgambo na walinzi wa jadi (Sungusungu).

Amesema awali, viongozi wa kijiji wakiwa kwenye kikao walipata taarifa kwamba kuna mifugo imevamia mashamba, hivyo walitumwa mgambo kwenda kuikamata.

Muda mfupi baadaye amesema alipokea simu ikieleza Mohamed Kassim alijeruhiwa kichwani na mfugaji wakati wa kukamata mifugo.

Mgambo wa kijiji hicho, Kibwana Mbegu aliyeshiriki kukamata mifugo amesema watu hao watatu walifyatuliwa risasi wakati askari akijihami baada ya wananchi kujaribu kupora silaha.

“Tulikamata mifugo isiyopungua 80 katika mashamba ya Kikwato ikila mazao, wakati tukifanya hivyo mwenzetu alijeruhiwa kwa kupigwa fimbo kichwani na mfugaji. Tuliwazidi nguvu wafugaji na kuswaga mifugo hadi ofisi za kijiji kwa hatua za kisheria,” amesema Mbegu.

Mbegu amesema baada ya dakika chache, wafugaji walifika ofisi za kijiji wakiwa na silaha za jadi, wakati huo wananchi wakiwa wanakusanyika huku kukiwa na askari polisi mwenye silaha kulinda amani eneo hilo.

Amesema baada ya wafugaji kufika eneo hilo, walianza kuchukua mifugo kwa nguvu jambo lililosababisha askari kufyatua risasi hewani kuwatawanya.

Mbegu amesema baadhi ya wananchi walimfuata askari kwa lengo la kumnyang’anya silaha, huku wengine wakirusha mawe.

Amesema askari alifyatua risasi ili kuwazuia ambazo ziliwapata watu wawili na baadaye alikimbia eneo hilo.

Mgambo huyo amesema kundi la wananchi lilimkimbiza ndipo alipofyatua risasi nyingine iliyomjeruhi mwananchi mwingine kwenye makalio.

Amesema askari huyo alijificha ndani ya nyumba kijijini hapo na alipiga simu kituo cha polisi Kisaki Gomero kuomba msaada kwa wenzake waliomuokoa katika eneo hilo ambalo lilikuwa limezingirwa na wananchi.

Chanzo: Mwananchi
 
Vuta vya wafugaji na wakulima kuisha ni ngumuu

Ova
 
Alirusha risasi hewani alafu zikawapata wananchi?

Alafu mtu anaekukimbiza unawezaje kumpiga risasi ya tako (makalio)?

I smell something fishy here!

Mazoea hujenga tabia.Polisi wataendelea kuua na wataendelea kutetewa na maboss wao kwa sababu ni Tawi la CCM
 
Huyo askari kama vile alikusudia Kuua. Kuna Paragraph zinakinzana.
1. Alirusha risasi hewani kuwatishia
2. Alirusha risasi kujihami na waliotaka kumnyanganya silaha.
Utata upo kwenye para inayosema "walikuwa wanamkimbiza ili wamnyang'anye silaha akawafyatulia risasi ikampata mmoja kwenye matako"

Hiyo risasi imeishi mombasa sana.
Yaani inazunguka kufuata makalio tu!?
 
Mazoea hujenga tabia.Polisi wataendelea kuua na wataendelea kutetewa na maboss wao kwa sababu ni Tawi la CCM
Kuna ka spirit nimeka acknowledge kwenye huu mtiti.

"watu walikuwa wanamfukuzia ili wamnyang'anye silaha"
 
Kuna ka spirit nimeka acknowledge kwenye huu mtiti.

"watu walikuwa wanamfukuzia ili wamnyang'anye silaha"

Kuna jambo amefanya siyo bure.Ukiona nyoka anakukimbiza ujue umemjeruhi
 
Kuna jambo amefanya siyo bure.Ukiona nyoka anakukimbiza ujue umemjeruhi
Wangemnyaka na kumnyang'anya smg mbivu na mbichi zingesomeka.
Iko siku watabugi!
 
WALIAMBIWA HARAKAHARAKA KABLA HAWAJANYANG'ANYWA SILAHA
 
Yaani askari hapo ana haki ya kupiga kabisa risasi, yaani wananchi wanamfuata kutaka kumnyang'anya silaha.. Hata ingekuwa mm napiga risasi.. Kuna wakati mwingine huna option zaidi ya kuwachapa tu
 
Alirusha risasi hewani alafu zikawapata wananchi?

Alafu mtu anaekukimbiza unawezaje kumpiga risasi ya tako (makalio)?

I smell something fishy here!
Anayekukimbiza ukimgeuzia risasi atabaki anakukodolea macho eeee?


Tumia akili ndugu, hata kama ni za kuazima. Zitumie tu
 
Samahanini naomba kufafanuliwa. Mimi sijawahi kujifunza matumizi ya silaa lkn je risasi ikipigwa juu inaweza kushuka chini na nguvu ile ile na ikaua mtu?
 
Kuna ka spirit nimeka acknowledge kwenye huu mtiti.

"watu walikuwa wanamfukuzia ili wamnyang'anye silaha"
Alafu hao watu wakaelekea hewani, akarusha risasi huko hewani ili kuwatawanya risasi zikawapata kwenye matako zikawaua.
 
Yaani askari hapo ana haki ya kupiga kabisa risasi, yaani wananchi wanamfuata kutaka kumnyang'anya silaha.. Hata ingekuwa mm napiga risasi.. Kuna wakati mwingine huna option zaidi ya kuwachapa tu
Tena inaonekana bunduki ilikuwa na risasi chache.

Otherwise, ningekuwa mimi na nina risasi za kutosha ktk mashine ningewapa za kichwa faster ili waache viherehere.
 
Back
Top Bottom