Momba, Mbozi: Basi la New force lapata ajali

Momba, Mbozi: Basi la New force lapata ajali

Donatila

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2014
Posts
8,269
Reaction score
25,308
index.jpeg

index.jpeg

Kuna taarifa ajali ya New Force eneo la mpaka wa Momba - Mbozi eneo la kwa wachina, hakuna vifo lakini kuna majeruhi.

Taarifa zaidi tutawaletea kadiri tutakavyo pata.

========

Ajali imetokea asubuhi ya leo ya basi la kampuni ya New Force yenye namba za usajili T 226 DJQ iliyokuwa inatokea Tunduma kuelea jijini Dar Es Salaam katika eneo la mpaka wa Momba na Mbozi eneo la kwa wachina.

Hakuna vifo, kuna majeruhi kadhaa, pia madereva wanaotumia barabara ya Mbeya Tunduma eneo la Senjera ya pili rolly imekata njia hivyo kuna foleni, juhudi za kuondoa gari zinaendelea.
 

Attachments

  • index.jpeg
    index.jpeg
    58.5 KB · Views: 39
Kuna taarifa ajali ya New Force eneo la mpaka wa momba - mbozi eneo la kwa wachina hakuna vifo lakini kuna majeruhi. Taarifa zaidi tutawaletea kadiri tutakavyo pata.
Duuuh haya mabasi sasa tutaogopa kuyapanda
 
Ni nini jamani!! ni vipuri vyao fake, tairi, uchaw... , laana, kukosa umakini, mgomo baridi wa watumishi au nini hasa!!! nakumbuka kipindi kile Scandinavia nazo zilizidisha ajali kumbe matairi yalikuwa ya ovyo ovyo hayana viwango
 
Yaani kukuta Bus la New Force limepata ajali ni mara chache sana, jamaa wako makini sana na habari za barabarani
 
Yaani kukuta Bus la New Force limepata ajali ni mara chache sana, jamaa wako makini sana na habari za barabarani
Momba miezi miwili ajali mbili, Morogoro ajali moja, miezi miwili ajali tatu, jamaa wako makini sana na habari za barabarani!
 
Usipandw new force,wanakimbia sana barabarani dar mbeya saa kumi na mbili jioni washafika wakat wengine wanaingia saa mbili usiku
 
limelala halijaanguka hilo.....leta taarifa kamili kwanza
 
Haya mabasi yatakuwa na Degedege hali inayopelekea kupata kifafa hawapo Barabarani.
 
Tena hili bus ndo alipanda yule aliyejiteka afu akashukia Mafinga akiwa hajitambui.
 
Back
Top Bottom