marcoveratti
JF-Expert Member
- Sep 21, 2017
- 1,106
- 1,948
Nimebahatika kuziangalia hizi zote, kitu cha kwanza kabisa, hazifanani, ni muvi tofauti ila ukija kwenyr uandishi, huyu aliyeandika hii Squid Game, ameiandika kiuandishi kabisa.
Muvi A: Series ya Money Heist inaanza vizuri sana, inakufanya uvutike na kutamani kuiangalia zaidi lakini baadaye, udhaifu unaonekana waziwazi, muvi inaanza kukaa kitoto, kuna matukio ambayo ni very simple kutokea, mwandishi akiyaandika kirahisi sana.
Duniani, pesa hazilindwi sana kama karatasi za kutengenezea pesa. Ni bora uingie benki ya dunia uibe mabilioni ya dola lakini si karatasi za kutengenezea pesa, hizo zina ulinzi mkubwa mno kwani ukifanikiwa kuzipata, wewe ni bilionea. Lakini kwenye hii series, yaani watu wanaingia kirahisi sana, huo ni udhaifu wa kwanza, halafu wa pili, watu wanaanza kuingizia mapenzi humohumo.
Jaribu kufikiri tu, sehemu kama hiyo ambayo inatakiwa milango yako yote ya fahamu iwe wazi, kinatokea kitu kama hicho, kiuhalisia, hamna kitu kama hicho.
Tokyo alibahatika kuondoka, akatoka humo, kilichotokea baadaye, akarudi tena[emoji16]yaani very simple tu, ni kitu abacho hakiwezi kutokea hata kidogo.
Ukifuatilia yule mama aliyekuwa akifuatilia hilo suala, naye alikuwa na udhaifu mkubwa. Hafuatilii kama mfuatiliaji, anafuatilia kama muigizaji na ndiyo maana watu wanasema kama kazi ya kumfuatilia angepewa Mahon wa Prison Break, series ingeishia season ya kwanza tu.
Nimeangalia muvi nyingi za kipelelezi, ila sijamuona mtu anayefuatilia kesi kama yule mama, mwandishi amekuwa dhaifu sana upande huo, hakutaka kumpa nguvu, alimpa nguvu Profesa.
Tazama Prison Break, Scofield alikuwa na akili sana, naye Mahon alikuwa na akili mno, alipewa nguvu sana na mandishi na ndio maana wakisumbuana sana.
Kwa Rate, kule IMBD nimeweka 6/10.
Nakuja kuichambua na Squid Game.
Uandishi wa Squid Game nineupenda sana. Kabla ya kumpa character nguvu kwanza tuambie kwa nini anapewa hizo nguvu.
Hii series imezungumzia zaidi mtu masikini, mwenye madeni ambaye hawezi kuyalipa, ili kuyalipa, anakuwa tayari kufanya lolote lile kwa ajili ya pesa.
Watu wenye madeni wamechukuliwa na kuwekwa sehemu moja. Kila mtu mbali na madeni, ana matatizo binafsi, huyu mama yake mgonjwa, yule hivi na vile.
Hapo mtazamaji unaona kabisa huyu mtu anahitaji pesa. Michezo ambayo wameicheza, ni kweli inasumbua kichwa, mbele ya bastola, huku ukiwa unatetemeka, unaambiwa uufanye mtihani fulani.
Hii muvi imenikumbusha muvi nyingi kama Escape Room na Saw. Games walizocheza ni za utotoni, ila kwa kipindi hiki zimejaa hatari.
Vitu ambavyo vimeifanya series hii kupendwa ni namna michezo ilivyochezwa, ukatili uliofanyika na hata mwisho kugundua babu ndiye mratibu, ni kitu ambacho hakuna mtu yeyote aliyehisi hilo.
Dhima kubwa ya series hii ni kukuonyesha mtu mwenye matatizo ya pesa, yupo tayari kufanya lolote lile ilimradi kupata pesa hata kama litagharimu maisha yake.
Endapo hii series ingetoka mwaka 2008 ilivyoandikwa, isingevutia kama sasa hivi kwa kuwa bado hatukuwa na muvi za namna hii, ila kwa sasa ni lazima tuipende kwa kuwa tumeona vitu ambavyo tumeviona kwenye Escape Room, Saw na nyinginezo.
Kwa kule IMBD nimeipa Rate ya 7/10.View attachment 1966185
Dah Squid Game nimelianza jana Money Heist ilikuwa bora pale mwanzo Professor alikuwa mchanganuaji kweli wa mambo lkn sasa imekuja kiovyoo sana je QUEEN OF THE SAUTH .Lakini Squid Game inanitia mashaka haya mambo yapo Duniani wale maiti wanakatwa viungo vyote muhimu baadae nafikiri wanawawachoma moto hakuna sijamaliza naendelea na burudani langu nilikua naangalia HOUSE OF CARDS nimeliacha kwanza ni siasa tu lkn kuna mauwaji ni kweli wana siasa kuua ni jambo la kawaida tu.Unajua sanaaa[emoji110]
Dah Squid Game nimelianza jana Money Heist ilikuwa bora pale mwanzo Professor alikuwa mchanganuaji kweli wa mambo lkn sasa imekuja kiovyoo sana je QUEEN OF THE SAUTH .Lakini Squid Game inanitia mashaka haya mambo yapo Duniani wale maiti wanakatwa viungo vyote muhimu baadae nafikiri wanawawachoma moto hakuna sijamaliza naendelea na burudani langu nilikua naangalia HOUSE OF CARDS nimeliacha kwanza ni siasa tu lkn kuna mauwaji ni kweli wana siasa kuua ni jambo la kawaida tu.
Nakazia ni zaidi ya utopolo yani ni upumbavu.Money Heist ni utopolo..
Credit to Nyemo Chilongani.Umecopy kwa nyemo chilongani toa credit
Watu wa Prison Break wanajaribu sana kuipinga Money Heist na series zao za kijinga. Kwanza story ya Squid na Money Heist hazina hata uhusiano hii comparison hata sijui inatoka wapi au kwa kua nao wamevaa masks?
Money Heist >>>>>Prison Break, nipo Tengeru Arusha karibu na shule ya Akheri njooni mniuwe.
Re-read my commentKwahiyo Prison break ni ya kijinga?...
Sio kwamba Kwenye Money heist Pesa zilikuwa zinalindwa sana bali walikuwa wameshikilia watu wa muhimu sana Kama Gavana Na wale wengine ambao walikuwa watoto wa Matajiri na Mabalozi,Money Heist Hukuielewa Mimi nimeangalia zote Hila Money heist Ni Top Sababu Yenyewe ina Account zake Mfano ya insta ina zaid ya 12M followers hapo Ujaweka za sehem nyingne ,Halafu Squid Game ni Mini series kama Wandavision hila Money Heist Ni moto wakuotea mbali zile theory za Profesor ni Noma ,kitu Kilichobeba Squid Game ni kwamba wamekuja na Idea Mpya Ya gamesNimebahatika kuziangalia hizi zote, kitu cha kwanza kabisa, hazifanani, ni muvi tofauti ila ukija kwenyr uandishi, huyu aliyeandika hii Squid Game, ameiandika kiuandishi kabisa.