Moja ya sababu zilisopelekea 'Armed Struggle' Africa ni kukomeshwa kwa vyama vya siasa.

TAWA

JF-Expert Member
Jun 23, 2013
3,667
1,566
Inawezekana viongozi mliopo hamfahamu, nataka tu kuwakumbusha kuwa, moja ya sababu uliyompelekea umwagaji damu kwa baadhi ya mataifa ya Africa wakati wa harakati za kusaka uhuru ni kukomeshwa kwa vyama vya siasa vilivyoundwa na waafrika weusi. Pia kupiga marufuku harakati zozote za kisiasa katika makoloni hayo.
Kwa waafrika, mataifa kama vile Mozambique, Angola, zimbabwe, South Africa na mengine, yote yalipata uhuru kwa njia ya mtutu wa bunduki.
Walifanya hivyo mara baada ya kuona wakoloni 'weupe' wanakandamiza haki za watu weusi huku wakiwaziba midomo kwa kuwanyima haki nyingi za kisiasa.
Sababu nyingine ni baadhi ya wakoloni hasa Wareno walikuwa wakidhani makoloni yao ni kama mikoa yao katika nchi zao, (overseas provinces) hivyo wakawa wanajiona wao ni watawala wa milele katika maeneo hayo. Kuwatoa ilihitaji siyo mazungumzo tena, bali ni mtutu wa bunduki na ujasiri wa watu.

My take:
Watawala wa hii nchi yetu tumshauri vizuri kiongozi mkuu wa taifa hili. Tusimwambie tu yale anayoyapenda kuyasikia, tumshauri hata vitu vichungu ambavyo pengine vitamuumiza. Washauri wa kiongozi mkuu wa nchi yetu lazima wawe majasiri kumshauri vizuri kiongozi mkuu.
 
umeandika kitu cha maana Sana asee
Ila hawa miungu watu hawataelewa kamwe... Misri wana jeshi Bora all Africa lkn kuna waasi kilasiku wanawaua polisi na wanajeshi wao
 
Uvumilivu wa mateso ukizidi huwa ni maafa.
Liwalo na liwe
 
umeandika kitu cha maana Sana asee
Ila hawa miungu watu hawataelewa kamwe... Misri wana jeshi Bora all Africa lkn kuna waasi kilasiku wanawaua polisi na wanajeshi wao
Yetu macho
 
Back
Top Bottom