Morogoro CCM isiruhusu waroho wa madaraka ya uwaziri kuleta mgawanyiko wa chama na wanachama

FDR.Jr

JF-Expert Member
Jun 17, 2008
1,359
353
CCM KUANZIA MEI 2015 MPAKA TAREHE MOSI AUG 2015 IMEPITIA DEMOKRASIA YA KUPIMA MAKADA WAKE WANAOWANIA DHAMANA ZA UONGOZI WA SERIKALI KWA NJIA YA DOLA KUU, BUNGE NA MADIWANI NCHINI KOTE.

MCHAKATO HUU WA CCM UMEKAMILIKA KWA KUGAWA MAKUNDI YALOUNGANA NDANI YA CHAMA KUTETEA WAMUAMINIYE ILI APEWE DHAMANA YA CCM KUSHINDANI NA WAPINZANI IFIKAPO OKTOBA 25 ,2015.

MKOA WETU NI SEHEMU CHANYA NA RAFIKI WA UHURU WA TANGANYIKA NA MAPINDUZI YA ZANZIBAR, HISTORIA IMEONYESHA HATA PALE ZUBERI MTEMVU MWANA MOROGORO MWENZETU ALIPOKIHAMA TANU NA KUUNDA ANC ,TANU ILIMSIMAMISHA MWALIMU NYERERE KUSHINDANA NA MTEMVU NA WANA MOROGORO WAKAMPA USHINDI NYERERE...SI HILO TU MWALIMU ALIWAHI KUWA MBUNGE WA ENO HILI AKIMSHINDA CHIFU KUNAMBI.

1995 NI CCM MOROGORO HII CHINI YA UONGOZI WA ISACK MWISONGO ILIMUUNGA MKONO JAKAYA KIKWETE LAKINI CCM IKAMPITISHA BEN MKAPA KUWANIA URAIS...

MWAKA 2005 CCM MOROGORO ILIMUUNGA MKONO KIKWETE TENA HUKU KINA DKT NGASONGWA WAKISIGANA NA MKUU WA MKOA MZEE MASHISHANGA ALIYEMUUNGA MKONO SUMAYE...KIKWETE ALIPATA

2015 WAZEE WA CCM WAKIONGOZWA NA ISACK MWISONGO, DKT NGASONGWA NA STEVE MASHISHANGA WALIMUUNGA MKONO MWANA CCM MWENZAO LOWASSA ILA CCM IKAJA NA DKT. JOHN MAGUFULI, WAZEE HAWA KWA KAULI MOJA WAKATAMKA MBELE YA MTEULE KUWA WALIMUUNGA MKONO LOWASSA KABLA YA UCHAGUZI , CCM IMEKUCHAGUA WEWE, SISI MOROGORO SI ZAIDI YA CCM TUNAHESHIMU MAAMUZI YA CHAMA CHETU NA TUNAKUUNGA MKONO TENA WAKIMPA HISTORIA YAO NA WATAWALA WALIOPITA NA WANAONDOKA NDANI YA CCM


NINAYAANDIKA HAYA LEO NA MUDA HUU KWA SABABU YA MUENDELEZO WA SIASA ZA MAJITAKA AMBAZO ZIMEASISIWA NA CCM ULANGA ILI KUMPITISHA MTU ASIYE NA SIFA WALA WEREDI WA SIASA NA MAENDELEO ANAYEITWA YASSIN NJAYAGHA.

LEO AMEENDESHA KAMPENI CHAFU DHIDI YA WAGOMEA WENZAKE AMBAO WILAYA HIYO YA ULANGA IMEWAPENDEKEZA MKOANI KWA ALAMA SAWA NA YEYE HAO NI dKT. MPONDA NA ANTIPAS MGUNGUSI.

WAGOMBEA HAWA WALIKUWA NA DOSARI KAMA TATU HIVI...


MSHINDI WA KURA ZA MAONI MH. DKT MPONDA-KURA BAADA YA UHAKIKI MPYA -3886
-Ana tuhuma za kupewa kura hewa takriban 2000 kijijini kwake-Imethibitika Kamati Maadili na ile yasiasa Ulanga
-Ametuhumiwa kutoa rushwa-Haijathibitika na haina ushahidi wowote
MSHINDI WA PILI KURA ZA MAONI ANTIPAS MGUNGUSI-KURA ZAKE HALISI 2510
-Ametuhumiwa rushwa,kuwa Dkt Ngasongwa anamsaidia-Haijathibitika na hakuna ushahidi wowote
MSHINDI WA TATU KURA ZA MAONI YASSIN NJAYAGHA-KURA ZAKE HALISI BAADA UKAGUZI MPYA NI 1954
-Ametuhuhumiwa kupewa kura hewa 1450 na Watumishi wa Chama Wilaya -Imethibitika mbele ya Kamati ya Maadili na ile ya Siasa Ulanga

Taarifa zetu zaonyesha Mtia Nia aliyeambulia nafasi ya Tatu ndie chanzo cha habari za uwepo wa Rushwa ktk mchakato huu akisaidiwa na Watia Nia waloshika na.4,5,6,7. Taarifa ni kwamba wote kwa pamoja wanasiadiwa na Waziri wa Nchi Kombani ambaye amejiapiza kumpa nafasi ya Ubunge Malinyi huyu Mgombea na.3

Mgombea namba tatu si mtu mgeni hapa JF kama mtakumbuka ni huyu huyu aliyewalaghai Msafara wa Rais Kikwete 2006 walipoenda USA na kujitambulisha kuwa yeye ni Rais wa Watanzania wanaoishi Marekani, taarifa ile ilimchafua sana Dkt Ngasongwa ambaye bila kujua alimtambulisha Yassin Njayagha kama kijana wa nyumabni aishiye Marekani na Rais Kikwete akampokea yeye na wenzake kwa kujali ni vijana wake walioko ughaibuni...Yassin Njayagha akijua wazi yeye si Kiongozi wa Watz waliopo America akaamua kuitumia nafasi kujijengea wasifu asio nao...

