Moja ya Sababu Zinazochangia Tanzania Kutoendelea.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Moja ya Sababu Zinazochangia Tanzania Kutoendelea..

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mtoboasiri, May 5, 2011.

 1. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #1
  May 5, 2011
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Wana JF,

  Naamini aliewahi/anaefanya kazi kwenye utumishi wa umma atakuwa ameona hiki nitakachokiweka hapa hadharani.


  • Maamuzi mengi mabovu serikalini na mashirika ya umma yamekuwa yakihusishwa na ufisadi, japo ni kweli kuna maamuzi ya kifisadi lakini kuna mengi yanayotokana na watendaji kutokuwa na uwezo kwa kazi walizopewa kufanya.
  Binafsi nawafahamu watu niliosoma nao na ambao leo wanashikilia nafasi kubwa lakini uwezo wao ukiwa ni mdogo mno. Vyeo vinatolewa kwa kufahamiana, si kwa ujuzi au uwezo wa mtu, katika mazingira hayo si ajabu maamuzi yanayotolewa yakiwa na matokeo mabovu kwa kuwa mtoa maamuzi HAJUI MAANA NA MATOKEO YA MAAMUZI YAKE.
  Majuzi nilisikia kisa cha kina mama fulani wakimsuta mwenzao -aliteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa wizara fulani. Huyu mama Katibu Mkuu alikuwa anajisifia kuwa ni utendaji wake bora ndio uliomfikisha hapo, lakini wenzake (class mates wake UDSM) wakamwambia "digrii yako ni ya chupi, na tunajua umekuwa unalala na kina nani hadi kufika hapo ulipo, kwa hiyo usitwambie kitu tutakuumbua bure". Mama Katibu Mkuu akanywea. Habari hii ilinifanya nifunguke macho, nimefanya kazi sehemu nyingi serikalini na sekta binafsi. Mabosi wangu Sekta ya umma wengi wamekuwa na uhusiano na wakubwa, na kwa kuwa utendaji wao unaonekana wazi kuwa mbovu - na bado walipewa hizo nafasi na hawatolewi japo inajulikana kuwa hawazimudu - basi atasamehewa mtu atakaeamini kuwa sifa ya kuteuliwa nafasi ya uongozi serikalini na mashirika ya umma si UWEZO bali UNAMFAHAMU nani.

  • Ukija sekta binafsi, kuna watu wanojulikana kuwa ni wafanyabiashara waliofanikiwa kwenye biashara zao. Lakini kila utawala mpya ukija biashara zao ama zinaanguka ama kutetereka (Unakumbuka Karibu Hotel enzi za Mzee Ruksa, Ngurdoto enzi za Mkapa?). Iweje mafanikio ya biashara yaendane na utawala fulani ukichukulia kuwa huwa hakuna mabadiliko katika sera za kiuchumi zaidi ya mabadiliko ya sura za watawala? kwangu mimi hii inaashiria jambo moja: "Patronage" ndio inayowaibua na kuwaangusha hawa "wafanyabiashara"

  • Kwa nini makampuni ya kimataifa yanaajiri watoto wa vigogo wasiojulikana wanachokifanya kwenye makampuni yao kama si kupata access ya kuwaona wakubwa na ku-influence maamuzi serikalini (wakijua udhaifu wa watendaji) kwa manufaa ya haya makampuni? Kwa mfano Barclays Tanzania waliunda cheo cha "Deputy MD" ambacho hakikuwepo kum-accommodate bwana mmoja. Umuhimu wake ulipokwisha wakamtosa, jamaa mara ya mwisho namuona alikuwa anaendesha Bar - iweje Deputy MD wa Barclays akose kitu mbadala kinachoendana na uzoefu wake wa uongozi?
  Mifano hii kwangu inaniambia kuwa tuna matatizo makubwa kwenye nchi yetu kiasi kwamba mafanikio ya mtu yanategemea unamfahamu nani alie na nafasi ya uongozi. Kama hali hii haibadilishwi, Nchi kama Comoro na Burundi zitakuwa mbele yetu muda si mrefu.
   
Loading...