Mokiwa ana tuhuma za jinai, Askofu wa jimbo atishia kuweka nyaraka hadharani

Uko deep sana mkuu wewe ni karani pale hekaluni nini..?

Aweke hadharani anaficha nini kwani ni mkataba wa IPTL huo..?
Hapana mkuu mimi ni mpenda haki na muumini wa kawaida kabisa.Niliumizwa sana na tabia ya Kanisa kugeuzwa shamba la bibi lakini hatimaye mwanga umeanza kuonekana na nikuhakikishie tu mkuu kila kitu kitawekwa wazi kwani mapambano haya yaliongozwa na vijana wenye "kiu ya haki" na kwa mbelee namuona aliyekuwa askofu akisajiliwa mahakama ya mafisadi.
 
Maaskofu Mungu anawaumbua kwa unafiki wao, walilinyamazia suala la zanzibara na upongeza uchaguzi ulikuwa huru na haki, sasa Mungu anasema nao ili tuwajue walivyo, Lusekelo wa upako yake yalianza hadharani, akaja yule wa KKT Malasusa na kuvunja ndoa ya muumini wake kwa kutembea na mama mchungaji, now Mokiwa, acha waumbuke tu Mungu alisema ukiwa vuguvugu atakutapika.. Bado mwingine sijui anguko lake litakuwa namna gani.
 
huyu askofu pamoja mimi sio wa huko lakini ni kichwa na namkubali sana na ndio maana anatafutwa kila kona.
yeyey kwanza haogopi kutamka anachokiamini na hata maubiri yake huwa yanawajenga watu.
tatizo kinachokuja tunawatafuta watu kwa kuwachafua na ubinafsi wetu na tunashindwa kujua au kufahamu umuhimu wa mtu katika jamii jinsi anavyotegemewa
 
Huyu ni tapeli kama matapeli wengine, ila anapita katika mkondo wa dini.

Sijawahi kumuamini toka nimfahamu.
 
huyu askofu pamoja mimi sio wa huko lakini ni kichwa na namkubali sana na ndio maana anatafutwa kila kona.
yeyey kwanza haogopi kutamka anachokiamini na hata maubiri yake huwa yanawajenga watu.
tatizo kinachokuja tunawatafuta watu kwa kuwachafua na ubinafsi wetu na tunashindwa kujua au kufahamu umuhimu wa mtu katika jamii jinsi anavyotegemewa
Alimshupalia sana "kipara" february kipindi kileeee cha kuelekea general election teh..teh...teh..!
 
Mokiwa kakosea sana tena sana!
Kwa vile zilishakuja tuhuma tena kutoka kwa viongozi wenzake ambao nao ni wa kiroho angekaa pembeni tu ili waliomtuhumu kama ni uongo basi ingejulikana baadae. Hapa tutoe mfano wa mke wa Kaisari kwamba tuhuma pekee!

Kuna story moja kuhusu uongozi wa dini ambapo alitokea mtu mmoja tena kwenye 'inner cycle' akidai yeye ndio kiongozi halali huku akimtuhumu aliyekuwepo kuwa sio. Baada ya huyu aliyetuhumiwa kuona hivyo wala hakuanza kubishana au kutoa maelezo bali alichukua maamuzi tofauti. Aliamua kuondoka machoni pa waumini na kwenda kuishi mbali kabisa (remote areas) na wale watu wa kule matokeo yake wakashtukia uwezo wake mkubwa wa kiroho na kuanza kumfuata. Sasa huyu aliyejidai ndiye kiongozi huku nyuma kila kitu kikamharibikia na kukwama na baada ya miaka kama miwili ikabidi waumini waweke mkakati wa kumfuatilia yule wa kwanza na kumshawishi arejee ili kuwanusuru.
Na hapo ndipo ilijulikana ni nani kiongozi wa kweli na muongo.

Nimetoa hadithi hii muhimu kama kipimo kizuri kwenye maongozi ya Imani, haya ya kukataa kujiuzuru, na kusemana kwenye media hayahakisi sifa za kiroho. Pia askofu mzima kuongelea eti katiba ya Kanisa ni aibu kubwa maana katiba kubwa kabisa ni Biblia na Biblia inafundisha sifa za kiroho ambazo ni unyenyekevu kwa yeyote hata aliyekuudhi, kujishusha nk.

Mokiwa akipitia hapa naomba ani PM nimpe ushauri zaidi kumuondolea aibu.
 
