GE2025 Monalisa anaendelea kukabia kooni issue ya Mpina kugombea urais ACT

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

tonicimmobility

JF-Expert Member
Joined
Jun 17, 2025
Posts
493
Reaction score
1,038
Leo amekuja na mpya tena alivyokuwa East Africa radio kuhusu kuvaa fulana yenye picha ya Hyati JPM, mpina atachomoka kweli wakuu?

Monalisa Joseph Ndala, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa ACT-Wazalendo Dar es Salaam, anazimwaga lawama za kutosha kwa mgombea wa kiti cha Urais kupitia chama chao Luhaga Mpina kwa kusema yeye kama mgombea hakupaswa kuvaa nguo yenye picha ya aliyekuwa kiongozi kwenye chama kingine.

Soma pia: Mpina awekewa pingamizi na mwanachama mwenza kugombea urais kupitia ACT WAZALENDO

Your browser is not able to display this video.
 
Shida ya watu kama hao, hawatumii akili bali mihemko.

Moina ni Mzalendo. Anakubaliana na yeyote alie mzalendo. Mimi nikivaa picha ya Nyerere na niko CUF ntakua na matatizo?

Hizo ni fikra mgando. Tunataka uzalendo na akili ndio ziongoze taifa sio upinzani na ushabiki wa kama ma ccm yaliyo mengi. Ili mradi ugali wao upo yanashabikia kila kitu.
 
Hoja ya msingi ipo. tararibu za Chama zimekiukwa, hivyo Mpina hana sifa ya kuwa mgombea wa urais kupitia ACT wazalendo.
 
Dada yuko kisheria zaidi.Mpina kaja kuidhohofisha ACT
 
Mara ya kwanza alikuwa sahihi.

Ila hapa hana point. Ameanza wivu wa kike.

Watu husoma vitabu vya Nyerere na wanatumia sera zake na CDM huwa wanatumia sauti ya Nyerere (Ya Mabadiliko) kwenye Majukwaa na wanaeleweka.

Huyu anataka chama kifanye mambo ya familia na sio ya nchi.
 
Tanzania Kuna Sheria zinazofuatwa? Kama tumeamua kuvunja Sheria kwa manufaa ya kibinafsi au kundi la watu wachache tuache maisha yaendelee tu
Hoja ya msingi ipo. tararibu za Chama zimekiukwa, hivyo Mpina hana sifa ya kuwa mgombea wa urais kupitia ACT wazalendo.
 
Wale wale... Yaleyale...!!!
 
Wakati wa urais wa Nyerere nchi ilikuwa ya chama kimoja. Watanzania wote walihesabiwa kuwa wanachama wa TANU au AFRO-SHIRAZ na baadae CCM. Magufuli alikuwa kiongozi wa chama pinzani na ACT-WAZALENDO. Kuvaa mfano wake ni kumtukuza mtu ambae hakukipenda chama chake cha sasa. Mtu afanyae hivyo anaonyesha kuwa mapenzi yake bado yako CCM.

Amandla....
 
Mawazo yenu yanafafana.

ACT sio chama cha familia, ni cha Umma.

Mtu anaweza akawa ACT akamtolea mfano mzuri wa mtu aliyeko CCM. Na hii ndio siasa.

Acheni ubinafisi ili chama kipanuke.
 
Mawazo yenu yanafafana.

ACT sio chama cha familia, ni cha Umma.

Mtu anaweza akawa ACT akamtolea mfano mzuri wa mtu aliyeko CCM. Na hii ndio siasa.

Acheni ubinafisi ili chama kipanuke.
Acha hizo, hata mimi sijamuelewa Mpina kuvaa tshirt ya Magufuli huku akiwa mgombea wa ACT. Ni sawa na mfanyakazi wa Cocacola kuvaa tshir ya Pepsi hadharani. Huyo Mpina amejigeuza mgombea binafsi ndani ya ACT.
 
Wenzako wanatafuta kura wewe baki na ufinyu wako wa mawazo.
CDM walikuwa wanatumia sauti ya nyerere kwenye majukwaa yao kutafuta kula, walikuwa ni CCM?
 
Wenzako wanatafuta kura wewe baki na ufinyu wako wa mawazo.
CDM walikuwa wanatumia sauti ya nyerere kwenye majukwaa yao kutafuta kula, walikuwa ni CCM?
Kura zipi, ni wapi cdm walikuwa wanatumia sauti ya Nyerere. Cdm sio chama cha wazee, watatumia vipi sauti ya mtu wa karne iliyopita kusaka kura? Kura kwa tume ipi kwanza?
 
Siku tundu lisu akivaa t-shirt ya Samia akiwa mahakami ndipo wataelewa maoni ya huyu dada.
 
Kura zipi, ni wapi cdm walikuwa wanatumia sauti ya Nyerere. Cdm sio chama cha wazee, watatumia vipi sauti ya mtu wa karne iliyopita kusaka kura? Kura kwa tume ipi kwanza?
Nimejua wewe una umri mdogo.

Moto wa Mabadiliko wa 2015 ulikuwa unatoka wapi?
 
Avae akiwa nyumbani kwake sebuleni jioni wakati anakunywa kahawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…