Morgan Heritage...

Morgan Heritage...

donlucchese

JF-Expert Member
Joined
Mar 23, 2011
Posts
17,258
Reaction score
22,129
Salaam Wakuu,

Kwa wale wapenzi wa nyimbo zenye mahadhi ya reggae na riddim lazima mtakua mnawafahamu hawa jamaa wanaoitwa Morgan Heritage. Jamaa hawa ambao ni ndugu wa tumbo moja waliunda kundi lao mnamo mwaka 1994. Kundi hili linaundwa na wanandugu watano ambao ni Peter "Peetah" Morgan, Una Morgan, Roy "Gramps" Morgan, Nakhamyah "Lukes" Morgan na Memo "Mr. Mojo" Morgan.

Ndugu hawa ni watoto wa mkongwe wa reggae jamaica aitwae Denroy Morgan na ni wazi kwamba maji huafata mkondo wake kwani hata baba yao alikua mwimbaji na mtunzi mzuri wa reggae. Wameshatoa takribani album 16 za reggae ambamo katika album ninazo zikubali personally ni album ya Full circle walioitoa mwaka 2005.

Katika nyimbo zao nyingi ninazozipenda, moja ambayo muda wote hua napenda kuisikilizana kuirudia mara kwa mara ni nyimbo ya Morgan Heritage - I'm Coming Home - YouTube huwa inanipa hisia kama najiona ndio nimemuacha wife nimeenda kutafuta maisha sehemu ya mbali na haieleweki nitarudi lini na kama nitafanikiwa ama la. kwa kweli jamaa wako poa.
 
Gramps morgani ametoa ngoma Kali inaitwa PEOPLE LIKE YOU........

Hawa jamaa hatari sana.
 
Back
Top Bottom