PreGE2025 Morogoro: Devotha Minja na baadhi ya G55 pamoja na wananchama wajivua uanachama CHADEMA

PreGE2025 Morogoro: Devotha Minja na baadhi ya G55 pamoja na wananchama wajivua uanachama CHADEMA

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
2,786
Reaction score
7,567
Wakuu, haya wacha tuone leo ni nani anajiahibisha leo na kuutangazia umma anaenda kuchukua 'chai' kwa CCM.

====

G55 Morogoro kuzungumza na waandishi wa habari kujiondoa CHADEMA

Meza Kuu inajumuisha;

Devotha Minja - ameanza kwa kutambulisha salamu yao ya mapambano: "Aluta Kontinua Mapambano Mpaka Kieleweke Hakuna Kushusha silaha chini mpaka kieleweke"

Nilijiunga CHADEMA toka 2010 na kushika nafasi mbalimbali kwenye chama, ikiwemo kuwa mwenyekiti wa BAWACHA Morogoro. Niliona chama stahiki cha kwenda kufanya mapambano ni CHADEMA, nilipoteuliwa kuwa mbunge wa Morogoro niliona nimepata nafasi ya kuwasema wananchi. Tulisaidiana kuhakikisha tunadhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma. Suala la No Reform No Reform kama mjumbe wa kamati kuu hakuna popote tumewahi kusema tunazuia au kususia uchaguzi, yanayoendelea sasa ni watu wachache wanaohadaa wananchi kuwa CHADEMA inauwezo wa kuzuia uchaguzi.

Mnaona yanayoendelea sasa wako watu mbalimbali wanapotea na kutekwa, maamuzi hayo ya kwenda kuandamana ni maamuzi ya watu wachache na sio kamati kuu. Makamu Mwenyekiti ameshindwa kuitisha kikao tujadili kama kamati kuu jinsi ya kukabiliana na suala Lissu ili atoke Gerezani. Tumeshuhudia viongozi na wananchama wetu wakishambuliwa siku ya kesi ya Lissu Aprili 24 lakini makamu mwenyekiti ameshindwa kuitisha mkutano kuhakikisha tunakabiliana vipi hili.

Ni kweli Mbowe alisema kuhusu No Reform No Election, lakini Mbowe alisisitiza kuwa wakati ukifika hatujapata reforms chama hakitafanya maamuzi sahihi, sasa hii ya sasa ni lini chama ilipitisha maamuzi haya wakati hakuna kikao ambacho tulihudhuria? Ndani ya Kamati Kuu kumekuwa na ubaguzi na matusi, kuna grup la whatsap ambalo linahakikisha wengine hatupati taarifa, niliondolewa kwenye group hilo baada ya kuhoji kutengwa kupewa taarifa. Naondolewa sababu ya kumuunga Mbowe?!

Tumezuiwa kushiriki uchaguzi hadi 2030, maamuzi haya ilibidi wote tushirikishwe, lakini haikuwa hivyo, nakwepwa kwenye ziara sababu tu nilikuwa namsapoti Mbowe, viongozi wanaendelea kuwahadaa wananchi kuwa tutashiriki uchaguzi wakati tumeshaondolewa, bora wakaewaeleza wananchi ukweli.

Nimetafakari sana, nimeona siwezi kuwa mbinafsi kuua ndoto za wananchi kwa kuwa sehemu ya CHADEMA. Wapo watu wanaoaminishwa kuhusu akidi kutimia kwenye kikao cha baraza kuu, kikao kile kilikuwa na wajumbe 85 kati ya kati ya wajumbe 412 ambao ilitakiwa kupitisha sekretariati na wajumbe wa kamati kuu. Chama kimegeuka kuwa chama cha matusi, kejeli, kutukana waliokuwa wanamsapoti Mbowe, hakuna upendo tena, wanachama wanandoka viongozi hawatoki kujibu, CHADEMA imegeuka kuwa chama cha kiuanaharakati. Natangaza rasmi leo Mei 15, 2025 kujivua uanachama pamoja na nafasi zote CHADEMA. Nilifikiri niko mwenyewe lakini baada ya kuona maelfu kwa maelfu mpo nyuma yangu nimeona sipo mwenyewe. SItakwenda CCM, CCM si mahali sahihi kwangu.

Walau Devotha Minja kapokea maswali japokuwa amejibu upuuzi 😂

Katibu BAWACHA Morogoro Mjini - Dorothy Mwansasu - Najivua uanachama CHADEMA, naachana na harakati za siasa morogoro mjini ntakuwa mwananchi wa kawaida katika nchi nchi, niwaahidi nitaendelea na mapambano ya kuwakomboa wananchi nchini.