Dhana ya uwajibikaji kwa mtu mweusi ni msamiati uliokosa maana kabisaaa, si kwa wanasiasa tu sasa dhana hii ni ngumu kutafsirika hata kwa viongozi wa dini, kuna mambo mm huwa nawaelewa sana kanisa catholic. Kwa utajiri wa RC hz siasa za kuchaguana zingeingizwa kanisa la RC nahisi kanisa hilo lingekua limesambaratika vibaya. Dr. Mokiwa angejitafakari tu katika muktadha wa kulinda heshima yake binafsi na ya kanisa angekubali kukaa pembeni, kwa kiongozi wa callibre yake kutuhumiwa tu kwa kashfa kama hzo zinatosha kumfanya akae pembeni, but that shall not be possible to we Africans......... Cc Yahya Jammeh
 
KATIBU Mkuu Kanisa la Anglikana
Tanzania, Johnson Chinyong’ole
amesema aliyekuwa Askofu wa
Dayosisi ya Dar es Salaam, Dk
Valentine Mokiwa anakabiliwa na
mashitaka ya jinai kwa kuingia
mikatiba mibovu na matumizi mabaya
ya fedha za kanisa makosa
yanayoangukia kuvunja sheria za nchi.
“Hatujakurupuka kuchukua hatua,
ushahidi wote tumeshauwasilisha kwa
vyombo vinavyohusika serikalini, sisi
tumetimiza wajibu wetu, hivyo
tunaviachia vyombo vinavyohusika
kufanya kazi yake katika eneo hilo la
ubadhirifu wa fedha,” alisema
Chinyong’ole.
Alifafanua kuwa wakati wanaenda
kutangaza uamuzi wa kumvua uaskofu
Dk Mokiwa juzi kanisa la Ilala, walienda
kutoa taarifa kwa msajili wa vyama
ambaye ndiye anayesajili makanisa,
lakini pia wameshatoa taarifa katika
ofisi za Wakala wa Usajili, Ufilisi na
Udhamini (RITA) kwa ajili ya kuchukua
hatua za kisheria.
Alitaja sheria alizovunja Dk Mokiwa
kuwa ni sheria ya miunganiko ya
wadhamini sura ya 318, sheria ya ardhi
namba 4 ya 1999 na sheria ya mipango
miji sura ya 355 kwa kuruhusu
mabadiliko ya matumizi ya ardhi katika
shamba la kanisa la Mtoni Buza na
eneo la Kanisa la Mtakatifu Mariam
Kurasini.
“Sisi tunasubiri mrejesho kutoka ofisi
ya Waziri Mkuu, Rita na kwa Msajili wa
vyama vya kiraia,” alisema katibu mkuu
huyo wa kanisa la Anglikana Tanzania.
Alifafanua kuwa katika mashitaka 10
anayokabiliwa nayo, shitaka la tatu
ndilo ambalo ni la ubadhirifu wa mali
za kanisa ndilo ambalo linaifanya
serikali kuingilia kati.
Alisema makosa ya Dk Mokiwa
yanahusisha pia kughushi na akatoa
mfano wa kuingia mikataba kwa
kuwatumia watu ambao si wadhamini
wa kanisa hilo wakati sheria inamtaka
atumie wadhamini wawili
wanaosimamia mali za kanisa, pamoja
na kutumika kwa muhuri bandia wakati
sheria inasisitiza muhuri unaotumika ni
ule wa moto.
Katibu Mkuu huyo alisema ripoti ya
tume iliyoundwa kuchunguza tuhuma
dhidi ya askofu hiyo yenye kurasaa 173
imewasilishwa pia serikalini ili vyombo
vinavyohusika kufuatilia tuhuma hizo
viweze kujiridhisha wakati vinapoenda
kuchukua hatua.
“Hakuna mtua aliyeonewa, wala
kuchafuliwa, hizi ni tuhuma za
ubadhirifu wa mali ya kanisa, lazima
vyombo vya dola vihusike hapa,”
alisema katibu mkuu huyo na kuongeza
kuwa serikali ndio inayotakiwa
kuchukua hatua kwa sababu tume
iliyoundwa na kanisa imeshaweka
hadharani ushahidi kwa lengo la kuokoa
mali za kanisa.
Amevunja kiapo cha utii Kwa hali hiyo
jambo hilo tayari wameliwasilisha kwa
msajili wa vyama ambaye ndiye msajili
wa kanisa hilo na pia wamewasilisha
suala hilo kwa wakala wa vizazi na vifo
(Rita) kwa kuwa sheria ya nchi
iliyovunjwa ni ya udhamini.
Akizungumza na gazeti hili jana,
Chinyong’ole alisema kwa mujibu wa
katiba ya kanisa hiyo ya mwaka 1970
iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2004,
pamoja na Dk Mokiwa kugoma
kung’oka madarakani baada ya
kuvuliwa madaraka yake na askofu
mkuu Dk Jacob Chimeledya, kwa sasa
katiba haimtambui kama askofu wa