2008 akarejeshwa Nchini toka USA...sababu tunazihifadhi...2010 akajitosa kugombea Ubunge akawa mshindi wa Pili nyuma ya Dkt Mponda, mwaka huu amejitosa tena akiwa wa tatu nyuma ya Mponda na Mgungusi lakini kwa hila za fitina akaamua kuutafuta Ubunge kwa nguvu wa wenye Mamlaka serikalini na Chamani Wilayani na sasa jana na leo Mkoani.

Morogoro leo jina la Mgungusi limeendelea kufanyiwa zengwe lile la Mahenge..safari Mgombea wa Ulanga anashawishi CCM Mkoa impitishe Njayagha na kumpa tuhuma mpya Mgungusi eti kwakuwa Ngasongwa na Wazee wa Morogoro walimuunga mkono Lowassa kwenye maoni ya Urais wa CCM na huyu kijana ni walewale...

Hoja hii imeshasambaa Malinyi na Morogoro ikimuhukumu kijana wa CCM mwenye miaka 32 kuwa hapaswi kufikiriwa na chama eti kisa wazee aliowaomba wamuunge mkono ni wale waliompokea Lowassa Morogoro!!!

Yassin Njayagha aliyejitambulisha kuwa ni swahiba wa Dkt. Magufuri kipindi cha kuomba UTEUZI wa CCM sasa anaimba wimbo huu mpya dhidi ya Mwana CCM Mgungusi....

SISI TUNAO USHAHIDI WA YOTE HAYA, PIA TUNAO USHAHIDI WA KIJANA HUYU WA CCM KWENDA KUWAONA VIONGOZI,WAZEE MAVETERAN WA CCM MOROGORO

1.KANALI MWISONGO
2.DKT NGASONGWA
3.MECK MDAKU
4.CELINA KOMBANI
5.NDG MBWASI

Wote hawa walimpa Baraka kuwa kijana aende akatie nia Malinyi.

TNIMETOA PICHA YA UHUSIANO WA KIDUGU WA CCM NA MOROGORO...TANGU UHURU ILA NINAIONA DALILI MBOFU NA YA HATARI YA WAPENDA UWAZIRI KTK AWAMU IJAYO KUWAWEKEA MIKINGAMO VIJANA WENYE WEREDI KUINUKA KTK SIASA ZA MOROGORO.


TUNAWAANDIKIA HAPA ILI KAMA NINYI NI SEHEMU YA MAAMUZI YA CCM MKOA NA TAIFA MUANZE KUKEMEA MZIZI MPYA WA DHAMBI YA UBAGUZI INAYOPANDWA NA WANA CCM WASIOITAKIA MEMA CCM NA KUJALI NAFASI ZAO.


MOROGORO NI SALAMA NA NGOME YA CCM TUNAWAOMBA KAMATI YA SIASA MOROGORO MSITULETEE WATU AMBAO KWA MACHO TU NI WAHALIFU LAKINI PIA WEREDI NA UHALIFU WA KUGHUSHI MATOKEO NI ALAMA TOSHA KUWA SI MSAADA WALA HZINA YA CCM.

ZUBERI MTEMVU NDIYE MWANA TANU ALIYEPINGANA NA MWALIMU NYERERE KWENYE UCHAGUZI MKUU 1962,MWALIMU NYERERE AKIPEPERUSHA BENDERA YETU YA TANU, ZUBER MTEMVU ALIYEASI TANU AKAPEPERUSHA BENDERA YA ANC.

RAIS JAKAYA KIKWETE NA MWENYEKITI WA CCM AMELIPITISHA JINA LA ABBAS ZUBER MTEMVU KUGOMBEA UBUNGE TEMEKE...

NJAYAGHA NA WANAOKUPIGIA DEBE UNATAMBUA KUWA WAZEE HAWA NGASONGWA,MWISONGO NA MASHISHANGA BADO NI WANA CCM WAAMINIFU KWA KADI NA ITIKADI YAO? UNATAMBUA MZEE MASHISHANGA MWANAE NI MBUNGE WA CDM LAKINI MZEE YUPO MOROGORO NA AMEDUMU NA UAMINFU NDANI YA CCM...

CCM MOROGORO, CHAMA HIKI KINA MISINGI YAKE, HAIJAYUMBA NA DAIMA KINABAKI KIMBILIO LA WANYONGE. TENDENI HAKI NA KUILINDA MALINYI DHIDI YA MMOMNYOKO WA UPINZANI....PELEKENI MGOMBEA ANAYEWEZA KUIFANYA KAZI YA CHAMA KWA WEREDI NA UAMINFU. WALIOSHIRIKI KURA YA MAONI WANAMJUA NI NANI...MSIJIPE UPOFU UTAKAOZAA UHARIBIFU WA USTAWI WA WILAYA MPYA YA MALINYI...MALINYI INAHITAJI KIONGOZI BORA..TUPATIENI KIONGOZI KTK WATATU HAWA BILA GHIRIBA WALA FITINA.

KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
 
Back
Top Bottom