Katibu BAVICHA Morogoro - Emmanuel Mpesa - naungana na Devotha Minja kutafuta njia nyingine ya mabadiliko, natangaza rasmi kuvua uanachama wangu CHADEMA

Katibu BAZECHA - Thomas Charles Kaumbe - Mwenyekiti wa sasa amekuwa mfadhili wa watu wanaotushambulia, hatuwezi kwenda mbele kama hakuna umoja najivua uanachama kuanzia leo, sitaenda CCM

Mjumbe Mkutano Mkuu Taifa - Wolfgang Ngalapa - Nimejisikia vibaya kutoshirikisha kamati, baraza, wanachama na mkutano mkuu kutoshiriki uchaguzi, kuanzia sasa najivua uanachama CHADEMA, natafuta mlango mwingine

Wajumbe wa kamati tendaji CHADEMA Morogoro Mjini - Athumani Kambi -
Natangaza rasmi kujivua uanachama CHADEMA. Mtu ukiona moto umezimika jimboni kwako uatatafuta kwengine moto unakuwaka ukaendeleze harakati huko. Leodigadi Kaizilege natangaza kuanzia leo kuvua nafasi zote nilizokuwa nazo pamoja na uanachama

Mwenyekiti BAWACHA Mji Mpya - Christina Ngowi - Naungana na Devotha, najivua uanachama CHADEMA pamoja na nafasi zangu

Katibu BAWACHA Mji Mpya - Jalina Mnota
- naunga mkono yaliyoongelewa na kujivua uanachama CHADEMA pmaoja na nafasi zangu zote

Mwenyekiti BAWACHA Mkundi - Latifa Mohammed
- kutokana na msuguano na matatizo yanayoendelea, namuunga mkono Devotha, najivua uanachama CHADEMA pamoja na nafasi zangu

Mwanahawa Sabo - nimekuwa mwanachama mpambanaji na huko ntakapoenda nytakuwa mpambanaji, anapoenda Devotha nami ntaenda, najivua uanachama wangu CHADEMA

Mjumbe wa Mkutano Mkuu, Kamati Tendaji Mkalama- Singida, Mtiania Jimbo la Mkalama - Babysh
- naungana na Devotha, najivua uanachama wangu CHADEMA
 
Ngoja waje chadema pro wajipe Moyo wakati kiuhalisia kuna kitu hakipo sawa chamani
 
Mtakebehi na kukejeli lakini kuna kitu hakiko sawa CHADEMA. Kaeni mzungumze muelewane. Udikteta uchwara hatimaye utaleta madhara makubwa Chamani. This is unprecedented na hawa wanaoondoka siyo kweli kwamba wote ni mapandikizi na hawafai. Kuna tatizo!
 
Wataondoka baadae wataona hakuna kinachobadilika.

Pia, wananchi mbali na kuzoea, wanaona hizi ni drama tu.
 
Wakuu, haya wacha tuone leo ni nani anajiahibisha leo na kuutangazia umma anaenda kuchukua 'chai' kwa CCM.

====

G55 Morogoro kuzungumza na waandishi wa habari kujiondoa CHADEMA

Meza Kuu inajumuisha;

Devotha Minja
Katibu BAWACHA Morogoro
Katibu BAVICHA Morogoro
LKatibu BAZECHA CHAZI
Mjumbe Mkutano Mkuu - Wolfgang
Wajumbe wa kamati tendaji CHADEMA Morogoro Mjini
Mjumbe wa kamati tendaji BAWACHA Morogoro
Mwenyekiti BAWACHA Mji Mpya
Mwenyekiti BAWACHA Mkundi
Katibu BAWACHA Kilakala
Mtiania Jimbo la Mkalama

Devotha Minja

Ameanza kwa kutambulisha salamu yao ya mapambano: "Aluta Kontinua Mapambano Mpaka Kieleweke Hakuna Kushusha silaha chini mpaka kieleweke"

Nilijiunga CHADEMA toka 2010 na kushika nafasi mbalimbali kwenye chama, ikiwemo kuwa mwenyekiti wa BAWACHA Morogoro. Niliona chama stahiki cha kwenda kufanya mapambano ni CHADEMA, nilipoteuliwa kuwa mbunge wa Morogoro niliona nimepata nafasi ya kuwasema wananchi. Tulisaidiana kuhakikisha tunadhibiti matumizi mabaya ya fedha za umma. Suala la No Reform No Reform kama mjumbe wa kamati kuu hakuna popote tumewahi kusema tunazuia au kususia uchaguzi, yanayoendelea sasa ni watu wachache wanaohadaa wananchi kuwa CHADEMA inauwezo wa kuzuia uchaguzi.

Mnaona yanayoendelea sasa wako watu mbalimbali wanapotea na kutekwa, maamuzi hayo ya kwenda kuandamana ni maamuzi ya watu wachache na sio kamati kuu. Makamu Mwenyekiti ameshindwa kuitisha kikao tujadili kama kamati kuu jinsi ya kukabiliana na suala Lissu ili atoke Gerezani. Tumeshuhudia viongozi na wananchama wetu wakishambuliwa siku ya kesi ya Lissu Aprili 24 lakini makamu mwenyekiti ameshindwa kuitisha mkutano kuhakikisha tunakabiliana vipi hili.

Ni kweli Mbowe alisema kuhusu No Reform No Election, lakini Mbowe alisisitiza kuwa wakati ukifika hatujapata reforms chama hakitafanya maamuzi sahihi, sasa hii ya sasa ni lini chama ilipitisha maamuzi haya wakati hakuna kikao ambacho tulihudhuria? Ndani ya Kamati Kuu kumekuwa na ubaguzi na matusi, kuna grup la whatsap ambalo linahakikisha wengine hatupati taarifa, niliondolewa kwenye group hilo baada ya kuhoji kutengwa kupewa taarifa.

Huyu DEVOTHA minja anaota ubunge wa morogoro muda wote, hawezi kumtoa abood morogoro kamweh....Ubunge atausikia redioni tu...
 
Back
Top Bottom