kanisa hilo.
Alisema kabla ya marekebisho ya
mwaka 2004, sinodi ya dayosisi ndio
ilikuwa inakuwa na tamko la mwisho
dhidi ya askofu wa dayosisi, lakini
baada ya marekebisho kufanyika
askofu mkuu ndiye msimamizi wa
maaskofu wote wa dayosisi na ana
mamlaka ya kuwastaafisha pale
wanapokiuka katiba ya kanisa.
“Dk Mokiwa amenyang’anywa utawala
wa dayosisi ya Dar es Salaam, katiba
inampa mamlaka askofu mkuu
kuwastaafisha maaskofu ikibainika
wameenda kinyume cha sheria na
katiba ya kanisa,” alisema
Chinyong’ole.
Aliongeza kuwa baada ya kumvua
utawala wa dayosisi, hatua inayofuata
ni taratibu zingine za kisheria ambazo
zitashughulikiwa na kanisa ikiwa ni
pamoja na kumbana Dk Mokiwa
kukiuka kiapo chake cha kumtii askofu
mkuu wa kanisa.
Alisisitiza kuwa Dk Mokiwa amevunja
kifungu namba 7 cha katiba ya kanisa
hilo kuhusu kiapo cha utii kwa askofu
mkuu aliposema
“Nakubali na kuahidi kumheshimu na
kumtii, kama inipasavyo, askofu mkuu
wa kanisa Anglikana Tanzania...
watakaofuata baada yake...”
Katibu mkuu huyo alisema Dk Mokiwa
kutokana na hatua yake kugoma
kujiuzulu baada ya kushauriwa na
askofu mkuu Tanzania, amevunja kiapo
cha utii kwa katiba ya jimbo
kinachosema,
“Ninaahidi pia kwamba nitakubali
kujiuzulu au kujitoa kwa hukumu yoyote
itakaoniachisha madaraka na mapato
yanayohusika na dayosisi hii
nitakayohukumiwa wakati wowote
baada ya uchunguzi wa kutosha wa
barza lenye kbali cha sinodi ya kanisa.”
Pia amevunja kiapo cha utii kwa katiba
ya dayosisi kinachosema “Ninaahidi pia
kwamba nijiuzulu wakati wowote kama
ikiazimiwa na Askofu Mkuu wa Kanisa
Anglikana Tanzania kwa mujibu wa
katiba ya kanisa na ya Dayosisi.”
Wachunguzi wa mambo wanabainisha
kuwa kugoma kwa Dk Mokiwa kung’oka
madarakani kutaleta mtafaruku
mkubwa ndani kanisa hilo kutokana na
baadhi ya makanisa katika Dayosisi ya
Dar es Salaam kuunga mkono uamuzi
wa askofu mkuu na wengine
wanamuunga mkono Dk Mokiwa.
Juzi, Askofu Mkuu wa Kanisa la
Anglikana Tanzania, Dk Jacob
Chimeledya alimvua uaskofu mkuu wa
Dayosisi ya Dar es Salaam, Dk Mokiwa
baada ya mashitaka 10 yaliyofunguliwa
na walei 32 wa kanisa hilo katika
dayosisi hiyo kumtuhumu kwa ufisadi
wa mali za kanisa hilo.
Uamuzi huo ulichukuliwa baada ya
Askofu Mokiwa kugoma kujiuzulu kama
ilivyoshauri nyumba ya maaskofu
ambayo ilimkuta na hatia ya ufujaji wa
mali za kanisa hilo na kukiuka maadili
ya kiuchungaji ambayo yalibainishwa
kwenye ripoti ya uchunguzi ya kanis
ahilo nchini.
Hata hivyo, Dk Mokiwa amegomea
uamuzi huo kwa maelezo kuwa, mwajiri
wake ni Sinodi ya Dar es Salaam
ambayo ndio yenye uamuzi wa kumfuta
kazi na si askofu mkuu au askofu
mwingine yeyote wa kanisa la
Anglikana Tanzania
Mods naomba hii ipandishwe pale juu inajibu maswali ya wengi
 
Askofu mkuu wa Anglikana ametishia kuweka hadharani nyaraka zote zinazomuhusisha Mokiwa na ufisadi wa mali za kanisa.

Chanzo: Mwananchi na Habari Leo
Yaani askofu mkuu hajui kuwa kufumbia macho jinai na kutoitolea taarifa kwa vyombo vya dola pia ni kosa la jinai?
Unakuwa "accessory to a crime".
 
Alimshupalia sana "kipara" february kipindi kileeee cha kuelekea general election teh..teh...teh..!
hilo ni kweli tena hakuangalia kuwa ni muumini wake yeye alichomoza na analoliona linafaa.
hata kumtoa kwake katika uongozi kipindi kile ni kutokana na waliokuwa wanachagua hawakuona mbali na huitajika wake kwa jamii.
mapungufu kila mtu anayo lakini kwa level kama za huyu jamaa ni kwamba kanisa linajipaka matope hata kama ni kweli watafute jinsi ya kulitengeneza.
 
Back
Top Bottom